ACETAMIN-220...(04)
MTUNZI:BARAKA GEOFREY
0652089642
ILIPOISHIA..........
"Nimewaletea chakula mchangamshe kidogo matumbo" Habiba aliwaambia akitoa chakula cha take away kwenye mfuko alioingia nao, kwa pamoja walikula na kisha Habiba alianza mazungumzo..
"Bite unaweza kwenda kupumzika chumbani kuna vitu tunataka kuongea"
"Abaki tu kwani ana shida" Bosco aliongea, Allen alimpiga jicho fulani kali Bosco
"Ok basi baki" Habiba alisema
"Hamna shida ngoja niwapishe" Bite aliongea
"Hapana baki tu" Habiba alisema
Bite alikaa chini...
"Ok guys kuna mambo ya msingi sana nataka niwaambie nadhani wote hamnifahamu ila mimi nawajua vizuri ni watu wa usalama wa taifa Tanzania labda Bite ndio nimemjua leo"
ENDELEA..........
"Mimi naitwa Habiba Hussein ni secret agent wa Kenya nipo kwenye mission ya siri sana ambayo nadhani mnaweza kunisaidia na mimi pia nikawasaidia...."
"Mbona sikuelewi hatuhitaji msaada sisi...." Allen aliingilia
"Tulia basi kaka amalize kuongea" Bosco alimwambia akiwa ameanza kukereka
"Miaka mitatu iliyopita idara yetu ilipata tetesi kuwa kuna kambi ya kijeshi isiyo rasmi imeanzishwa nchini na kundi la kigaidi linaloitwa 'maharib alhuriya' ikimaanisha freedom fighters (wapigania uhuru) kwa kushirikiana na baadhi ya vigogo serikalini, lengo ni kujenga misingi yao katika ukanda wote wa Afrika mashariki.... ni kundi lilioanzishwa mwaka 2010 huko nchini Somalia waanzilishi wake wakiwa ni Al qaeda ambao pia walianzisha Al Shabaab mwaka 2004, baada ya kupata taarifa hizo mimi na wenzangu watatu tulipewa kazi ya kuhakikisha kama taarifa hizo ni za kweli na kulichimba hili swala kiundani kuhakikisha kuwa wahusika wote wanatiwa hatiani na kikundi hicho kinafutiliwa mbali katika harakati zetu wenzangu wawili waliuawa kwahiyo tumebaki wawili mimi na mmoja yupo kule kwenye kambi yao kama undercover agent" Habiba alitulia kidogo ili maneno yake yawaingie vyema, hakuna aliyeongea kila mmoja alikaa kimya akitafakari
"Sawa mimi nimekuelewa lakini umetujua vipi mimi na Allen?" Bosco aliuliza
"Wewe Bosco nilikufahamu mda mrefu kwani tulikuhisi kama mmoja wa mtandao wa kundi hilo Kenya na hivyo nilianza kukufuatilia ndipo nikagundua wewe ni mpelelezi wa Tanzania, japokuwa ulikuwa nchini kinyume cha sheria ila niliachana na wewe kwani haukunihusu"
"Na ofisi yangu umeijuaje?" Bosco alimuuliza akimshangaa mdada yule kwani aliwaza uwepo wake Kenya ni wa siri sana lakini kumbe alifahamika vyema
"Hahahaha sio kuifahamu tu ila nimeingia mara kadhaa" alijibu Habiba akitabasamu
"Umeingia? umeingiaje?" Bosco aliuliza maswali mfululizo hakuamini kabisa
"Hayakuhusu hayo Bosco" alijibu Habiba
"Lazima uniambie umefikaje ile sehemu ya siri" Bosco alijibu akikunja sura kwa hasira
"Huwezi kuniamuru Bosco nimeingia na huna cha kunifanya na wala sikwambii nimeingiaje" Habiba aliongea maneno ya kibabe lakini akitabasamu tu, Bosco alijihisi kuchoka mno
"Na kuhusu wewe Allen mwenzangu alinipa taarifa ya kuwa kuna jasusi wa Tanzania anakuja kumfuatilia mtu ambaye amesafirishwa na hao freedom fighters ameniambia mtu huyo aliyesafirishwa ni muhimu sana kukamilisha lengo lao Afrika mashariki yote, hivyo mipango imepangwa ili kumuua huyo jasusi asigundue chochote hivyo nilianza kukufuatilia toka siku unaingia ili nikulinde lakini sikutaka kuingilia moja kwa moja, nilitaka kupima uwezo wako wa kujilinda, kwa kiasi unajitahidi kwani uliweza kuwagundua wanaokufuatilia na kuwashikisha adabu ila bado haukuwa makini kwani haukunigundua mimi ambaye nimekufuatilia mda wote uliokuwa Kenya, so next time ongeza umakini" Habiba alimwambia
"Kwanini ulikuwa unanifuatilia" Allen aliuliza
"Ili niwasaidie mkiwa hatarini kama leo"
"Na kwanini utulinde?"
