DADA MDUNGUWAJI: UTANGULIZI

 DADA MDUNGUWAJI


SEHEMU YA KWANZA


STORY NA Mbogo Edgar

WHATSAPP NO:- 0743632247 (MATUMIZI YA OFISI TU)

Iikuwa yapata saa nne kasolo zausiku, mtaa wa Kimbamba njia panda ya shule, ndani ya nyumba moja kubwa ya wastani, Denis akiwa namwanae Fransis, mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu, sebuleni wakiangalia movie kwenye tv kubwa ya ukutani, na kunywa pombe aina ya bia, huku mala kwamala Denis alionekana kuangalia saa kwenye simu yake ya mkononi, wakati mwingine akijaribu kupiga simu, lakini alijibiwa kuwa “mtumiaji wasimu unayempigia apatikani kwa sasa” Denis alionekana kuzidi ku changanyikiwa “atakuwa wapisasa, mbona mama yako anazidi kunichanganya” Denis aliongea kwa sauti, akiweka simu mezani, mwanae Fransis, alimwangalia baba yake asijuwe lakumwambia, kwani ata uongea jiwake bado ulikuwa wakubabaisha,

Wakati Denis na wakiendelea kuangalia movie huku mawazo yaliyo changanyika na wivu yakimsonga Denis, kwambali wakaanza kusikia ving’ola vyapolisi, kwanza Denis alizani kwenye Tv, lakini vikazidi kusikika kwauwazi vikisogea upande wamtaa wao akapunguza sauti ya TV, iliaweze kusikia vizuri , kweli aliweza kusikia ving’ola kwakaribu zaidi, akamwangalia France akataka kumwuliza kunanini, lakini ata angemwuliza ingekuwa kazi bule, asingeweza kumjibu, wakati ving’ola vikiendelea, akaanza kusikia vishindo vizito vya mtu akikimbia kusogelea nyumba yao, mapigo yake yamoyo yakaongeza kasi, kwa uoga uliomjia ghafla, vishindo vya mtu huyo alie onekana kuvalia buti kama za kijeshi, vilikuja na kishia mlangoni, hapo Denis nusu ajikojolee akakumbuka kuwa ameufunga ameufunga kwa funguo, hapo akaona kitasa cha mlango kikinyongwa, lakini mlango aukufunguka, hapo ikafwatia sauti ya mtu anaita, “baba France, baba France” ilikuwa sauti ya mke wake mpendwa Jackline, ambae aliita kwasauti ya chini sana, kama vile akutaka wawatu wasikie, moja kwa moja Denis akahisi kuwa mke wake yupo kwenye hatari, hivyo haraka sana akainuka, na kwenda kumfungulia, akamwona mke wake akiingia ndani kwa kasi ya hajabu, Denis akapigwa na butwaa, siyo kwa kasi aliyoingia nayo mke wake, ila kwa mavazi aliyorudi nayo mke wake, ambae aliondoka akiwa mevalia gauni lake refu jekundu na viatu vya mchuchumio vyeupe, lakini sasa anamwona amerudi akiwa amevalia suluwali ya kaki yenye muundo wanguo za kijeshi, za kupingania vita (kombati) juu amevalia tishet nyeusi mkononi amebeba begi dogo jeusi, analikumbuka ilibegi, toka mala ya kwanza alipomwona miaka miwili na nusu iliyopita, akiwa anajiusisha na bishara ya chakula, mama ntilie, lakini sasa lilikuwa linakaa wanako laza gari (park)kwenye makolokolo ya vifaa vibovu, Jackline au mama France, alikuwa amevalia buti nyeusi zenye shingo ndefu, kama za wanajeshi, kikubwa zaidi ambacho kilimstua, ni damu zilizo tapakaa kwenye uso wake na mikononi, kwa mke ake huyo, ata kwenye suluwali, lakini kwenye tishert aikuonyesha, kutokana na rangi yake nyeusi, wakati huo Ving’ola vilizidi kusogea upande wao, Denis alimshuhudia mke wake akipitiliza mbio mbio, na kuingia jikoni, kabla ajasikia mlango wa kutokea nje upande wajikoni, ukifunguliwa na baada ya sekunde chache, akasikia mlango ukifungwa, na mke wake akarudi sebuleni, Denisi alikuwa amerudi na kukaa kwenye kochi na mwanae