NGOJA NILEWE 7
MTUNZI: Mbogo Edgar
WHATSAPP +255743632247
ILIPOISHIA 6
Naaaam Sebastian akiwa amesha jihakikishia kwa macho yake, na kuujuwa ukweli wote, walirudi kibamba, na kumsimulia baraka kila kitu, huku akimweleza kuwa, kwa sasa mpango wake ni kutafuta kazi, “sikia Seba wewe ni mwanaume, cha msingi achana na yale yaliyopita, we fanya kama ayajatokea, anza kupambana upya, bahati nzuri elimu unayo, unaweza kupata kazi haraka” alisema Baraka, siku iliyofuata Sebastian akiwa na matumaini ya kupata kazi, akaanza kuzunguka kwenye maofisi kutafuta kazi, huku akitoa sifa zake kuwa alisha wai kufanya kazi ya uhasibu. ,…… . ENDELEA……..
Lakini mambo yalikuwa tofauti kidogo, kila alipoenda waliitaji awe na cheti cha chuo, alicho somea fani ambayo anataka kuajiliwa nayo, yani kama ni mhasibu awe amesoma chuo cha uhasibu, ukweli hali ya ajira ilikuwa ngumu sana, tofauti na miaka mitatu nyuma, kipindi yeye ametoka mkoani kuja kuingia kazini moja kwa moja, licha kuzulula mwezi mzima, lakini akupata ata kazi ya kukaribisha wageni.
Ikaongezeka miezi mingine mitatu, Sebastian akiangaika kiguu na njia kwenye maofisi na viwanda mbali mbali, pasipo mafanikio, tena kuna sehemu nyingine walimweleza kuwa, “yani tulikuwa tunaitaji mtu kama wewe, lakini umechelewa kidogo, tumeajili jana tu” hii ilikuwa kama mkosikwa Seba, ambae sasa akakubari kushindwa, “kaka sina ujanja inabidi nirudi songea, japo sijuwi watu watanitazamaje, maana narudi nikiwa ovyo zaidi ya nilivyoondoka, lakini nyumbani ni nyumbani” Seba akimweleza Baraka, “ni kweli kaka nivyema kama ukirudi kwanza nyumbani ukaanze upya, usiwezi kujuwa, maana maisha popote” alisema baraka, na hapo likaja jambo moja tu, nauri atatoa wapi.
Naam baada ya kuwaza na kufikiri kwa muda wa week nzima, ndipo siku moja akapata wazo la kwenda kuomba msaada FSC, kwenye kiwanda alicho wai kufanyia kazi, lengo ni kwenda kumwona mzee Ngimba au meneja, wazo ambalo lilimsaidia sana, maana akupofika pale, alipokelewa vizuri na wenzake, ambao walisikitika kwa kumwona akiwa katikahali ile, wote kwa umoja wao walimchangia kila mmoja alicho kuwa nacho kama mtu alikuwa na elfu moja, mbili au tano, walichangia, na kumkabidhi, kitu ambacho akukitegemea, ni kwamba, licha ya kupata elfu ishilini ambayo ingetosha nauri ya kufikia songea, pia kwa utaratibu wa wamiliki wa kiwanda hiki cha viatu vya wazi, wenye hasiri ya nchi ya jilani, ya #mbogo_land, walimtunzia mshahara kwake wa mwezi ule wa mwisho kufanyia kazi pale FSC, ambao ulikuwa ni elfu alobaini na tano, pia alikuta barua kadhaa toka kwa mama yake na ndugu mbali mbali, ambao walikuwa wanaitaji misaada, akiwepo ndugu yake Geroge, mtoto wa baba yake mkubwa.
Akiwa na jumla ya tanzania shilingi elfu sitini na tano, Sebastian alirudi kibamba na kumweleza Baraka mafaniko yake ya kule alikokwenda, yani kigamboni kwenye kiwanda cha FSC, “kaka huo ni mwanzo mzuri” alisema Baraka, ambae alionekana kufurahi sana, baada ya kuona rafiki yake akiwa amepata fedha ambayo itamfikisha songea.
Siku ile angalau Seba stian alilala kwenye nyumba ya wegeni, ambapo alipata japo kausingizi kazuuuri, na siku ya pili alienda mjini kununua nguo mbili tatu, kwaajili yake, na pia zawadi wa ndugu na jamaa, pamoja na mama yake kisha siku ya pili akapanda basi na kuelekea Songea, ambako aliingia mida ya saa mbili za usiku, mfukoni akiwa amesalia na elfu kumi nambili pekee, akakodi taxi kuelekea mji mwema kwa kaka yake George, baada yalipa nauri ya taxi, akabakiwa na elfu kumi tu.
