Acetamin 220_03



ACETAMIN-220

BARAKA GEOFREY

+255652089642

ILIPOISHIA..........

Ndani ya gari kwa Bosco hali ilikuwa mbaya tayari alishapigwa risasi mbili na alikuwa ameishiwa risasi Allen pia alibakiwa na risasi moja akajua kabisa wamezidiwa bado risasi ziliendelea kumiminika upande wa Allen na Bosco pia Keddy naye alikuwa anawasili mda huo na kuendeleza mashambulizi....Bosco alishajikatia tamaa na alitulia tu akisubiri mwisho wake

ENDELEA............

Lenita alianza kujivuta taratibu kuelekea kwenye gari kwani alijua kuwa Bosco ameshazidiwa......

Ghafla piki piki moja kubwa iliingia eneo lile kwa kasi juu yake alikuwepo mtu aliyevaa kofia ngumu 'helment na alikuwa ameshika bunduki ya kivita aina ya 'SG 443 Carbine' na alianza kumimina risasi za kutosha kuelekea kwa kina Lenita na mara hiyo hiyo king'ora kilianza kusikika kwa mbali kikikaribia mahali hapo

Lenita alijikuta akitoa tusi la nguoni kwani alijua mambo yameharibika, kwanza hakujua yule mtu ametoka wapi pia alijua polisi wanafika baada ya mda mfupi kutokana na milio ya risasi iliyosikika


"Keddy tuondoke" alimwambia Keddy 

"Tumchukue na Mahmoud" alimwambia 

"Tumwache tu atakufa tu huyo"

"Hapana amepigwa tu risasi ya bega"

Keddy alimuweka begani na Lenita alivurumisha risasi huku wakipotelea vichakani

Baada ya kuona wameondoka mtu yule alishuka kwenye pikipiki lakini na Allen alijitokeza kutoka mafichoni

"Wewe nani?" Allen aliuliza

"Hatuna mda Allen polisi wanakuja sasa hivi ingia ndani ya gari unifuate" sauti ya kike ilimjibu

Kwa haraka Allen aliingia kwenye gari alimkuta Bosco akiwa kwenye maumivu makali

"Pole kaka" alimwambia akiwasha gari

"Asante" alijibu na kuendelea kuuma meno kwa maumivu makali

Allen aliwasha gari na kuondoka akiifuata pikipiki ya yule mdada, gari ilikuwa imechakazwa vibaya kwa risasi kiasi cha kutisha.... alimfuata kwa takribani dakika kumi na walifika kwenye nyumba moja ndogo ila ya kisasa geti lilifunguka na waliingia ndani

"Karibuni" yule mdada alisema akivua helment yake, alikuwa ni binti mwenye weusi wa kung'aa

"Wewe ni nani?" Allen alimuuliza

"Naitwa Habiba"

"Bado sijaku......"

"Hakuna mda wa maswali Allen tunatakiwa tumsaidie Bosco apatiwe huduma haraka muda wa maongezi baadae" Allen alimshangaa mdada huyo amemjuaje yeye na Bosco pia, walimsaidia Bosco kushuka na kumwingiza ndani na kisha kumlaza kwenye kochi

"Ngoja nimpigie daktari wangu aje akutibu hapa hapa huwezi kwenda hospitali..."

"Hakuna haja mnipeleke tu nyumbani then nitajua cha kufanya" Bosco aliongea kwa sauti ya kinyonge

"So sorry Bosco nyumba yako imechomwa moto na hawa watu" mdada yule alimwambia akimwangalia kwa huruma

"Whaaaaaat??" Bosco alipigwa na mshtuko alijaribu kuinuka lakini maumivu yalimrudisha chini

"Come down brother" (Tulia kaka) Allen alimtuliza, uchungu alioupata Bosco haukuwa wa kawaida alitumia fedha nyingi kujenga nyumba yake na pia nyaraka zake zote za siri na kazi zake alizibidadhi humo

"I have lost everything..." (Nimepoteza kila kitu) alilalamika kwa uchungu

"Usijali Allen ofisi yako ya chini ya ardhi ipo salama haijateketea" Habiba alimwambia, Allen na Bosco walishtuka kuwa mdada huyo anafahamu hata ofisi ya siri ya Allen

