DADA MDUNGUAJI EPISODE 3
September 17, 2022
0
DADA MDUNGUWAJI
EPISODE 3
STORY NA Mbogo Edgar
ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI : ndipo Denis akatafuta sehemu nzuri karibu na bar, akaparki gari, Jackline akamtazama kwa umakini sana, akujuwa yule kijana mlevi anataka kufanya nini, Denis akamgeukia Jackline, ambae alikuwa amekaa seat ya nyuma, huku akiachia tabasamu lake la kilevi, hapo Jackline akaona kuna dalili ya kujeruhi mtu au kuuwa kabisa, maana alihisi kuwa huyu kijana mlevi ameingiwa na tamaa ya kimwili, endelea ......
“vipi.. we! mdada..umesha kula” aliongea Denis kwa sauti kilevi levi, Jackline akashusha pumzi kwanguvu, ni kweli Jackline njaa ilikuwa imemkamata, maana tokea alipo kuwa amekula mchana pale Mapambano bar, Jackline akatabasamu kidogo, na kusababisha vijishimo kujitokeza kwenye mashavu yake, na kufanya sura yake izidi kuwa nzuri, “kweli kaka yangu, nina njaa sana” aliitiakia Jackline, akiendelea kumsoma huyu kijana, ambae aliduwaa kidogo akimkodolea macho usoni, kabla ajafunua kwenye mkebe wagari, yani kwenye dash board, akachomoa noti mbili za elfu kumi, kati ya noti nyingi zilizomo ndani ya kile kikebe, kisha akakirudishia kifuniko chake, kisha akashuka nakuelekea kwenye hile bar iliyopo maeneo hayo maalufu kwa jina la full dose, wadau wengi wanajiuliza kwa nini inaitwa hivyo, ni kwasababu ya mambo yanayo fanyika maali hapo, Denis alipotelea ndani ya bar, akimwacha Jackline ndani ya gari, jackline mle ndani ya gari akapandisha gauni lake na kuchomoa simu, kwenye mfuko wakikaptula chake cha jinsi haraka, na kumpigia baba yake, huku akiangalia kule alipo elekea Denis “baba nime uwa vijana wa tatu, waliokuwa wanajaribu kunibaka” alongea Jackline kwa sauti ya chii yenye tahadhari kubwa, badaa ya baba yake kupokea simu, “je ulionekana namtu yoyote?” aliuliza baba yake na Jackline akamsimulia tukio zima lilivyokuwa, mpaka alipo pata msaada wa huyu kijana mlevi, “ok! sasa kajifiche kwa huyo kijana, ila uwenae makini sana, akikisha agunduwi lolote kuhusu wewe” aliongea baba yake Michael Nyati kwa msisitizo “sawa baba” Jackline alikata simu na kuiweka kwenye kikaptula cha jinsi ndani ya gauni lake chakavu, mle ndani ya gari akiwa amebaki peke yake, Jackline alimtafakari sana huyu kijana mlevi, kuna mambo machache aliya gungua juu ya huyu kijana, la kwanza ni kwamba huyu kijana anapenda sana pombe, pengine kwa kuwa akuwa na familia, au amesababishiwa na kitu ambacho kime mfanya asiwe na familia, la pili nimcheshi sana, la tatu ni mtu mwenye moyo wa kutoa msaada na mwenye huruma sana, sababu alijitolea kumsaidia japo akujuwa ni kwasababu gani alimpatia huo msaada, labda kwa ajili ya matamanio ya kingono, au ni ulevi ndio ulimfanya kutoa msaada bila kujijuwa, na kwa mtu asiye mfahamu, lakini tokea wameingia kwenye gari mpaka hapa walipo, akuonyesha dariri ya kuendekeza ngono, sababu ata naongezi yao yalikuwa ya kawaida tu!, “mh! ngoja tufike, akianza ujinga tu! nayeye atakiona cha moto” aliwaza Jackline, Denis alikuwa ana rudi, huku amebeba mifuko midogo mitatu myeusi ya rambo, akamkabidhi Jackline “yote hii ya kwangu” alishangaa Jackline huku anapokea “ndiyo..kwa..kwa sababu siku kuuliza utakula nini.... nimeeee..amua kubeba ili ujichagulie mwenyewe, utakachokula” alijibu Denis kilevi huku akichomoa kopo moja la bia kwenye katoni lake, na kuifungua kisha aka gugumia mafundo mengi mfurulizo, alafu akaiweka sehemu ya kuwekea vinywaji mle ndani ya gari, kisha anaingiza gia ya kuondokea, na kuliingiza gari barabarani, na kukanyaga mafuta kufwata uelekeo wa kibamba kwa mwendo wa fujo, akimfanya Jackline ashindwe kula, akabaki ameshikilia vifuko vya chakula, ***** Mtaa wa manzese Tip Top polisi walikuwa wamezagaa, wakimsaka dada mwenye mabegi, wakati huo huo inspector Johnson alikuwa anaingia akiwa na askari wake kumi na magari mawili, aina ya land lover 110, baada ya kupewa taharifa ya kutokea mauwaji maeneo ya manzese, karibu na eneo yalipotokea mauaji ya mchungaji Chilumba, asubuhi ya siku hiyo, magari yapolisi yalisimama mbele ya mapambano bar and guest house, wale askari wakiwa tayari kimapambano, waliruka na kujipanga kulizunguka lile jengo la bar, huku Insp Johnson akiingia ndani ya ile bar, akikaribishwa na mkuu wa kituo kidogo cha manzese, na kumwongoza moja kwa moja, kwenye chumba ambacho ile miili ya vijana watatu ilikuwa bado hipo chini, insp Johnson aliitazama kwa dakika kadhaa huku akijaribu kutafakari ili na lile, “ina maana aliyo ya fanya haya ni mwanamke?” Insp Elenest alimwuliza mkuu wa kituo, “ni kwa mujibu wa maelezo ya mhudumu wa vyumba, kuwa aliefanya haya ni mwanamke kutoka jijini ambae alikuja hapa tokea jana” alijibu mkuu wakituo, “yupo wapi huyo mhudumu?” aliuliza insp Elenest “yupo huku pamoja na wahudumu wengine, tuliwaifadhi kwenye chumba kimoja” alijibu mkuu wakituo, na hapo ilitolewa amri kuwa aitwe ule mhudumu wa vyumba, aliitwa yule dada mhudumu wa vyumba, alikuja akiwa amevimba usoni huku damu zikiwa zime gandiana sehemu kubwa ya pua na mdomo wake, kutokana na kichwa alichopigwa na Jackline, “awa vijana walikuwa wana fanya nini chumbani kwa mwanamke na mapanga mkononi?” hilo swali alikuwa na jibu kwa huyu manamke, maana alijuwa akisema ukweli na yeye angeozea jela, “sijuwi, mimi niliwaona wanaingia tu! nikajuwa ni wenzake” Insp alimuoji maswali machache yaliyo mfanya agundue kuwa yule dada alichukuwa chumba, jana yake jioni aliandikisha jina la Sikujuwa Saidi, anatokea bagamoyo anaelekea mtwara, akuandika kazi wala namba ya kitamburisho, licha a kunduwa hayo, lakini kuna maswali yalimchanganya sana insp Johnson, kwamba inaonekana hawa vijana walikuwa na nia ya kumzuru huyo mschana, akawazidi nguvu, je? huyo manamke ni nani anauwezo kiasi gani cha kuichinja midume mitatu kama kuku? ****** saa nne za usiku, Jackline alikuwa amesha fika nyumbani kwa kijana mlevi, alikaribishwa ndani na mwenyeji wake mlevi, Jackline akiwa pamoja na mizigo yake, akaingia ndani, huku akiitazama ile nyumba kwa umakini sana, walifika na kukaa sebuleni, Jackline alimwona mwenyeji wake akimkaribisha kwa sauti ya kilevi iliyo jaa ukarimu, akaletewa maji ya kunywa na kunawa pamja na soda, kwaajili ya kupata msosi ule alio kujanao, toka full dose, Jackline baada ya kulizika na maandalizi na ukalimu wa mwenyeji wake cha pombe, akaanza kula