Mwanzo George alimpokea vizuri sana, na kwa furaha kubwa, lakini mala baada ya kumwona ndugu yake alivyopauka, na aliposimuliwa kilicho mkumta ndugu yake huyo, ndipo vituko vilipoanza katika siku ya pili tu, ya uwepo wake pale nyumbani kwa George, nyumba ambayo yeye ndie alikuwa analipia kodi, na ata vitu vya ndani alinunua yeye.
Kwanza kabisa siku hiyo ya pili, Sebastian akiwa amshinda pale nyumbani anawaza jinsi ya kwenda kijijini kupeleka zawadi kwa mama yake, anajikuta akiwa peke yake huku mwenyeji wake, akiondoka na kumwachia nyumba kama ilivyo, ndan akukuwa na chakula chochote, akalazimika kununua baadhi ya vyakula, ili aweze kujipikia.
Sebastia akiwa katika mji huu mwenye baridi kali, na mtaa wenye nyumba moja moja, aliweza kuona majilani wa George, asa wakike walioshinda nyumbani, wakiwa wanaendelea na kazi zao, katika hali ya utulivu na baridi, Sebastian anajikuta anaanza kuwa tamani wanadada wale, ambao ajajuwa kama ni wake au ndugu wa wapangaji wenzie na George, lakini ata hivyo, kutokana na mwonekano wake, wa choka mbaya, akuweza kufanya lolote, sababu ata wale wanawake, awakumtazama ata kidogo, ukweli Sebastian usingeshishwa kumfananisha na mtu alie tokea vijiji vya mbali sana, kwa jinsi alivyo onekana kwa wakati ule, usingefikilia kuwa alitokea mjini dar es salaam.
Sebastian ambae siku ile alishinda nyumbani, aliweza kujionea mambo mengi sana, ikiwa pamoja nawanawake ambao japo awakuwa wenye kuvaa nguo fupi za kubana, kama wale wa dar es salaam, lakini walivutia machoni pa Sebastian, ambae mida ya saa kumi na mbili jioni alitembea kidogo maeneo ya jilani, japo akuwa ameizowea mtaa hii, lakini alijuwa kuwa awezi kupotea.
Seba alitembea taratibu, huku anawaza jinsi atakavyo anza kutafuta kazi, katika mji huu mdogo wenye ajira chache, na kati ya izochache nyingi uwa niza hali yachini, zenye vipato vidogo na vya chini, japo kwa sasa akuwa na chaguo lolote, ingemlazimu kufanya kazi yoyote, ili aweze kujikimu kimaisha, kuliko kurudi kijijini ambako angemtia unyonge mama yake.
Naaam saa mbili za usiku, ndio muda ambao, Seba aligeuza kurudi nyumbani, maana tayari baridi ilikuwa kali, na njaa ilianza kumtafuna, na wakati Sebastian, akiwa anakatiza kwenye safu ya maduka, yenye bar ndogo, iliyoandikwa MAMA EVA, akaliona gari moja aina ya Nissan Patrol, likiwa limesimama karibu na bar ile, yenye duka pembeni, siyo kwamba lilegari lilimvutia sana Sebastian ambae akuwa na uwezo ata wakuomba lift, ila niwatu wacache waliokuwa wamekaa kwenye vitu vyao, mbele ya ile bar, wakipata vinywaji vyao taratibu kabisa, katika meza tano zilizokuwepo pale mbele, ya ile bar ndogo, ambazo kila moja ilikuwa na watuzaidi ya wawili, kama siyo wanne basi watano, wote wakimchanganyiko, wakike na wakiume.
Sebastiana anavutiwa na meza moja, ambayo alikaa mwanamke mmoja tu, ambae licha ya kuwa alikuwa amekaa, lakini usingeweza kukosa kuona kuwa, nimrembo na mzuri sana, ni kutokana na alivyovaa rangi ya ngozi yake, japo tukuweza kuiona sura yake, aliyokuwa ameizuwia kwa gazeti, alilokuwa analisoma, huku chupa kubwa ya wine toka #mbogo_land ambayo imetengenezwa kwa nazi, wine anayo ipenda sana, ikiwa mezani, na grass pembeni, ilimtamanisha sana Sebastian, ata hivyo Sebastian aliona kuwa, aya mambo aya kumhusu, wachapambane na hali yake, akuwa na uwezo wakupata wine anayo ipenda, wala kukaa na wanawake wazuri kama awa, hivyo anaondoka zake kuendelea safari ya kurudi nyumbani.
