MRUDIE MUUMBA WAKO

Umeshakuwa malaya, stadi na maarufu,
Africa hadi ulaya, unazo sifa sufufu,
wasema wewe ni yaya, mwenye moyo mkunjufu,
ndugu bado ni mapema, rudi tubu kwa jalali,

Wizi ka umesomea, kweupe weye waiba,
hujui unakosea? Binadamu kuwakaba,
kwa mungu hutaingia, ukiendelea kwiba,
ila bado ni mapema, rudi tubu kwa Rabana,

Wazini ndani ya ndoa, hata mchana kweupe,
hayo mapepo kemea, yakutoke na yasepe,
ila ukiendelea, utaenda kwa tope,
Ndugu bado ni mapema,rudi tubu kwa jalali

Wachawi nanyi acheni, hayo maurogi yenu,
msiabudu shetani, eti kama mungu wenu,
shida zitawapateni, na hizo jeuri zenu,
ila bado ni mapema, rudi tubu kwa Rabana

Uovu muuacheni, na mutubu kwa Jalali,
mema nayo mutendeni, kuyakuza maadili,
hayo yamewatosheni, toka kwangu Manueli,
na mapema mutubuni, uovu muuacheni.

Na: Emmanuel Charo
©️jbsons media™️ 2019


Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Your Thoughts