wapo kimya akimtazama mke wake, kama anamwona kwamala ya kwanza, wakati huo ving’ola vya polisi vilikuwa vina sika nje ya nyumba yao, Jackline aliwatazama mumewe na mwanae, akataka kusema jambo, lakini alikatishwa na sauti kali kutoka nje ya nyumba yao, toka kwenye kipaza sauti, kama kile ya kuuzia dawa ya panya, “Jackline Michael Nyati, ilinijeshi la polisi, tupo nje ya yumba yako na silaha zenye risasi za moto, fungua mlango, utoke nje ukiwa mikono juu, vinginevyo tuta tumia nguvu zaidi kukutoa humo ndani” Denis na mke wake wote kwa pamoja, waliuangalia mlango, ile sauti ya kwenye kipaza sauti ikarudia tena maneno kama yale yamwanzo, Denis akiwa aelewi, kinacho endelea, au mkewake amefanya nini, Jackline yeye aliwatazama mume wake na mwanae, akamwambia mume wake “ Denis kesho njoo tuonane popote watakapo nipeleka, utafahamu kila kitu” akaitoa simu yake mfukoni, na kumkabidhi mume wake, mjulishe baba mwambie nimekamtwa, na kazi nimesha maliza, husi saau pia kesho kuja mahabusu yoyote nitakayo wekwa” Denis aliitikia kwa kichwa huku amejawa na wasiwasi, kiasi kwamba akaanza kumwogopa mkewe, hapo Denis akamwona mkewake mama France au Jackline, akifungua mlango taratibu, mala mwanga wataa za magari ya polisi, ulimpiga machoni, akapandisha mikono juu, kama alivyo amriwa, akatoka nje kabisa, “simama hapo hapo ulipo, kisha piga makogoti, weka mikono nyuma yako kisogo” kile kipaza sauti kikapaza sauti, na Jackline akafanya kama alivyo amriwa, na hapo haraka sana, askari polisi sita, wakiwa na silaha aina ya SMG sub machine gun kwenye mikono yao, pia wame valia mavazi maalum yakuzuwia risasi (bullet proof) na kofia za chuma, walimzingira Jackline, huku wakimwelekezea mitutu ya bunduki zao, kitendo kile kilimshangaza sana Denis, mke wake amefanya kitu gani mpaka awekwe chini ya ulinzi namana ile, wakati huo Denis alishuhudia kundi kubwa la askari wengine, wakiwa wamevaa kama wenzao, pia mikononi walikuwa na siraha tofauti tofauti, kama bastora, SMG na uzi gun, walikuwa wamezunguka nyumba nzima, kiukweli ungezani wanapambana na kundi kubwa la majambazi, au magaidi waliojaribu kuiba ikulu, wakati wale askari sita wakiwa wame msogelea Jackline nakumlaza chini, kifudi fudi, wakimfunga pingu mikono kwa nyuma, (mgongoni) akaonekana akisogea polisi mmoja mwenye nyota tatu, Inspector, alipofika pale aliachia tabasamu pana akachuchumaa alipolala Jackline, akasogeza mdomo sikioni kwa Jackline, kisha akamwambia, “hupo chini ya ulinzi mshenzi we! Utalipia vifo vyote” Jackline alikuwa anamtazama huyu inspector kwa hasira na ghazab, kisha kwa shida sana, kutokana na kukandamizwa na goti na askari mmoja, alimwambia yule inspector “nitakuja kuongea na wewe, sizani kama unajuwa unachokifanya” hapo yule polisi mwenye nyota tatu, akatabasamu tena tabasamu lililo chanyika na hasira kari sana, “ulishindwa kuongea na mimi kabla ujafanya upuuzi wako, utaongelea mahakamani” alisema yule inspector, huku akimtazama mama France kwa zarau kubwa sana, lakini kitu cha hajabu Jackline akatabasamu, tabasamu lililo changanyika na maumivu ya kuminywa na wale askari, “mahakamani?, sijajuwa ataenda nani, kati yako na yangu ila ukweli nitakuja kwako kesho jioni” kwa maneno hayo yalionekana kumchukiza sana yule inspector “pelekeni ndani ya gari hii takataka”