Huko nako kulikuwa moto, kwanza kabisa ile anafika nyumbani, akakutana na viatu pea mbili mlangoni, moja ikiwa niraba za George, lakini pea ya pili ilikuwa ni kanda mbili, mlango ulikuwa umefungwa, hivyo akasikilizia dakika kadhaa pale nje, hapa kuwa na sauti yoyote ndani, ilikuwa kimya kabisa, na akukuwa na dalili ya kuwepo kwa jambo linalo endele, Sebastian akagonga kwa hodi, kabla ya kuingia ndani, “nani?” iliuliza sauti ya kavu ya George, ambae nikama akupendezwa na ujio wa mgeni huyo, “mimi Seba” alisema Sebastian, nakusubiri jibu toka ndani, “ingia” alisema George, kwa sauti ile ile kavu, ni wazi akupenda mtu aingie wakati ule, lakini kutokana na hali ya baridi na njaa aliyokuwa nayo Seba, akaamua kuingia ili akajionee muendelezo wa mpango wa kula na ikiwezekana achukuwe ata koti moja la George ajilinde na baridi.
Seba aliingia ndani, ambako alimkuta George akiwa amejilaza kitandani na mwanamke mmoja hivi, ambae Sebastian akuwa anamjuwa, waliokuwa wanatazama video bila sauti, ni wazi awakutaka mtu wanje asikie sauti ya video ile, nazani nikutokana na aina ya video, waliyokuwa wanaitazama, “hooo! kumbe hupo nashemeji kaka, vipi miangaiko lakini, naona uliniacha peke yangu” alisema Sebastian, mala baada ya kuingia ndani, na kumwona mwanamke huyo, ambae kiukweli siyo kwamba, ni wivu au ni chuki, ila kiukweli mwonekano wa mwanamke huyu, aukuwa wa kulidhisha, pengine ungeweza kusema ni chakula cha simba mzee, badala ya ule msemo wa simba akizidiwa, ula shika ata mijusi, “ndiyo bwana, siunajuwa hapa, mjini mwanaume uwezi kushinda nyumbani, uwezi kukaa bila kazi” alisema George, kwa namna flani ya kujinasib, huku yeye na mwanamke alie kuwa nae, macho wakiwa wameyaelekeza kwenye video.
Atakama George akumaanisha, lakini ukweli ni kwamba, Sebastian alijishtukia kama vile anasemwa yeye, “ni kweli bwana George, ata mimwenyewe kiukweli, najisikia ovyo sana, kukaa bila kazi, maana nilizowea nikitoka asubuhi na rudi zangu jioni” alisema Sebastian, huku anataazama jiko, ambalo lilikuwa pembeni pasipo dalili ya kupikwa kitu chochote, akaona kuwa kama atochangamka basi anaweza kulala na njaa, “tena hapa mjini usiangalie sijuwi nimesoma mpaka form six, utatoka kapa” alisisitiza George, ambae mapaka dakika hii, Seba akuwa anajuwa kama anafanya kazi gani, maana siku zote yeye ndie aliekuwa anamhudumia kwa kila kitu.
Seba ambae litaka kuchukuwa jiko lile, ili akawashe moto, kwaajiliya maandalizi ya chakula cha jioni ile, mala akasikia harudu nzuri ya chakula mlandani, akkatupa macho mezani na kuona bakuri flani lililofunikwa vizuri, akajuwa kuwa kulikuwa nachakula ndiomaana George akuangaika kuandaa chakula, hivyo kwa bakuri lile, hapakuwa na aja ya kupika chakula kingine, hapo Seba akaona itakuwa vyema kama atawapisha wapendanao awa wawili, na yeye akatulie nje mpaka shemeji yake huyo ambae kukiachilia rangi yake ya chungu cha zamani, pia alikuwa mwembamba, na miguu kama vifuniko vya kiyetulia tofari za udongo, amwone akitka nje, ndipo aningie kuja kula chakula alicho kiona mezani, chakula ambacho, pengine ndio sababu ya kaka yake huyu, kumpenda mwanamke huyu, ambasie ata yeye na ukame alionao, asinge weza kuthubutu, kupititisha mwiko wake kwenye kwenye chungu chake.
Lakini kabla Seba ajatoka nje, George akamuwai, “Seba ngoja nikutambulishe kwanza, huyu ni shemeji yako, anaitwa Adija, anaishi hapo mbele ya maduka ya mama Eva” alisema George, huku wote wakiwa macho kwenye Video, “nifurahi sana kukufahamu shemeji, naimani kesho tukikutana barabarani utanikumbuka” alisema Sebastian huku anatazama tazama mle ndani kama angeona jacket, alivae kuzuwia baridi, lakini akuliona, “ata mimi shemeji nimefurahi, karibu sana songea” alisema Adija akijitaidi kutabasamu, lakini akiwa amejawa na aibu, nazani ni kurokana na kile ambacho walikuwa wanakitazama wawili awa, “asante shemeji” alisema Sebastian ambae akuweza kuona kabisa jacket au sueta la kuvaa, “George, unajaketi niazime” aliuliza Seba, “kwani we ukujuwa kuwa huku sonea kuna baridi, mi ninalo moja tu, na nitalivaa kumsindikiza shemeji yako, alisema George, bila kupepesa macho, hakika ukiwa auna kitu, ni mtihani kwa walimwengu.
