RIWAYA; NGOMA NGUMU.
NA; BAHATI K MWAMBA.
SIMU; 0758573660/0624155629.
SEHEMU YA SABA..
“Ooh Sorry, nilikuwa nafanya tahajudi kidogo!” Miguu ya kuku alisema huku akipisha mlangoni ili kumruhusu mgeni wake aingie.
“Usijali!” Mgeni alisema huku akipita mlangoni kwa madaha na kuacha pua za Miguu ya kuku zikiteseka kwa harufu nzuri ya uturi wa bei mbaya.
Zuki Gadu alibaki mlangoni akiwa amezubaa. Hakuamini kama Dunia hii bado ina wanawake wazuri ambao hawajapoteza rangi zao za asili, wala kuwa na maumbo mazuri namna ile. Ilikuwa imepita miaka mingi bila nafsi yake kutekwa na mwanamke lau kwa sekunde kadhaa. Nafsini mwake alijikuta akitamani kujua yaliyoko ndani ya mwanamke yule. Mwanamke ambae alikuwa ameumbika pasi kifani. Hakuwa mnene wala hakuwa mwembamba lakini nyama za maeneo shawishi zilikaa vema kwa mpangilio sawia, kifuani kuliota embe sindano ambazo hazikuonekana kuwa na haraka ya ukuaji. Macho yake yalikuwa madogo yaliozungukwa na kope halisi zilizoota kwa mpangilio mzuri. Nyusi zake hazikuhitaji wanja na hata mwanamke yule hakuwa ameziwekea wanja, aliacha ziwe kama alivyopewa na Mungu. Hakuhangaika kuzinyoa wala kuzichonga. Ngozi yake ilikuwa imetakata weusi mzuri ambao hakuhitaji mafuta makali ili kulinda ubora wake. Sura yake ilivutia kuliko michoro ya katuni za Jiriwa. Susa hakika alikuwa Susa aliekamilika.
“Nimepewa maelekezo machache na Bob, hivyo si vibaya nikisikia kutoka kwako pia.” Susa aliongea taratibu kama vile hakuwa na haja na maongezi ndani ya hicho chumba.
“aah! Okey,” Miguu ya kuku alisema huku akijibweteka kwenye sofa lililokuwa limewekwa ndani ya kile chumba.
“Ninahitaji unifanyie jambo moja hivi…” Zuki alinyamaza na kumtazama usoni, kisha aliendelea…
“Nina kazi moja ambayo imenileta hapa Nairobi. Kazi hiyo ni ngumu kuliko kawaida. Na Bahati mbaya ni kwamba hadi sasa kuna funza ameanza kulitoboa chungwa hata kabla halijaanguliwa. Mtu huyo ofisa wa jeshi la polisi.”
“Hapo mimi kazi yangu ni ipi?” Susa alihoji bila kupepesa macho yake madogo.
“Nataka uwe Mzungu wake!” Zuki alijibu.
“Honey trap?”
“Yes!”
“Lakini sioni kama kuna haja hiyo. Kwani unataka kumteka au unataka kumuua?”
“Vyote hivyo sivihitaji.”
“Sasa hapo siyo Honey trap, bali ni poison trap.!”
“Haiwezi kuwa poison kwa sababu itakubidi utoa utamu wako kama ikibidi. Hivyo hadi hapo itakuwa imeshavuka poison na itakuwa imeingia kwenye asali.”
“Garama ya kutoa mwili wangu huwa ni kubwa sana. Utaweza kunilipa?”
“Sina hakika kama nimewahi kushindwa kulipa. Nimeandaa Milioni tano za Kenya kwa ajili ya kazi yako na itaongezeka kadri utakavyofanikiwa.”
“Oh my God! Una hakika na unachosema?” Susa aliuliza huku akiwa anamtizama Zuki Gadu kwa mshangao.
“Nipe jina la akaunti yako nikufanyie muamala dakika hii!”
“Wait! Utanilipa katikati ya kazi kwa sababu sitaki wajue nalipwa na wewe endapo kutakuwa na taarifa wanafuatilia kuhusu wewe!”
“Good! Una mawazo makubwa sana.”
“Ok, nipe kazi niifanye kuanzia leo.”
Haraka Zuki Gadu aliiendea kompyuta yake, kisha akagusa hapa na pale na picha kubwa ilijaa kwenye kioo.
“Huyu jamaa anaitwa Sajini Nyau, ni mtata sana. Mpenda ngono na mpenda rushwa kuliko askari wote ambao unawajua hapa Duniani. Naomba ufuatilie nyendo zake za leo na ikibidi uchukue namba yake kwa siku ya leo. Ukifanikiwa, tutaingia sehemu ya pili ya mpango wetu.”
“Sawa. Nitaanza kumpata wapi?”
“Yupo hapo Benki ya Umoja.”
“Good!” Susa alisema huku akijiinua kitandani.
“Wait! Aah, una gari?” Zuki alimuuliza.
“Ninazo gari tatu. Moja nimekuja nayo ipo hapo nje.”