"Ili mnisaidie kumaliza mission yangu na mimi niwasaidie pia"
"Haiwezekani tuondoke Bosco" Allen aliongea akianza kuinuka kwenye kiti
"Sikiliza Allen sio kwamba nakubembeleza kunisaidia ila mission zetu zinahusiana wewe jiulize kwanini hai freedom fighterswaanze kukufuatilia wakuue? unajua mgonjwa alikuwa nani na anapelekwa wapi? na pia kaa ukijua hawataishia Kenya tu bali lengo lao ni kusambaa ukanda wote wa Afrika mashariki na nchi yako ikiwepo, fikiria mara mbili" Habiba alimwambia kwa ukali
"Mda mwingine jifunze kuamini watu Allen" Bite alimwambia kwa upole, Allen alijikuta anarudi tena kwenye kiti
"Sawa mimi nipo tayari kufanya kazi na wewe kama lengo ni kuokoa nchi zetu kwani Tanzania na Kenya ni ndugu" Allen alisema
"Mimi pia" Bosco naye alisema
"Na mimi pia" Bite naye alisema na kumshangaza kila mtu kwani walijiuliza atasaidia vipi misheni yao wakati hana mafunzo yoyote
"Msinishangae mimi wananiita 'mchawi wa kompyuta' nitautumia utaalamu wangu wote pale mnaponihitaji kwa ajili ya nchi yangu" Bite alisema na kila mmoja alitabasmu
"So we are a team now?" (kwahiyo sisi ni wamoja sasa?) Habiba aliuliza
"Yeah" Allen alijibu
"Ok kesho asubuhi tukutane kupanga mikakati ya kazi yetu" Habiba aliwaambia na wote waliondoka kuelekea vyumbani kwao Allen akimsaidia Bosco kwenda kupumzika kwani alikuwa bado mgonjwa kiasi
"Unamwamini?" Allen alimuuliza Bosco kwa sauti ya chini walipofika chumbani
"Kwa kiasi kidogo" alijibu
"Kuna kitu nahisi Bosco ni kama anataka kututumia kukamilisha kazi yake kama kweli yeye ni secret service" Allen alimwambia kwa msisitizo
"Sidhani kaka...pengine inawezekana ni kweli" Bosco alimjibu
"Hebu jiulize kwanini ajianike kwetu kirahisi tu I am sure she want to use us (nina uhakika anataka kututumia)"
"Bro me nashauri tuwe naye makini sana ila tujaribu kufanya naye kazi kidogo anaweza kuwa na msaada kwetu" Bosco alihitimisha
****************
DAR ES SALAAM MIAKA 17 ILIYOPITA
Ilikuwa ni siku ya ijumaa tarehe 7/8/1998, ilikuwa ni siku mbaya na chungu kwenye ukanda wa Afrika mashariki na dunia yote kwa ujumla
Kama ni mfuatiliaji mzuri wa historia utakumbuka kuwa ni siku ambayo balozi za marekani nchini Tanzania na Kenya zililipuliwa na kundi la kigaidi la Al qaeda wahusika wakuu waliopanga shambulio hilo walikuwa Fazul Abdullah Mohammed na Abdullah Ahmed Abdullah katika mashambulio hayo mawili watu 224 walipoteza maisha (11 Tanzania na 213 Kenya) na pia watu zaidi ya 4000 walijeruhiwa
Dorcus alikuwa ni mwanamke anayefanya kazi katika ubalozi wa Marekani nchini Tanzania kama mtunza rekodi, mme wake alifariki miaka mitano iliyopita na kumuacha na watoto wawili siku ya shambulio alikuwa na watoto wake wawili ofisini
Ilikuwa ni mda wa kazi kuisha hivyo watoto wake wawili Austin ambaye alikuwa na miaka 9 na Aaron aliyekuwa na miaka mitano walikuwa hapi ili warudi nyumbani kwa pamoja, wakiwa wanaendelea na hadithi za hapa na pale ndipo walisikia mlipuko mkubwa katika ofisi kuu za ubalozi, kwa bahati nzuri ofisi ya kutunza mafaili ilikiwa nje kidogo ya ofisi kuu za ubalozi