Sebastian aliejisikia vibaya kwa jibu la kaka yake George, alijichekesha kwa aibu, huku anatoka zake nje, ambako pasipokujari baridi kali iliyokuwa inanyunyiza, alienda mojaa kwa moja mpaka kwenye barabara, iliyokatiza mbele ya nyumba yao, safari hii akifwata barabara, kuelekea upande wakulia, ambako mita hamasini mbele upande wakushoto, ndio kuna nyumba kubwa yenye fensi, na geti kubwa, ambayo licha ya kuwa na taa zilizo angaza kila kona ya eneo lila kwa ndani, lakini ilikuwa kimya kabisa, ungesema hapakuwa na mtu anaeishi ndani yake.
Sebastin, ambae miezi kadhaa iliyopita alikuwa na maisha mazuri, ambae akuwa mtu wakujiuliza ata lala saangapi au nitapata wapi koti la baridi, alitembea taratibu huku kimenywa na baridi, dudu imemsimama kwa kumbu kumbu ya kile alicho kiona ndani ya chumba cha George, akijuwa fika kuwa, lazima wawili wale wakimaliza kutazama video yao, lazima wangefanya majaribio, kwa kile walicho kiona, na sasa Seba alikuwa na miezi zaidi ya sita ajagusa kitumbua, wala kukiona kwamba.
Naam Seba alijikuta anafika mwisho kabisa wa mtaa ambako apakuwa na dalili ya mwendelezo wa makazi ya watu, zaidi ya mashamba ya maindi, yaliyokuwa yana subiria kuvunwa, “mh! nisije kukamatwa na fisi” alijisemea Sebastian huku anageuka na kuanza kurudi alikotoka, ambako alifika mida ya saa tatu na nusu, na kwabahati mbaya sana, licha ya kumkuta George akiwa ametoka kumsindikiza Adija, lakini alikuta tayari amesha maliza chakula kilichokuwepo kwenye bakuri, na siyo kwamba alikimbaliza chote, ila kilibakia kidogo, ambacho kisingeweza kulika, maana kilikuwa kimetiwa maji, yani ni kama mlaji alipomaliza alinawia mle kwenye bakuri, “dah! Huyu jamaa bwana, yani wali na dagaa nyasa, anaufanya hivi, akujuwa kama sijala” alijisemea Sebastia, ambae sasa alitakiwa aanze kupika.
Baada ya kuwaza na kukujifikilia sana, akaamua kuchemsha viazi viwili, moja ya vyakula alivyonunua asubuhi, ata George aliporudi, alimkuta bado anasubiria viazi viive kisha achemshe chai, “kaka ukujuwa kama sijala nini, naona chakula umetia maji?” aliuliza Seba katika hali ya kawaida tu, “kwani uliletewa wewe” jibu la George, lilikuwa kavu sana, hapo Sebastian akuongeza neno, akatulia zake akimwacha George akipanda kitandani na kujifunika shuka.
Sebastian aliona wazi chuki na ukosefu wa upendo, wa kaka yake, lakini akutaka kuweka akilini maana alimini kuwa ata pata kazi hivi karibuni, na kuhama hapa kwa kaka yake, hivyo aliendelea kuchemsha viazi na baadae chai, alipomaliza akala na kujilaza, kitandani huku akipiga mahesabu ya namna kesho atakavyo ipeleka siku yake.********
Naaam, siku ya pili Sebastian aliamka mapema sana, na kujiandaa, kisha akaondoka zake kuelekea mjini, akiwa na mfuko wa zawadi ambao alikuduia akautume kuelekea kijijini Namabengo, wakati huo kwa barabara ya mji mwema apakuwa na dala dala, hivyo safari ilikuwa ni kwamguu, kipindi hicho siyo tu, songea ata dar es salaam apakuwa na usafiri wa boda boda, kwahiyo kutembea kwake aikuwa ajabu kwa mtu yoyote, maana uwe na fedha usiwe nayo, wote mnge utwanga mguu.
Wakati anakatiza sehemu akamwona Adija akiwa anafagia uwanja, nje ya nyumba moja kubwa hivi, yeye akaendelea na safari yake, na kabla ajafika mbali, akaliona gari lile lile aliloliona jana jioni pale kwenye ile bar ndogo, ambalo wakati lina mpita, likiwa lime shushwa vioo vya milango ya mbele, akamuona dereva wagari lie, ambae alikuwa ni mwanamke, yani siyo tu mwanamke mrembo ila alikuwa ni nzuri aswaaaa, tena ni kitu kweli kweli, ambae licha ya kuendesha gari lile aina ya Nissan patrol, lakini umri wake ulionekana kuwa sawa na wake, na kama walizidiana basi aikuwa zaidi ya miaka mmoja au miwili.