Wakati huo Denis akiwa amembeba mwanae France, alikuwa amesimama mlangoni akimtazama mkewe akiwekwa chini ya ulinzi, na kundi kubwa la polisi ambalo lipo kamili na silaha za kimapambano mikononi, na sasa alishuhudia mke wake akipelekwa kwenye gari, lakini Jackline kabla ajaingizwa kwenye gari, aligeuza kichwa na kuwatazama, mume wake na mwanae France, macho yao yaka gongana, Jackline akaachia tabasamu lililoongeza machungu moyoni kwa Denis, huku mwanae France akianza kuangua kilio, akimlilia mama yake, yule jamaa mwenye nyota tatu, inspector, alimfuata Denis pale mlangoni aliposimama namwanae, huku akiwapa ishara polisi wenzake, kuipekua ile nyumba yote, “nazani wewe ndie mume wa Jacline Michael Nyati” aliuliza yule polisi mwenye nyota, Dennis akaitikia kwa kicha, “mkeo anashikiliwa na polisi, kwa kuhusishwa na mauwaji mfurulizo yawatu zaidi ya ishirini, wakiwepo viongozi wadini na wafanyabiashara wakubwa, maelezo zaidi utayapata kesho, fika kituo kikuu cha polisi, ambako mkeo atakuwepo pale akisubiri kushtakiwa” aliongea yule inspector, kisha akageuka na kuelekea kwenye magari akifwatiwa na askari wake, huku wengine wakitoka nje ya nyumba ya Denis, wakipiga kelele kila mmoja “hakuna kitu” “hakuna kitu” “hakuna kitu” Wote wanaingia kwenye magari yao wanaondoka kwa kasi ya hajabu, gari alilopakizwa Jackline au mama France, lilikuwa katikati likilindwa na askari wenye silaha, waliokuwa wamening’nia kwenye magari ya wazi (defender) nyuma na mbele, baadhi ya raia ambao walishaanza kutoka majumbani kwao, walishangaa na kuanza kuongea kila mmoja la kwake, lakini ukweli nikwamba, Denis pekee ndo alieambiwa, mkewake ameuwa watu zaidi ya ishirini, kitu ambacho akiku muingia akilini atakidogo, kwamba mke wake ni muuaji, jinsi alivyomfahamu ni mpole mtaratibu mnyenyekevu na mwenye huruma, itakuwaje aue watu ishirini, Denis alikuwa ameshaingia chumbani, mwanae France alikuwa amesha pitiwa na usingizi, yeye usingizi uligoma kabisa, akachukuwa pombe kwenye friji na kuendelea kunywa, akakumbuka kuwa mkewake aliingia garage usiku hule akiwa na begi dogo jeusi, akutoka nalo na polisi hawajaliona, akainuka haaraka na kwenda kule garage wanakopark gari lao aina ya Toyota Noah, akaanza kutafuta lile begi pale anapolionaga sikuzote, lakini akuliona, alitumia muda mrefu sana lakini hakuliona kabisa, akajilahumu kwanini hakuwai kulipekua ata siku moja, toka siku ameanza kuliona, akarudi chumbani na kujilaza kitandani huku akiendelea kunywa bia, akianza kuwaza miaka miwili nanusu nyuma, kipindi alipokutana na Jackline mama France, enzi hizo akiuza mama ntilie, akavuta kumbukumbu jinsi ya siku ile alipo mwona usiku akikimbia watu waliokuwa wanataka kumbaka, nyumbani kwa mama aliekuwa anakaa naye, ndipo alipo amua kumsaidia, ikiwa pamoja na kuwaudumia wazazi wake waliopo Songea, wakitegemea msaada wa mtoto wao Jackline, japo hakuwai kuwaona walakukutana nao, lakini wazazi hao walitokea kumpenda na kumshukuru sana, aliwaza mengi sana Denis, lakini hakuona dalili ya kwamba mke wake ni muuwaji, wa idadi kubwa ya watu tena nizaidi ya hapo, maana walisema zaidi ya ishirini, Denis akakumbuka kitu, akainuka na kuchukuwa simu ya mkewake, akatafuta namba iliyoandikwa baba, akaipiga iliita kidogo alafu ikapokelewa, “hallow Jackline, nipe ripot” aliongea mtu waupande wapili kwa namna iliyo mshangaza kidogo Denis “haaa! nimimi mzee, shikamoo baba” alisema Denis huku akianza kuingiwa na shaka kidogo, “ho! Samahani bwana kumbe ni Denis, m naendeleaje huko” aliongea huyo mtu