Enyi bado wanafunzi, siku yenu itafika,
Msijifanye wazinzi, wakupita mipaka,
Mtajiona washenzi, kutakapo pambauka,
Jiepusheni na ngono, hadi mfunge akidi,
Ewe dada nakujuza, nawe kaka nisikie,
Aloeleza ajuza, mabaya musirudie,
Jiulize na kujaza, mazuri muyafikie,
Jiepusheni na ngono, hadi mfunge akidi,
Mwenzio wamtongoza, akutimizia haha,
Tena anakuongoza, hadi yaliko mapaja,
Nyinyi mnajipoteza, na mabaya yanakuja,
Jiepusheni na ngono, hadi mfunge akidi,
Je tuwaiteni mama, baba au wanafunzi?
Shuleni mnakuhama, mwenda kufanya mapenzi,
Yatimiapo majuma, tumbo la pata mwenzio
Jiepusheni na ngono, hadi mfunge akidi,
Hizo mimba za mapema, kisa ni huno michezo,
Peke yako utahema, kwa hayo yako mabezo,
Kitoto utakitema, ukione na mbonizo,
Jiepusheni na ngono, hadi mfunge akidi,
Mwisho mwisho nimerichi, mike gona nayaacha,
Jueni mbivu na mbichi, kabla hakuja kucha,
Huno kalamu siachi, hadi nyinyi kuyaacha,
Jiepusheni na ngono, hadi mfunge akidi.
NA: Mike Gonard
©️jb sons media™️ 2013
Ukweli mtupu
ReplyDeleteHongera malenga
Kabisa
ReplyDeleteYour Thoughts