"Wewe ni nani? na umejuaje kuhusu ofisi yangu ya siri?" Bosco aliuliza kwa tahamaki

"Hahahaha nilijua utafurahi kuwa ofisi yako iko salama....najua mambo mengi kukuhusu Bosco ila hicho sio muhimu kwa sasa, tushughulikie matibabu yako tutaongea vizuri baadae....." mlio wa simu ya Bosco uliwashtua wote na Allen alimsaidia kuitoa mfukoni....Beatrice ndiye aliyekuwa anapiga

"Bosco naomba uje unisaidie haraka kuna watu naona wananifuatilia kuanzia natoka ofisini please Bosco naogopa" sauti ya Bite ilisikika akiwa anaogopa kupita kiasi

"Uko wapi?" Allen alimuuliza

"Naelekea nyumbani nipo hapa Milimani road please Bosco naogopa"

"Usijali wewe endelea kuendesha kama kawaida tunakuja usionyeshe kuwa umewagundua" Allen alimweleza

"Sawa" alijibu Bite alikuwa na wasiwasi mpaka alishindwa kugundua kuwa yule sio Bosco ni Allen


"Kaka twende tukamsaidie" Bosco aliongea kwa tahamaki

"Tulia Bosco huwezi kwenda ukiwa hivyo" Allen alimtuliza

"Lakini mimi ndio nimemsababishia matatizo lazima niende" alijibu akijikaza kuinuka

"Tulia Bosco..." Habiba alimwambia kwa ukali

"Mwache Habiba ashapenda huyo...wewe mpigie daktari aje mimi naenda kumsaidia" Allen alijibu akitabasamu, alichukua simu ya Bosco na kuanza kuondoka

"Hujachukua silaha" Habiba alimwambia na kumrushia bastola aina ya revolver iliyojaa risasi na magazine moja

"Kitu cha Samuel Colt hiki" Allen alisema akitabasamu na kuondoka


                      **************

"Asante sana Allen wangeniua washenzi wale" Beatrice alimwambia Allen wakiwa kwenye gari kuelekea nyumbani walikohifadhiwa na Habiba

"Usijali" alimjibu kifupi

"Bosco yuko wapi?" 

"yupo nyumbani utamkuta" Bite alipiga kimya ila moyoni alijiuliza kwanini hakuja naye kumuokoa

"Mbona sio nyumbani huko.." Bite alimuuliza kwani alipajua vyema nyumbani kwa Bosco

"Tumehama" Allen alimjibu kifupi kwani hakutaka kumzoea Bite aliujia vyema ugonjwa wake wa kupenda warembo asija kugombana na Bosco bure.....Bite alipoona jamaa hataki hadithi nyingi alitulia zake kimya

Walifika kwa Habiba na kuingia ndani walimkuta Bosco amelazwa chumbani baada ya kutolewa risasi na kupewa huduma na daktari

"Amefanya nini" Bite aliuliza kwa wasiwasi

"Kazi zetu hizi mama ajali kazini tu hiyo" Allen alimjibu ,Habiba aliwatoa na kuwapeleka sebuleni ili wamwache Bosco apumzike

"Allen hujafanikiwa kumchukua hata mmoja tumhoji" Habiba alimuuliza

"Hapana ilikuwa sehemu ya watu wengi na hatari kwa hiyo nilifanya ujanja tu kuwapotea"

"Una uhakika hawajawaona mnapofika hapa?"aliuliza tena kwa mashaka kidogo

"Usiwe na shaka nimewapoteza mbali sana na washukuru mizimu yao kulikuwa na watu wengi ningewafanyia kitu kibaya walipe kwa kumuumiza Bosco, kuchoma nyumba yake na kuharibu kazi yetu kenge hawa" Allen aliongea akiuma meno kwa hasira

"Okay nenda kapumzike na Bite pia upumzike baadae usiku Bosco akiamka kuna mambo nataka niwaeleze" Habiba aliwaambia

"Sawa lakini ni vizuri ningekujua ili nikae kwa amani" Allen alimwambia kwani kwa mtu kama yeye haikuwa rahisi kumuamini mtu asiyemjua kirahisi tu

"Allen sikia ningekuwa na nia mbaya na wewe ningekumaliza toka siku ya kwanza unaingia Kenya kama huniamini beba vitu vyako uondoke mimi sijakulazimisha kukaa hapa" Habiba aliongea kwa hasira kwani alikerwa na tabia ya Allen kutomuamini toka mda, alianza kuondoka kwa hasira

"Habiba sorry kama nimekukera lakini huwa simuamini mtu..."