Sebastian alimtazama mwanamke, ambae ni wazi kabisa ndie yule wa jana pale kwa mama Eva, japo hapa songea alikuwa mgeni, lakini sura yake aikuwa ngeni sana machoni pake, lakini yule mwanamke mbae pia alimtazama mala moja tu Sebastian akuangaika kumtazama mala ya pili, akatazama mbele na kuendelea kuongoza gari lake, kwa mwendo wa taratibu, ni kutokana na hali ya barabara hii yenye emashimo na mawe.
Sebastian alikumbuka wakati akiwa na maisha mazuri, hakika angesimamisha gari lile na kumwuliza yule mwanamke walionana wapi, maana licha ya ugeni wake hapa songea, ila pia miaka minne iliyopita, seba alikuwa amesoma hapa songea, kwa muda wa miaka sita, na alikutana na wanawake wengi sana waliokuwa wanasoma songea Girls, ruvuma sekondari na luhuwiko, pia chuo cha uuguzi na chuo cha ualimu cha matogoro, kwahiyo ingekuwa lahisi kwakekukumbushana na pengine kupata msaada wa kupata kazi, lakini mwonekano wake uli mnyima kujiamini.*******
Naaam mizunguko ya Sebastian iliisha saa kumi na mbili ndio muda mbao, alikuwa amefika nyumbani, huku tayari akiwa amesha tuma zawadi za mama, kwakuoitia mabus yanayoenda namabengo, pia alisha zunguka kwenye ofisi na viwanda kuomba kazi, pasipo mafanikio, sehemu zote akipewa majibu yanayo fanana, kwamba awakuwa wanaitaji mfanya kazi kwa wakati ule, labda aje pindi wakitoa matangazo ya nafasi za kazi, hii ilikuwa ni kwanafasi za kazi za maofisini, na baadae alipopata wazo la kuomba kazi za kwenye kiwanda, muda ulikuwa umeshaenda, hivyo akapanga kuwa kesho yake ange jaribu upande wa viwanda, ata kama zina mshara mdogo, lakini ingesaidia.
Pale nyumbani siku hii yale ambayo aliwai kudogo, nakukuta ndugu yake bado ajamleta yule dada wakazi wawatu, akapika haraka mpaka saa mbili za usiku alikuwa amesha kula, huku George akiwa ametulia anatazama TV akuwa na mpango wowote wakula, lakini ile anapanda kitandani tu, mlango ukafnguliwa na Adija akaingia, na bakuri kama lajana.
George alimkaribisha mpenzi wake, akala chakula alicholetewa, huku Seba yupo kitandani anatazama TV, maana alimini kuwa endapo ata toka nje kidogo tu, ingemgharimu masaa kadhaa, lakini uweli ni kwamba, aikusaidia ata kidogo, maana baada ya George kumaliza kula tu, akapanda kitandani huku akimshika mkono Adija ambae alijilegeza na kujiangukasha kitandani toka kwenye sturi.
Ilikuwa ni ajabu sana kwa Sebastian, ambae aliamini kuwa mwanamke mwenye heshima zake, asingekubari kupanda kwenye kitanda kile wakatikuna mtu mwingine juu yake, lakini huyu, akiwa mwenye uso mkavu kabisa, akapanda kitandani kitana cha futi nne kwa sita.
Kiunyonge kabisa, Sebastian akainuka toka kitandani, na kuvaa kandambili zake na kutoka nje, ambako maana leo akwenda mbali, kutokana na uchovu aliokuwa nao, wakuzulura mchana kutwa songea mjini, uchovu ambao ulimsababishia usingizi wa mapema, baridi la pale nje, lili mfanya atamani maisha ya kulala gengeni kwa baraka, au kurudi kijijini, kitu ambacho alichukulia kama kukata tamaa, na pia ni matumizi mabaya ya juhudi za mama yake za kumsomesha.
Sebastian aliendelea kukaa pale nje, huku anatembea tembea kama askari alipo kwenye lindo, akipunguza baridi na usingizi vilivyo mkabiri, mida ya saa nne kasoro, aliliona lile Nissan likipita uswa wa nyumba ile aliyofikia, na kwenda mpaka kwenye ili nyumba yenye geti geti kubwa, na kupiga honi mala mbili, kisha geti likafunguliwa, na mwanamke mmoja alieonekana kuwa ni dada wakazi, kisha gari likaingia na yule mwanamke akalifunga, sijuwi kwanini kila alipoliona gari ili, lilimkumbusha gari lake na maisha yake ya zamani, roho ilimuuma sana
Naam ilimgharimu masaa mawili, akipigwa na baridi, ni bahati wakati ulesongea apakuwa nambu wengi, asa msimu kama huu wabaridi, hapakuwa na mbu kabisa, vinginevyo, ingekuwa shida kwa Sebastian, ata saa nne na robo, alipowaona wawili awa wakitoka nje na kusindikizana, kuelekea upande wa madukani, na yeye akapata nafasi ya kuingia chumbani, ambako alikuta siyo tu chumba kina harufu, ila kitanda kilikuwa kimevulugwa vibaya sana.