vyakula vyake kwenye mifuko, chips mayai pamoja na nyama za kuku wa kukaangwa na mishikaki ya ng’ombe, Jackline alikula huku akiendelea kuingalia ile nyumba, kwandani ilikuwa nzuri sana yenye vitu vya thamani na vizuri, alishangaa kuona yule kijana licha ya kuwa mlevi, lakini alikuwa amejijenga vizuri kimaisha, Denis muda wote tokea wameingia humu ndani, alikuwa amekaa kwenye kochi pembeni ya Jackline, akinywa pombe zake alizo zibeba, huku wakimwongelesha mwenyeji wake mambo mawili matatu kuna kipindi wakawa kimya kabisa, Jackline akitafakari machache kichwani kwake, juu ya kazi aliyopewa na baba yake ya kutoa roho za watu sita, mpaka sasa ni mmoja alie mpoteza, lakini kun watu wengine watatu tayari, wamesha msindikiza mchungaji Chilumba, baada ya kuwaza ita kuwaje mpaka anawamaliza hao watano waliobaki, atakuwa amewauwa wangapi, kisha mawazo yake yalirudi kwa huyu kijana mlevi, kwanini licha ya kuishi kwenye nyumba kubwa kama hii lakini haja oa na wakati umri una mruhusu, Jackline akaamua kuvunja ukimya “eti! Kaka, kwanini ujaoa mpaka leo” kimya Jackline akujibwa, akamtazama mwenyeji wake, akamwona akiwa ameegemea kochi amesinzia, sekunde chache baadae akasikia akikoroma, “amepitiwa na usingizi”, Jackline akacheka kidogo, kisha akajisemea “mgeni siku ya kwanza, analala sebuleni” Jackline alitikisa kichwa chake, na kucheka kidogo,
Jakline aliendelea kula mpaka alipo maliza, kisha akatafuta bafu lilipo, alipo lipata akajaribu kufungua maji ya katoka, Jackline akaoga haraka kisha akarudi sebuleni, alimkuta Denis ambae bado akuwa akimjuwa jina mpaka muda ule, akiwa bado amelala vile vile kama alivyo muwacha, alicho fanya ni kulinyanyua lile begi lake dogo jeusi na kutafafuta sehemu nzuri ya kuliifadhi, alizunguka mpaka akafika kwenye store iliyojaa vifaha vya ujenzi, akalihifadhi humo, kisha akaanza kuikagua nyumba nzima kwa ndani, akagundua ilikuwa ni nyumba kubwa ya vyumba vinne, yenye jiko na sehemu zote muhimu kwa nyumba za familia, pia ina milango mitatu ya kutokea nje, alipomaliza akarudi sebuleni, akamkuta mwenyeji wake ametopea kwenye usingizi, akikoroma, Jackline akaenda kwenye kochi moja kubwa, kati ya makochi seti mbili (sofa) ya kisasa ya mle ndani, na kujilaza akimwigiza mwenyeji wake, **** Michael Nyati akiwa na mke wake Anitha au mama Jack, walikuwa bado sebuleni mama Jack akiwa amejilaza kwenye mapaja ya mume wake, macho kwenye tv, wakijaribu kufwatilia habari zilizotokea leo, alipata kusikia tukio la kuuwawa ya askari mstaafu wa jeshi afisa mteule Chilumba, ambae alijulikana kama mchungajiwa kanisa la kilokole, alipata kushuhudia polisi wakitoa taarifa hiyo, waki haidi kumsaka muuwaji mpaka watakapo mtia nguvuni, muda wote Michael alikuwa ametabasamu, “hivi huyu Jack amesha fika huko anakoelekea na huyo kijana mlevi” aliuliza mama Jack, bila kujibu Michael au baba Jack aliinua kitu mfano wa simu kubwa mezani na kuitazama, akabonyeza kidogo, kisha akamwonyesha mke wake “inaonyesha wameshafika, ni maeneo ya kibamba njia panda ya shule,” aliongea baba Jack akirudisha kile kipad mezani, “naimani atamaliza kazi vizuri, japo vikwazo ni vingi sana, maana amewauwa vijana watatu waliojaribu