"Then you are free to go" (Basi unaweza kwenda) Habiba alimwambia na kuelekea zake chumbani

"Allen mda mwingine unatakiwa kuamini watu hata kidogo" Bite alimwambia kwa upole

"Nimekutana na vitu vingi Bite I trust nobody" Allen alijibu

"Hata Bosco humuamini?" Bite aliuliza kichokozi akitabasamu, Allen alicheka tu lakini hakumjibu

"Answer me" Bite alimwambia

"Guys natoka nitarudi baadae ambae anajiona hayuko salama anaweza kwenda pia" Habiba aliongea na kuondoka


"Allen kwani huyu mwanamke ni nani?" Bite alimuuliza, alishasahau swali lake la kwanza halijajibiwa

"Simjui alitusaidia tu wakati tunatoka uwanjani tulivamiwa" Allen alimjibu aliondoka akielekea chumbani alikolazwa Bosco, hakupenda kabisa kukaa karibu sana na Bite kwani alijua ambacho kingeweza kutokea na alimheshimu Bosco

'Ila yule mtoto kisu' alijiwazia Allen


Koh! Koh! Koh! Bosco alianza kukohoa

"Bosco pumzika umeumia" Allen alimwambia

"Aah kaka toka lini jasusi akalala kama mjamzito hata kama ameumia" Bosco alimwambia na wote wakacheka

"Unajisikiaje lakini kaka"

"Afadhali kidogo daktari amesema risasi hazijagusa mfupa kwa hiyo nitapona baada ya siku chache tum..wangeniua washenzi wale... kuna kadem pale kalikuwa na shabaha hatari" Bosco alimwambia

"Halafu walituvamia ghafla" alijibu Allen

"Kama sio huyu Habiba sijui ingekuwaje"

"Kaka unamwamini huyu" Allen alimuuliza

"Ndiyo"

"Hiyo ndo shida yako Bosco unaamini watu kirahisi hasa wanawake umeshasahau kilichokuopata kule Botswana"

"Hamna kaka sasa mtu ametuokoa...."

"Usibishe Bosco 'you are so weak to women'

"Sawa kaka mimi sitaki kuongea sana"

"Kwanza ngoja nikakuitie mke wako Bite aje akusalimie" Allen alimwambia akitabasamu

"Hahaha acha zako....halafu nilisahau kukuuliza ulimpata"

"Ndiyo shem lazima atunzwe"

"Allen bwege wewe....Asante lakini kwa kumuokoa ningejisikia hatia sana kama angepata shida yoyote, Allen hakujibu alitabasamu tu na kwenda kumwita Bite

     

                   **************

Majira ya saa 2 usiku Habiba alirudi aliwakuta wakipiga soga za hapa na pale.....

"Mnaendeleaje" aliwasabahi 

"Salama tu" Bite alijibu

"Mgonjwa unaendeleaje?" 

"Vizuri tu" Bosco alijibu, Habiba alimwangalia tu Allen kwa macho fulani ya kinyongo na kutomuongelesha

"Nimewaletea chakula mchangamshe kidogo matumbo" Habiba aliwaambia akitoa chakula cha take away kwenye mfuko alioingia nao, kwa pamoja walikula na kisha Habiba alianza mazungumzo..

"Bite unaweza kwenda kupumzika chumbani kuna vitu tunataka kuongea"

"Abaki tu kwani ana shida" Bosco aliongea, Allen alimpiga jicho fulani kali Bosco

"Ok basi baki" Habiba alisema

"Hamna shida ngoja niwapishe" Bite aliongea

"Hapana baki tu" Habiba alisema 

Bite alikaa chini...

"Ok guys kuna mambo ya msingi sana nataka niwaambie nadhani wote hamnifahamu ila mimi nawajua vizuri ni watu wa usalama wa taifa Tanzania labda Bite ndio nimemjua leo......

ITAENDELEA USIKOSE SEHEMU IJAYO......

Jaba Zulma

Siyumbi

Your Thoughts

Previous Post Next Post

Contact Form