Chakushukuru ni kwamba, Seba alikuwa amechoka sana, hivyo alipata usingizi mapema kidogo, na kulala fofo mpaka saa moja kasoro za asubuhi, ambapo alikurupuka na kujiandaa, kwa kuwa akuwana fedha ya kula akachemsha viazi na kunywa chai, kisha akaondoka zake, kuelekea mjini.
Naaam hali ya ajira upande wa kiwandani, ilikuwa vile vile, katika kampunzi zote alizoenda, majibu yalifanana, “tumeajiri week iliyopita, uwa tunajari mwisho wa mwezi tu” hayo ndiyo majibu aliyo yapata kila sehemu aliyoenda, na kwa udogo wa mji mji huu, mpaka kufika saa kumi mbili alikuwa amesha maliza sehemu zote, na kuanza safari ya nyumbani, ambako nako kulikuwa moto, lakini alipanga awai akale ata kama Adija akifika yeye awe tayari amesha kula, “lakini mbona yule mwanamke juzi akuja kabisa, inamaana baada ya mimi kuja ndio ameanza ratiba kuja na kuchelewa kuondoka, au wananikomoa mimi” aliwaza Sebastian, ambae licha ya kuwaza hivyo akuwa na namna zaidi ya kuendelea kukaa pale kwa George.*******
Ukweli nikwamba, leo Seba alichelewa kufika nyumbani, maana alimkuta tayari Adija yupo ndani, tena mbaya zaidi walifanya wanacho kifanya bila kificho, seba leo alicheka kupita kiasi, alikaa pale mlangoni akiskiliza kinachoendelea huko ndani, matamanio yalimshika akuwa na lolote la kufanya, akuwa na uwezo wa kupata wanamke, ambae angemwelewa, na kumpa dhamani ya kumiliki penzi lake.
Mambo yalivyo mzidi Seba aliinuka na kujietembeza kidogo, lakini baridi na uchovu vilimrudisha tena mlangoni, ata walipomaliza na kutegemea kuwa sasa wanaondoka, lakini akashangaa kuona wanaendelea kuganda mle ndani, na ata wakati anasema wanatoka sasa hivi, mala akasikia wanataka kuendelea kupeana dudu, ndipo alipoamua kutembea tembea kidogo, ndio wakati ule ambao aliliona gari la yule mbrembo likwa linaingia pale kwenye jumba kubwa. ******
Naam mala baada ya George kuondoka na Adija, Seba aliingia ndani, na kukula viazi vitamu kisha akaingia kulala, ambapo licha ya uchovu aliokuwa nao, lakini alichelewa sana kupata usingizi, maana alitumiamuda mwingi kuwaza jinsi mwenyeji wake, alivyo mtendea, ungesema ni mtu ambae aliwai kumtendea vibaya siku za nyuma, lakini kinyume chake ni kwamba, Sebastian ndie alie sababisha George kuishi katika nyumba hii, hapa mjini, inamaana amesahau kila kitu, na kumfanyia aya.
Wakari anawaza hayo, mala Mlango ukafunguliwa na akaingia “hivi George, aiwezekani ukanivumia kwa siku chache, ili kuliko kufanya hivi, wakati hapa tunaishi wawili” alisema Sebastian, kwa sauti ya upole yenye kusihi, “kwani mimi nilikuambie ufanye upumbavu wa kupoteza kazi?” alisema George, kama ambae akujari malalamiko ya ndugu yake, “George, siyo kwamba nilipenda kupoteza kazi, ni mambo ambayo mtu yoyote yanaweza kumkuta” alisema George, kwa sauti yenye kutia huruma, “kila mtu vipi bwana, mi siwezi kufanya ujinga kama huo, we fanya fanya uondoke hapa, uoni kama unanibana sana?” aliuliza George kwa dharau.