kumbaka” aliongezea baba Jack, mama Jack naye akadakia “tena na huyo aliejifanya kumsaidia ajiangalie, akileta ujinga wamapenzi atapotea” walicheka wote huku Anitha au mama Jack akianza kusinzia ***** Asubuhi na mapema mida ya saa kumi na mbili na nusu, Jack alistushwa na pilika pilika za Denis, akijiandaa kwenda kazini, Jackline akajifanya bado amelala, alikuwa juu ya kochi kama alivyolala jana usiku, akamwona yule kijana mlevi akiwa mevaa vizuri akijilekebisha tai shingoni, wakati akitokea kenye chumba kimoja cha mle ndani, akaiendea friji na kutoa soda moja ya kopo aina ya cola, ni zile alizokuja nazo usiku, akainywa kwa kuigugumia mala mbili mfurulizo, ikawa imekwisha, Jackline akamwona mwenyeji wake akichukua kopo jingine la soda kwenye friji, kisha akachukua makopo mawili ya bia, zile alizobakisha jana mezani, akataka kutoka nje akaonekana kama amekumbuka kitu, hapo Jackline akamwona akiyaweka yale makopo mezani, kisha akaingia kwenye chumba alichotoka mwanzo, akutumia muda mrefu akarudi na shuka mkononi, Jackline alimshuhudia yule kijana mlevi akimfwa pale alipolala, kisha akamfunika na ile shuka, ni kweli kulikuwa na kaubaridi flani, alafu yule kijana akaingiza mkono mfukoni akatoa wallet nakuifungua, akachomoa noti tatu za elfu kumi kumi, na kuziweka mezani, akazikandamizia na kopo moja wapo la bia, kisha akamwona akiinua makopo yake ya soda na bia na kutoka nayo nje, muda mchache akasikia muungurumo wa gari likiondoka, Jackline akafungua macho yake, akabaki amejilaza juu yakochi akitafakari machache, juu ya huyu kijana mlevi, akupatajibu, akajaribu kutafuta usingizi lakini aukuja tena, akaamua kuamka, akakunja shuka nakulipeleka kwenye kile chumba alichoingia yule kijana mlevi wakati akijiandaa, Jakline akakitazama vizuri kile chumba akagunndua kuwa kilechumba ndicho cha mwenyeji wake, japo kilionekana smati kama kilikuwa akitumiki sana, alipotoka mle chumbani akavua lile gauni lake, akabaki na kikaptula cha jinsi na tishert, akaanza mazoezi ya viungo ya kupasha mwili, pia akapiga push up nyingi sana, akamalizia kwa mazoezi ya ngumi aina ya gou jo lou, na Tai kwondo, alipo maliza akaingia bafuni kuoga, alipomaliza akaanza kufanya usafi, nyumba yote, maana ilionyesha kuwa aifanyiwi usafi mala kwa mala, alikagua jikoni akakuta kuna vifaa vyote vyakupikia, ikiwepo jiko la gesi na umeme, pia jiko la mkaa na mkaa wenyewe, masufuria ya kila size, na vingine vingi, **** Michael Nyati alikuwa amesha amka, amekaa mbele ya TV akitazama kipindi cha magazeti, habari kubwa ilikuwa ni, mauwaji yaibuka dar, mchungaji maarufu auwawa, na nyingine ikiwa ni, mauwaji kwenye guest manzese, habari hizo ziliambatana na picha, Michael aliangalia picha za magazeti ambayo yalikuwa kipita pale kwenye TV, huku akisikiliza zile habari zikisomwa kwa kifupi, habari moja ilimvutia sana bwana Michael, iliyosema kuwa viongozi wa dini watoa tamko juu ya mauwaji ya mchungaji Chilumba, habari hii iliambatana na picha ya watu watatu wakiwa wamesimama, alichoweza kuona ni jina la gazeti kisha ile habari ikapita, alitaka kujilidhisha na ukweli wa alichokiona kwenye picha, akaagizia gazeti mjini haraka sana.....