“Unaonaje ukiniachia hiyo uliyokuja nayo ili inirahisishie mambo yangu?”
“Wazo zuri, lakini nitakuagizia gari nyingine na ndani ya dakika kumi na tano itakuwa hapo nje. Dereva atakupa taarifa akishafika.”
“No! Dereva akupe wewe taarifa na wewe utanipa mimi taarifa.”
Susa hakujibu, badala yake aliondoka ndani ya kile chumba na kumwacha Miguu ya kuku akianguka kitandani kizembe.
*****
Dakika ishirini baadae, simu ya miguu ya kuku iliita na mpigaji alikuwa ni Binti Susa. Aliipokea na kusikiliza maelekezo ya upande wa pili, kisha alikata simu bila kuongeza neno lolote. Baada ya kukata simu aliinuka kitandani na kuelekea nje, ambapo alienda mapokezi na kuomba kupewa funguo zilizoachwa na mgeni wake. Mapokezi walimpa bila kuuliza lolote.
Baada ya kupewa funguo alienda nje ya uzio wa hoteli, huko alitumia kibati cha funguo za gari kulitafuta gari husika ambapo; alibofya kitufe chenye rangi ya kijani na taa za gari fulani ziliwaka na kuzima mara moja. Alilisogelea lile gari na kulitizama kwa umakini, kisha alifungua mlango na kuingia ndani yake ambapo aliliwasha na kuliacha liungurume huku yeye akiwa ndani yake. Gari iliunguruma kwa zaidi ya dakika tano, kisha aliizima na kushuka.
“Itanifaa kwa mizunguko yangu.” Alijisemea huku akianza kupiga hatua kuelekea ndani ya hoteli na akiwa na wazo moja kichwani, wazo ambalo hakuwa na hakika kama litakuwa wazo sahihi kwake. Lilikuwa ni wazo lenye hatari lakini lingelikuwa salama kama, lingelifanikiwa vile alivyotarajia.
Wakati yeye akiwaza jambo lake upande wa pili Sajini Nyau alikuwa anamalizia kuzungumza na mtu kwenye simu. Alipomaliza kuzungumza aligeuka kulia kwake kivivu, kisha alizungusha macho yake pande kadhaa na kuanza kuondoka pale alipokuwa amesimama. Alikuwa amehakikisha hakuna mtu ambae alikuwa amemwona wakati alipokuwa akizungumza na simu.
Alipiga hatua zake taratibu kuelekea upande wa mbele wa benki ya umoja ambapo kulikuwa na maofisa kadhaa wakiendelea kudumisha ulinzi eneo lile. Alipofika walipokuwa wengine, alianza kuangaza huku na huko hadi alipofanikiwa kumuona aliyekuwa anamhitaji. Haraka alipiga hatua na kumfuata na alipomfikia alikakamaa kwa heshima na kusaluti, kisha alisema..
“Ninahisi kuna jambo kubwa linaendelea kuhusu kilichotokea hapa Afande!”
“Unahisi au una uhakika?” Aliulizwa.
“Ninahisi ila kama itakupendeza naomba nifuatilie jambo,kisha nikupe uhakika.”
“Sawa, chagua vijana unaodhani wanaweza kukusaidia kwenye majukumu yako. Saa kumi na mbili zinatosha kuleta mrejesho?”
“Zinanitosha mkuu!”
“Sawa! Ripoti kwangu baada ya saa hizo!”
“Natekeleza mkuu.” Sajini Nyau alisema huku akipiga saluti na kuanza kuondoka.
Tofauti na alivyoagizwa kuambatana na maofisa wengine, yeye aliamua kuondoka bila kumshirikisha mtu yeyote. Alipanda kwenye gari lake na kuelekea kituoni. Alipofika alielekea ofisini kwake, ambapo alibadili nguo na kutoka mkukumkuku kama anaekimbizwa.
Haraka alirudi kwenye gari lake na kuliondoa kwa kasi kuelekea katikati ya jiji la Nairobi. Kuna mtu muhimu sana alikuwa anahitaji kuonana nae. Uwepo wa Miguu ya kuku ndani ya jiji la Nairobi, kwake iliamsha hisia za hatari kuliko mtu yeyote. Hatari hiyo iliongezeka zaidi alipogundua aliyeharibu mfumo wa utoaji pesa ni huyohuyo Miguu ya kuku.
Alihisi kuna jambo litakuwa linaendelea na hakutaka kumshirikisha mtu kwenye mashaka yake, ila alihitaji apate taarifa zaidi kisha aziuze kwa namna ambayo angeliweza na kama lingelikuwa jambo lenye manufaa zaidi, basi alipanga kumweka mtu kati Miguu ya kuku ili nae anufaike na jambo hilo. Kitu ambacho hakujua ni kuwa, alikuwa anajaribu kumfuatilia mtu ambae alimzidi kila kitu. Alimzidi akili, pesa, hata urefu alimzidi mbali tu. Hivyo ni kama simba kujaribu kufuatilia nyayo za Dubu kwa imani ya kuweza vita.