Sebastian aliumia sana kwa maneno ya kaka yake, asa akikumbuka jinsi alivyo kuwa anajitaidi kutaia shida za kaka yake huyu, huyu, ambae leo hii ana mtolea maneno kama aya, “sawa George inawezekana nilifanya upumbavu, lakini kumbuka ata uwezo niliokuwa nao mwanzo, siyo toka utotoni, nilitafuta nikapata, naamini kama sikufanya makosa, nitatafuta tena na nitapata, najuwa uwezi kuzingatia msaada niliokupa, kwakuwa nimepoteza, tuombe mungu, kikubwa uzima” alisema Seba, kwa sauti moja yenye kuudhunika sana, kama una roho yenyepesi, unaweza kudondosha mchozi.
Lakini uwezikuamini, George akumjari kabisa, alikuwa mkavuuuu, “utapara wapi bwana, kwaniujuwi kuwa bahati aiji mala mbili” alisema George kwa sauti kavu kama vile alikuwa na ugomvi, huku anapanda kitandani na kujifunika shuka, dakika kumi mbele tayari alianza kukoroma, huku akimwacha Sebastian anawaza la kufanya.
Ukweli Sebastian alikuwa katika wakati mgumu sana, maana aligundua kuwa ata mbegu za wema alizo zipanda, nzimegeuka mbigiri, na sasa baada ya kula matunda anajikuta anachomwa na miba hiyo, lilikuwa ni somo kubwa sana kwake, kwamba unapokuwa nakazi wewe ni ndugu wa wote, lakini unapopoteza kazi, unakuwa mwenyewe, labda na mama na baba pekee ndio wanakuwa wakwako.
Baada ya kuwaza sana, George ana pata jibu la kwamba, ni vyema kesho jioni akaelekea kijijini, kwa mama yake, ambako angekaa mpaka karibu na mwisho wa mwezi kisha arudi mjini kuwania nafasi ata za viwandani, ambazo zingemsaidia kusalia hapa mjini, na kuendelea kutafuta kazi nzuri zaidi, huku anaendelea na kazi za viwandani, lakini siyo kukaa hapa kwa kaka yake, ambae alionyesha wazi akuitaji yeye akae hapa, “yani mtu anakula wali na kutia maji unaobakia, wakati mimi nakula viazi asubuhi na jioni” aliwaza Sebastian, huku anausaka usingizi.
Kwenda nyumbani ni swala la msingi, lakini atayakabiri vipi maneno ya wanakijiji wa namabengo, baada ya kuiona hali yake ya sasa, japo swala ilo alikukwepeka, kama ilivyokuwa kule alikotoka, lakini sasa lazima ajitaidi watu wasimwone jinsi atakavyoingia, na siku ya pili ajidamkie shambani, na hiyo iwe ratiba yake, mpaka atakapokuja mjini, kuangallia nafasi za kazi za viwandani, ambazo malanyingi uwa zinatoka mwishoni mwa mwezi, na katika hesabu zake, kijijini angekaa kwa week mbili tu.*******
Naaam siku iliyofuata ilikuwa ni ijumaa, siku ambayo ilianza vibaya sana kwa Sebastian, Seba, ambae mfukoni alikuwa na shilingi mia tano tu, njaa ili anza kumutafuna mapema sana, saa mojana robo tayari alikuwa ameanza kuhisi njaa, na viazi viwili vilivyo bakia, alikuwa amaesha vimaliza jana usiku, kwa kuwa alikuwa na mpango wa kushinda hapa mpaka jioni ndipo aelekee stendi, Sebastian ambae akuona mpango wowote wa chai kwa mwenyeji wake, akaona nivyema atumie akiba yake, kutafuta japo maandazi manne, ambayo moja lilikuwa linauzwa shilingi ishilini, ili kupooza njaa, na alinunua manne, kama akiba, pengine kaka yake pia angekunywa chai, maana akutaka kuyaweka moyoni yale maneno yajana, George akuwa na wasi wasi wakumaliza nauri, maana nauri mpaka namabengo ilikuwa ni shillingi mia mbili.
Sebastian akiwa amevalia kaptula yake ile ya jana na tishert lake lile lile la jana, akatoka zake nje taratibu, akimwacha kaka yake amelala, sababu alisha yajuwa maeneo ya kununulia maandazi, akatoka moja kwa moja nje na kuifwata barabara ya inayokatiza mbele ya nyumba yao, na wakati huo huo akaliona geti la ile nyumba ya jilani yao likiwa linafunguliwa, na dada ambae kwa mwonekano ni dada wakazi, japo akuwa kama yule mwanamke wa George, huyu alikuwa anatamanisha, ni wazi boss wake siyo tu kuwa mwenye fedha, ila pia alikuwa ni mwenye upendo, maana matunzo bila upendo, inakuwa ni jela yenye afadhari, na hapo likanekana gari ndogo aina ya Toyota Crester, rangi ya maziwa jipya, kwa kipindi kile ningesema ni lakisasa, Seba kuona vile akapunguza mwendo, maana alijuwa kuwa lazima angelazimika kulipisha lile gari, ambalo ni kweli lilishika uelekeo ule ule wa kule ambako yeye angetakiwa kuelekea.