ambae yeye alizani kuwa ndie mzee Nyati “mzee huku siyo salama kabisa, yani na shindwa kuelewa kabisa” hapo Denis akamsimulia baba mkwe, jinsi mwanae alivyokamatwa napolisi, na kosa aliloambiwa kuwa Jackline kalifanya, “ila kabla hajakamatwa aliniambia nikujulishe kuwa kazi ameimaliza” alimaliza kusimulia Denis “vipi lile beg jeusi amekuachia, au polisi wamelibeba?” Denis alistuka tena, inamaana huyu mzee anaweza kuwa anafahamu kilichotokea “polisi hawaja lichukua, nazani amelificha humu humu ndani?” akuwa nanamna Denis ilimbidi ajibu tu! “ok! sikia Denis, wewe nimwanamume na Jackline nimke wako, tuliza hakili, mimi na safiri usiku huu kuja Dar es salaam, nitakupigia simu asubui nikishafika dar tujuwe la kufanya, chamsingi beba simu ya Jackline sehemu yoyote utakayoenda” aliongea baba yake Jackline kwa sauti ya uturivu, bila wasiwasi wowote, akimaanisha anacho kisema, japo Denis aliona kuwa mzee huyu anaongea ndoto, kwa sababu hakuwa na uwezo wakusafiri toka songea usiku ule, hasinge pata usafiri pia hasinge kuwa na pesa za kusafiria mpaka yeye atume, siku zote walimtegemea yeye, kwa fedha za matumizi japo hakuwai kumwona kwa macho baba mkwe wake, zaidi yakuwasiliana kwenye simu, ***** Asubui na mapema Denis alikuwa njiani akielekea mjini, mwanae France alikuwa amelala kwenye siti ya nyuma ya noah akiwa amefungwa kwenye kiti special cha watoto, likuwa saa kumi na mbili nanusu foleni yaubungo ilikuwa imeshakuwakubwa magari yendayo mikoani yalikuwa yakitililika kwafujo kutoka nje ya jiji, denis alishasimama kwa muda wa dakika kumi akisubiri traffic aruhusu magari yaendayo katikati ya jiji, mala akasikia simu ikiita, simu ya Jackline anapiga baba yake, akaipokea “shikamoo baba habari za songea” alisalimia Denis baada ya kupokea simu “marahaba Denis, legeza lock ya mlango wa mbele wa abiria” Denis hakuwa ameelewa akageuza macho huku na huko “unasema ni…” aliuliza kwa mshangao, “hacha kuangaika Denis, foleni karibu inaruhusiwa ebu! Toa lock ya mlango wa kushoto” aliongea baba Jack au babu yake France kwa sauti ya utulivu tofauti na alivyo mzowea siku zote, uwa anaongea sauti flani ya uchanganfu sana ule wa kizee, Denis akatoa lock ya mlango wa kushoto wa gari lake, na sekunde chache baadae akashangaa kuona mlango ukifunguliwa na akaingia mtu mmoja, akiwa amevalia kofia ya duara, jangle hut (super fry) iliyo ficha sura yake kidogo, akuonyesha kuwa ni mzee sana, na wakati huo huo, foleni ikafunguka, magari yakaanza kutembea, lakini Denis akabaki ameshangaa ata asione kama magari yanatembea, “endesha gari, u” aliongea yule mtu ambae akuonyesha uzee wowote, baada ya kuona Denis kishangaa bila kuendesha gari, na magari mengine yakipiga honi kumstua, wakizani amesinzia, Denis akaondoa gari, yule jamaa mtu mzima akatoa kofia kichwani kwake, aikuwa sura ngeni sana kwa Denis, ni kama kuna sehemu alishawaai kumwona, akufanana na jinsi Denis alivyokuwa akiwaza, juu ya baba yake Jackline “naitwa Michael Fransis Nyati, au baba Jackline, au babu yake France” aliongea yule jamaa kwa sauti tulivu sana, na yaupole, HAYA WADAU STORY NDO INAANZA HIVYO, NI KWELI JACKLINE NI MUUWAJI, NA IMEKUWA JE DENIS ASIJUWE KAMA MKE WAKE NI MUWAJI,? NI KWELI HUYU NI BABA MZAZI WA JACKLINE AMEFIKAJE TOKA SONGEA, DENIS AMEWAI KUMWONA WAPI HUYU MZEE?, INAKUWAJE ANAMWONA TOFAUTI NA ALIVYOKUWA ANAWAZA JUU YA WAZAZI WA MKEWAKE, HUU NIUTANGULIZI TU! WA STORY HII KUPATA KISA KAMILI COMMENT LIKE, ENDELEA KUFWATILIA #DADA_MDUNGUAJI

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.