Wakati huo Denis naye alikuwa anapark gari lake kwenye maegesho ya kazini kwao manzese, nje ya jengo la Mazao, akaliangalia gari la rafiki yake Mahadhi kama alikuwa ameshafika, akuliona alikuwa bado ajafika, akashuka kwenye gari, akiwa na makopo mawili matu ya bia, alizo kuwa amezinywa njiani, akafunga vizuri Milano ya gari lake aina ya Toyota Noah, kisha akapitia kwenye debe maalumu la kutupia taka taka, (garbeg bin) akayapupa yale makopo, na kuelekea ndani ya jengo, muda wote alikuwa akimuwaza yule dada mama ntilie alie mwacha nyumbani kwake, huku mpango wake ukiwa ni kwenda kutoa udhuru ofisini, ili akakae namgeni wake, ikiwezekana ajaribu kumweleza jinsi anavyo jisikia moyoni mwake, maana jana akuweza kuongea nae vizuri, baada ya kupitiwa na usingizi, na ukichukulia kutongoza kwake ilikuwa kazi ngumu sana, maana toka alipo tongoza kipindi yupo shuleni, na siyo kwamba alitongoza ni kwamba mwanamke alijilengesha mwenyewe, Denis akiwa bado anapandisha ngazi, akasikia sauti ya Mahadhi akimwita toka nyuma yake “vipi kaka inamaana ukuniona wakati napark gari?” aliongea Mahadhi huku akipandisha ngazi haraka haraka, nusu ya kukimbia, “haa! nimeangalia gari lako sijaliona, nikajuwa bado ujafika” aliongea Denis hulu akisimama kumsubiri mwenzie, “basi ile wewe una toka tu! hapo park, na mimi naingia, nikajuwa umeniona ila una muwai Janeth” wote wakacheka, Janethi ni secretary wa boss wao, waliongea mengi sana huku wakipandisha ngazi “ujuwe leo sijisikii vizuri, nataka nimwambie bosi naenda yumbani kupumzika” aliongea Denis, akimdanganya Mahadhi alihisi akimwambia ukweli juu ya mama ntilie, angemtania sana, na kudadisi mambo mengi tena pengine ange taka waende wote akamwone, kwa sababu Mahadhi akumwona yule mdada jinsi alivyo mzuri, “mh! au mtungi wajana ulikuzidi, tena hapo ulipo una arufu ya pombe, kama umetoka kuongezea sasa hivi” aliongea Mahadhi kwa sauti ya chini, maana ndio walikuwa wakiingia kwenye ofisi yao “ho! Wanaume ndio mnaingia kazini” walipokelewa na Janeth secretary wa boss wao, alie kaa kwenye kiti chake cha kuzunguka, mbele ya meza kubwa, yenye computer na makablasha kadhaa, huku TV, kubwa ikiwa kwenye kona moja ya chumba kile kikubwa cha mapokezi, “leo kijana wako amewai hen?” alichombweza Mahadhi, sababu anajuwa kuwa siku zote amekuwa akimshobokea Denis, lakini Denis akuwa tayari kusawazisha, “nimeona, tena leo Denis kapendeza sana, nitampa offer ya lunch mkirudi” alibwabwaja Janeth akiendelea kuweka vitu vyake sawa , tayari kwa kazi, “tukirudi?, tukirudi Kutokawapi?” aliuliza Denis kwa hamaki, na mshangao, wakati mwenzie Mahadhi, alishangaa kimya kimya, maana awakuwa na safari yoyote ya kikazi leo, “boss ameniagiza kwamba, mkifika tu! nendeni kwa mhasibu, mkachukue fedha kwa ajiri ya mafuta ya gari, kisha muende kisalawe, kuna wahindi wanataka kujenga gholofa, mkaiangalie site, malipo ya ziada mtayapata huko huko” Janeth aliwakabidhi na namba za simu, za hao wahindi, kiukweli Denis hakuwa na namana ilibidi aifanye hiyo kazi, maana licha ya kuwa na ujuzi zaidi ya mahadhi wa kuset majengo ya kuyasanifu, pia ilipo tokea kazi kama hiyo uwa wana ipwa fedha nyingi sana, wakaondoka mala moja wakitumia gari la mahadhi, wakiofia kutumia la Denis kutokana na kukosa side morror *** saa mbili asubuhi, Jackline