Naam Sebastian akalitazama lile gari lilikuwa lina kuja kwa mwendo wa taratibu, huku dereva wake akiwa niyule mwanamke mrembo sana, ambae mpaka sasa akuwa anajuwa aliwai kumwona wapi, ila ni kweli alisha wai kumwona, labda kilicho changia asimkumbuke, ni ile tabia yake ya kuto kujichanganya na wanawake wakati akiwa anasoma, pengine asingekuwa wa waina hiyo angeweza kumkumbuka mwanamke huyu, na kujitambulisha yeye mwenyewe na kujipatia kazi.
Sebastian akiwa anamtazama yule mwanamke huku anajaribu kuvuta kumbu kumbu, mala akamwona yule mwanamke pia anageuza kichwa kumtazama, macho yao yakakutana, yule mwanamke akuonyesha dalili yoyote ya kumfahamu Seba, maana lazima angejitabasamulisha au kupunga mkono, japo alisha poteza hadhi ya kufnyiwa hivyo na watoto warembo kama huyu.
Lakini akiwa anaamini mwanamke yule ajamkumbuka, kama yeye anavyo tamani itokee, mala akaliona gari linasimama usawa wa ile sehemu ya kuingilia kwao, kisha yule dada akatazama kule kwao, kama vile kunamtu anaitaku kumwita au anamsubiri, Seba akushangaa maana ni kaida kwa wenyeji kufahamiana, hivyo akageuka nyuma, kutazama anae suburiwa, maana yule mrembo siyo tu kusimama, ila pia alitazamaupande ule wanyumba aliyofikia Sebastian, akaona kuwa licha ya kuwepo kwa watu wengi sana mbele ya nyumba ile, wanaoendelea na kazi zao, huku wakipiga macho ya chini chini, kulitazama gari la mrembo, lakini hapakuwa na ata mmoja, ambae alikuwa na mwelekeo wa kuwa alikuwa anasubiriwa na dada huyu, Sebastian akahisi kuwa anae subiriwa alikuwa ndani, hivyo yeye akaona kuwa akuwa na bundi ya kuendelea na safari yake, maana asingeweza kusubiri muda wote.
Lakini kila alipozidi kusogea, ndipo alipoona kuwa, nikama yule dada alikuwa anamtazama yeye kwa umakni sana, kama vile kuna ukweli alikuwa anautafuta, au kuna jambo alikuwa anaitaji kujilidhisha, ata Sebastiana mbae nae mapig ya moyo yalianza kumwenda mbio akiingiwa na tamaha ya kwamba itokee miujiza dada huyu, awe anamsubiri yeye, alipolifikia lile gari akajaribu kusalimia, “habari za leo” hiyo ilikuwa ni sauti toka kwa wote wawili, ikiwa ni mgongano wa salamu, na kuwa kama kiitikio cha wimbo flani, wote wakacheka kiicheko cha chini chini, huku wote wawili wakiwa na dalili za kujawa na aibu nyusoni mwao wakishindwa kutazamana usoni.
Tabasamu lile kwa upande wa yule dada, lina zidi kumfanya awe mzuri zaidi, asakutokana na vidimples kwenye mashavu yake, “samahani kaka, kuna kitu nilitaka kukuuliza” alisema yule mwanamke mrembo ambae ata sauti yake ilikuwa nzuri na tamu, ambayo ingefaa kukata kiu jangwani, kuwakiburudisho wakati wa safari, “bila samahani dada yangu, unaweza kuuliza tu” alisema Sebastian huku akijikaza kidogo, hapo mdada akaongeza tabasamu, “samahani kaka yangu, hivi unandugu yako anaishi dar es salaam?” aliuliza yule dada, kwa sauti flani tamu, yenye unyeyekevu kiasi, huku tabasamu likiendelea kushamili, na uso wake ukionekana kusubiri jibu kwa hamu kubwa.
Hapo Seba akacheka kidogo, maana alijuwa fika kuwa akuwa na ndugu yoyote dar, ila yeye ndie ndugu pekee wa ndugu zake, alie wai kuishi dar, tatizo akujuwa kwanini ameulizwa swali ilo, “hapana dada yangu, akuna ndugu yangu anaeishi dar, labda kama mama ajawai kunieleza” alisema Sebastian ambae alikuwa anasubiri huyu dada amalize ili na yeye amuulize alisomaga sekondari gani, ili uwe mwanzo wa kuelekeza shida yake ya kuomba msaada wakupata kazi, “kweli una uhakika, kaka yangu?” aliuliza yule dada, huku akionyesha kuto kumwamini Sebastian, kwa jibu alilompatia.
Itaendelea
Your Thoughts