Dorcus na watoto wake walipigwa na mshtuko mkubwa na kuanza kupiga kelele punde walisikia milio ya risasi kwenye jengo la ofisi yao walikuwa ni baadhi ya magaidi walioingia kumalizia watu, na ghafla mlango wa ofisi ulipigwa teke, Austin aliyekuwa mkubwa aliwahi kuruka na kujibanza nyuma ya kabati na mara waliingia watu wawili walioshika mitutu aina ya AK47, Dorcus alimkumbatia mwanae Aaron kwa nguvu na akiwaomba wasiwadhuru, hakukuwa na maswali Dorcus aliwekwa pembeni na kumiminiwa risasi za kutosha na kupoteza uhai pale pale, mmoja alipotaka kumuua mtoto mwenzake alimzuia
"Usimuue tuna matumizi naye" alimwambia , walimbeba mtoto na kuondoka naye
Austin nyuma ya kabati alishuhudia kila kitu na moyo ulimuuma sana kuona mama yake alipoteza maisha mbele ya macho yake na mdogo wake akachukuliwa, machozi yalimtiririka sana aliogopa hata kutoa sauti au kutoka nyuma ya kabati kwa kuwahofia watu wale, alishindwa kuendelea kuvumilia na alitoka nyuma ya kabati na kumkimbilia mama yake, alimkumbatia kwa nguvu na kuanza kulia kwa uchungu
"Mama amka.....amka mama" aliendelea kulia kwa uchungu
"Mama kesho ilikuwa birthday yako amka basi mama" Austin aliendelea kulia lakini hakuna aliyemsikia
Mda mfupi baadae polisi waliingia ubalozini na kuwakusanya wote waliosalimika katika shambulio hilo Austin akiwa mmoja wao, pia waliendelea na shughuli nyingine za kiusalama hakika ilikuwa ni siku ya simanzi saina
"Umesema baba yako pia alifariki?" alikuwa ni polisi mmoja wa kike akimhoji Austin kwa huruma
"Ndiyo"
"Maskini pole mtoto mzuri" ilikuwa ni kama amechochea maumivu upya kwani Austin alianza upya kulia kwa uchungu sana na hapo polisi huyo alipata kibarua cha kumbembeleza Austin mpaka alipotulia
"Unawafahamu ndugu zako wengine?"
"Hapana"
"Babu na bibi?"
"Mama aliniambia alitengwa kwao baada ya kuolewa na baba ambaye alikuwa ni kabila lingine kinyume na tamaduni zao"
"Na upande wa baba pia"
"Siwafahamu" polisi yule alishusha pumzi za kuchoka
"Sawa usijali tutakuwa pamoja na wewe" yule polisi alimwambia akimkumbatia kumfariji
Polisi yule aliwasiliana na wakubwa zake ili waone jinsi ya kumsaidia mtoto yule na walikubaliana wampeleke kwenye kituo kimoja cha kulelea watoto yatima..mchakato ulifanywa na Austin alikabidhiwa kwenye kituo kimoja kilichoitwa charity orphanage center
Austin alipelekwa kulelewa huko ili alelewe, asomeshwe na atimize ndoto zake kwa mara ya kwanza ilikuwa vigumu sana kwa Austin kujichanganya na wenzake kwani tukio la kifo cha mama yake na kuchukuliwa mdogo wake lilimuathiri vibaya kisaikolojia lakini baadae alijikuta akisahau na kurudi katika hali ya kawaida
"Austin ukiwa mkubwa unatamani kuwa nani?" mlezi mmoja aliyeitwa sister Magreth alimuuliza
"Nataka kuwa daktari bingwa ili nitibu wengine"
"Sawa mtangulize Mungu siku moja utafikia malengo yako"
ITAENDELEA USIKOSE SEHEMU IJAYO.........