alikuwa amemaliza shuguli zake, sasa alikuwa ametulia kwenye kochi amewasha TV akiangalia habari za matukio na michezo, alikuwa amesha fahamu jina la yule kijana mlevi, ni baada ya kupekua na kuchunguza chumbani kwa yule kijana mlevi, alikuwa anaitwa Denis Edgar Mbogo, akajuwa kuhusu kazi yake, kuwa ni msanifu wa majengo na mbunifu wa ramani za majengo ya aina zote, kingine alicho gunduwa, ni kwamba mle ndani ya nyumba hapakuwa na dalili ya kuwa kuna mwanamke aliwai kuishi, Jackline akiwa anaangalia TV, mala akastushwa namlio wasimu yake, akaitazama kwenye kioo, “baba, hooo! shit!” alikuwa amesahau kumpa report ya asubuhi kama alivyo agizwa kufanya kila asubuhi “hallow! shikamoo baba” aliongea kwa utulivu Jackline, mala tu baada ya kupokea simu, “malahaba mwanangu, naona leo umelala sana ugenini, vipi hupo peke yako?” tofauti na alivyo tegemea, baba yake aliongea taratibu na kwa upole “ameenda kazini, nimebaki mwenyewe” aliongea Jackline, wa sauti tulivu huku anainuka na kuchungulia nje ya dirisha, “ok! sikiliza maelekezo, kuna target imeonekana, inabidi uifwatilie” baba mtu aliongea na kuanza kutoa maelekezo **** Saa mbili nanusu Ndani ya kituo kikuu cha cha polisi, Inspector Johnson David alikuwa amesimama mbele ya askari kumi, wakiwa na vyeo mbalimbali, wakiwa wamejipanga mistari miwili, walio valia mavazi ya utayari kimapambano, na bunduki zao aina ya SMG, zikiwa mabegani mwao, Inspector Johnson David alipewa report na askari mwenye cheo cha sajenti, kuwa wote wapo na wapo tayari kwa kazi, akaamuru waingie kwenye magari kisha uelekeo asubuhi ile ni kule manzese ya lipo tokea mauwaji ya mchungaji Chilumba, kwenye jengo la Kamanga Plaza, kumbe baada ya kuwaza sana Inspector Johnson David, akakumbuka kuangalia security camera za jengo la pembeni na Kamanga Plaza, linalojulikana kama Mazao Building, ambalo muuwaji alitumia kumdungua mchungaji, safari ikaanza kuelekea manzese, **** saa tatu kasolo Jackline alikuwa njiani, kwenye kituo cha daladala cha kibamba njia panda ya shule, akisubiri mabasi aina ya Toyota coster, yatokayo nje ya mji kibaha chalinze mpaka msata na mkata, akiacha hiace ambazo utumia muda mrefu kufika mjini, kabla ya kuingia kwenye basi alinunua gazeti moja, kwenye meza za wauza magazeti, walipo eneo hilo la kituo cha daladala, leo alikuwa amevaa gauni moja kubwa kama la jana, lakini hili lilikuwa jipya kidogo lililo shonwa kwakutumia kitenge, pia begani alitundika upande wa kitenge, na mwingine akiwa ameufunga kiunoni, kichwani mwake akiwa amejifunga kilemba kibwa cha upande mzima wa kanga, nakumfanya azidi kuonekana mzuri zaidi, leo Jackline, akuwa na begi jeusi, ila kama kawaida yake, ndani ya gauni lake la kitenge, alivaa kikaptula chake cha jinsi, akiwa amenig’iniza bastora yenye silence baller na upande mwingine, kisu kikali cha kijeshi, aikuwa lahisi basi kustukia kutokana kuzibwa na ukuwa wa hipsi na makalio yake ya kuvutia, gari lilifika na Jackine akapanda, akiwa na gazeti mkononi, alifwata seat iliyo kuwa wazi, na kukaa, kisha aka geuza gazeti lake, ukurasa wambele kabisa, kulikuwa na picha ya watu watatu, na kichwa cha habari ya picha hiyo kilisema, viogozi wadini watoa tamko kifo cha mchungaji Chilumba, akasoma maandishi chini ya picha, ni kweli ya liwatambulisha wale watu wa kwenye