Hakujua nyayo za Miguu ya kuku huwa hazifuatiliwi kwa namna aliyoamua kutumia. Wakati anajaribu kuchimba taarifa za Miguu ya kuku, hakujua tayari yeye alishawekewa mtego wenye harufu ya Waridi, mtego unaonukia.
Sajini Nyau alifika Poa hoteli akiwa ametumia zaidi ya dakika ishirini safarini. Alipofika mapokezi, aliomba kuonana na mgeni aliyekuwa chumba namba 107. Aliruhusiwa kuelekea huko kwa sababu kulikuwa na taarifa zake kutoka kwa mtu aliyekuwa amepanga kwenye hicho chumba.
Sajini aliingia ndani ya chumba bila kugonga na alikutana na tabasamu mwanana la mwenyeji wake. Kabla ya jambo lolote walikumbatiana kwanza, kisha walipigana busu za hapa na pale ilimradi kuonesha wako pamoja kwa mara nyingine.
“Nambie, nile kwanza kisha tuongee au tuongee kwanza kisha nile?” Sajini Nyau aliunguruma taratibu masikioni mwa mwenyeji wake.
“Sina hakika kama ni busara kula kabla ya kuongea na tukiongea, sioni kama tutakuwa na nafasi ya kulana.” Mwenyeji alimwambia Sajini huku akijiondoa mikononi mwake.
“Mh kwa nini leo unanikatili namna hii?” Sajini alilalamika huku akizishuhudia nyonga za mwenyeji wake zikipishana mithili ya nyanga za mganga wa kienyeji.
“Hapana sijakukatili, bali ni uzito wa jambo nililokuitia.”
“Jambo hilo unahisi laweza shinda hisia za matamanio yangu kwako?”
“Come on Sajini! Nimekuitia utajiri na si mapenzi ati…”
Sajini alimakinika kidogo joto lililokuwa limeanza kumpanda, likiishia bila maana yoyote.
“Sawa, hebu nipe dokezo kidogo, maana tulipoongea kwenye simu hukuwa umenifafanulia lolote!”
Haraka mwenyeji wa kile chumba alikimbilia mkoba wake na kutoa simu yake, kisha alianza kuperuzi hapa na pale hadi alipopata alichokihitaji.
“Huyu kiumbe unamfahamu?” Mwenyeji aliuliza huku akiwa amebinua simu yake ili mgeni wake aweze kuona alichoulizwa.
“Hakika ninamfahamu. Kwani vipi?” Sajini Nyau aliuliza huku akiichukua ile simu na kuendelea kuitizama picha ya mtu aliyekuwa amejaa vema kwenye kioo.
“Unamfahamu vipi?” Aliulizwa.
“Miaka ya nyuma kidogo aliwahi kuishi hapa Nairobi. Wakati huo alikuwa mlinzi binafsi wa kiongozi wa genge la uhalifu la Sadon. Baadae alipotea na kiongozi huyo aliishia gerezani. Jambo kubwa ninalolifahamu kuhusu yeye ni kuwa; wakati akiwa mlinzi binafsi wa huyo kiongozi, alishiriki vema kulifanya kundi hilo kutekeleza uhalifu kwa akili kubwa sana. Lilijitanua sehemu kubwa ya mji wa Nairobi, lilimiliki mali nyingi za halali na zisizo halali. Lakini cha kuvutia zaidi ni namna walivyoweza kufanya matukio yao bila kuacha alama nyuma, walikuwa makini sana wasikamatwe wala kuingia mikononi mwa macho ya serikali, ijapokuwa serikali ilifahamu uwepo wao lakini ushahidi wa kuwahukumu haukuwepo. Yote hayo yalifanikishwa na huyu jamaa na tulimfahamu kwa jina la Dogo.”
“Duh! Basi huyu jamaa karudi tena hapa Nairobi na wakati huu anajina jipya, anajiita Zuki Gadu. Nimejaribu kufunua taarifa zake lakini hakuna hata taarifa inayomhusu. Nimejaribu kupigia simu watu kadhaa huko Tanzania, nao wameishia kunambia huyo mtu hana rekodi yoyote zaidi ya ile ya utambulisho wa mpiga kura na hati za kusafiria. Zaidi sana anamiliki yadi kubwa ya magari na pikipiki ndani ya jiji la Dar Es laam.” Mwenyeji alisema huku akijibweteka kitandani.
“Sasa wewe hiyo picha umeipata wapi?” Sajini aliuliza huku akimtizama mwenyeji wake.
“Nilimpiga kiujanja sana wakati nilipokutana nae saa chache zilizopita.”
“Ulikutana nae? Ikawaje sasa!” Sajini Nyau aliuliza huku akiwa ameanzaRIWAYA; NGOMA NGUMU.

“Ulikutana nae? Ikawaje sasa!” Sajini Nyau aliuliza huku akiwa ameanza kujenga hisia za wivu.
“This time you’re his target!”
“Whaaat!” Sajini aliropoka kwa sauti na asiamini alichokisikia.
ITAENDELEA. kujenga hisia za wivu.

ITAENDELEA.