picha, Jackline hakuwajari wale wengine, yeye alimjari wakatikati, maana wakulia tayari alisha kufa ni mchungaji Chilumba, wa kushoto msaidizi wa mchungaji Kileo, ambae ndie alie mkusudia katika ilepicha, japo maelezo ya baba yake ni kwamba, aende akamfwatilie apajuwe anapoishi, kisha ajuwe watu atakao kutana nao, pengine ange wajuwa wengine zaidi, kisha baada ya hapo ndie awe wapili baada ya mchungaji Chilumba, **** Denis na Mahadhi tayari walikuwa kisalawe, kwenye site wakiseti jengo ambalo ina bidi lijengwe hapo, namna jengo litakavyo kaa, ili wakaichagulie ramani moja wapo kati ya nyingi zilizopo ofisini kwao, awakutumia muda mrefu sana mahali hapo, wakakubariana na wateja wao, ambao waliwaelekeza waende upanga (mtaa) ambako zipo ofisi za wateja wao, kwa ajili ya malipo ya ziada, wakaingia kwenye gari na kuanza safari, walitumia gari la Mahadhi gari la Denis walilihacha ofisini kwa kuwa alina side mirror moja, ambayo Denis alipanga akisha toka upanga achukuwe gari lake akatafute side mirror kwenye maduka ya spare za magari, kisha aelekee nyumbani kumuwai mgeni wake, ambae jana usiku alishindwa kuongea naye kutokana na kupitiwa na usingizi, ‘hivi Denis unajuwa kuwa jana yame tokea mauwaji mengine, mitaa ya ile karibu na bar tuliyo kuwa tume kaa jana usiku?” alongea mahadhi lakini Denis akustuka, “mbona mimi sikuona, au nilikuwa tungi sana?” aliliza Denis huku akitamani kumaliaza mizunguko mapema apate chakula na bia ata mbili hivi, “mimi mwenyewe nimesikia asubuhi hii, wengine wana sema kuna demu sijuwi ni jinni, lime uwa watu watatu, yani midume kabisa, na mapanga yao” hapo Denis akacheka sana, kiasi cha ku shangaza Mahadhi, “ina maana mimi naongea upuudhi?” aliuliza Mahadhi kwa hamaki akionekana kukasilishwa na kitendo cha Denis kucheka namana hile, “hilo ni kwanyinyi wazinzi, weunazani jinni lina mpenda mlevi?” hapo wote wakacheka, huku safari ikiendelea, **** Inspector Johnson David alikuwa mbele ya computer za chumba cha usalama, cha jengo la Mazao, akiwaangalia sana watu walioingia na kutoka ndani ya jengo ilo jana, muda ambao mauwaji yalitokea, baada ya kupitia HDD za computer zinazoendesha camera za usalama kwenye lile jengo, kwamuda mrefu sana, akuna alichokiona zaidi ya mschana mmoja alievalia gauni cha kavu, huku amebeba sahani mbili za chakula, na begi dogo jeusi kwa pani, lakini awakujua alikoelekea zaidi ya kumwona akirudi nje akiwa na sahani tupu, hapo Inspector akatia shaka kidogo, juu ya yule dada, maana alificha sura isionekane kwenye camera, unge zani ni mtu ambae alijuwa uwepo wa camera zile ndani ya jengo lile, ila mwonekano wa yule dada wakifukara, ukamfanya apotezee yale mawazo yake ya kumtilia shaka, akaona bora aende hospital ya muhimbili, ambako mwili wa marehemu Chilumba na wale vijana watatu ilihifadhiwa, japo miili ya wale vijana wabakaji aikuwa mihimu kwake, ilihifadhiwa hapo kwaajiri ya uchunguzi zaidi na kusubiri mazishi, na yeye aliamua kwenda kupata report ya madaktari, maalumu, toka kwenye jeshi la polisi, baadea ya kushuka toka kwenye dala dala, kituo cha buguruni rozana, jackline akaanza kutembea kuelekea msibani, kwenye kanisa la mch Chilumba, akatoa simu yake, na kumpigia baba yake, ambae alimweleza kuwa ameshalipata gazeti na sasa anaelekea msibani, hile kutaamaki
akashangaa simu yake imekwapuliwa na kijana mmoja, ambae litimua mbio na kutimua mbio, kilikuwa kitendo cha ghafla, kama kipanga anavyo pitia vifaranga vya kuku, huku yule kijana aifwatiwa na mwenzie, na sasa wakawa wawili, hapo Jackline akatabasamu, pasipo kupiga kelele za mwizi, kama wafanyavyo watu wengine wanapoibiwa, akatazama kusoto na kulia, akaona watu wachache tu! wakimtazama bila msaada wowote, hapo Jacklini akainama na kushikilia gauni lake kwa chini, akainua gauni lake na kulishikia kwa juu, na kuanza kuwa kimbilia wale wezi, kwani aliangalia mbio za wale vijana, akaona zipo ndani ya uwezo wake, , “weee dada usuwafwate weweeee” zilisikia sauti za watu kimtahadharisha Jackline kuwa asiwafate wale vijana, ambao walikimbia mbio nakuingia kwenye vichororo vya hapa buguruni, upande wa kwa mzee malapa, wakidai itakuwa hatari sana kwake **** vijana awa wenye mwonekano wa kudhoofu, kwa matumizi ya mihadarati, walikimbia na kwenda kutokea kwenye uzio wanyumba moja, ambayo ilikuwa chakavu, na hapo waliingia kwa fujo na kuwastua wezao watatu, walikuwa wanatumia dawa za kulevya, wengine wakijichoma kwa sindano wengine walikuwa wanamisokoto ya bangi mdomoni, "hoya wana vipiiii, mnakata
stimuuuu?, mnakuja mbiiiiooo" aliongea mmoja kwa sauti ya kilevi, akiwalaumu wenzake, kwa kumwaribia starehe yake, lakini alipowaona wakiwa wameshika simu nzuri, akachanua tabasamu la kilegevu, utazani anausingizi, "hoyaaa wapi tena, meutoa uo mzigo mpya kabisa" aliuliza yule alie walahumu wenzake mwanzo, ndie alionekana kuwa mbabe wao pale, huku akinyoosha mkono ili apewe ile simu, "kuna demu mmoja hivi alikuwa na mbwela mbwela, hapo mtaa ya katat..." akuwai kumalizia maneno yake yule alie shika simu, akastulliwa na sauti toka nyuma yake, "mimi hapa" wote wakageuka kwa mstuko, baada ya kusikia sauti ya kike nyololo, hapo wote watano wakatabasamu, wakiamini wamepata kitu chabuleee, “hoyo, sikilizeni wanangu, hapa mimi mwenyewe na kuwa wakwanza, alafu ebu msachini kwanza,” maneno hayo Jackline aliyasikia, na kuzidi kumtia hasira, wale vijana ambao kwa sasa walisha fikia idadi watano, walishuhudia yule dada mrembo sana, akifunua gauni lake, na wao kuliona paja lake laini lililo nona na kuwa fanya dudu zao zisisimke, na kuanza kusimama tayari kwa kazi ya kutafuna kitumbua, kwa kitendo kile, vijana walizani, mschana mrembo ameamua kuwapa kitumbua kwa iyali yake, lakini walishangaa kuona akiibuka na kisu,"wasalimieni kuzimu" ilikuw nisauti moja ya kutisha, toka kwa mrembo huyu, **** kumbe tukio lile la yule dada kuonekana kuwa ana wakimbilia wale wezi lilionekana kwa watu pale mitaa ya rozana, kuna bahadha ya wananchi wakaonelea waende kufatilia lile tukio, lakini kutokana na sifa zakutisha za wale vijana, wakashidwa kwenda kufwatilia, watu wakiwa wame jikusanya kikundi, bado wana jadiliana la kufwanya mala waka mwona mmoja kati ya vibaka maarufu wa lile chimbo, akija maali walipo simama wao, huku ame jishika tumboni kwa mikono miwili, iliyo lowa damu, wakamshangaa akizidi kuwasogelea, kwa mwendo wa kidhaifu sana, akionyesha kuwa amezidiwa na maumivu makari sana, lakini alipo wakaribia wakamwona akiziwa na maumivu na kujibwaga chini, huku akiacia mikono yake aliyo kuwa ame jishikilia tumboni, hapo watu wakapiga kelele za uoga na kutawanika, wakiwaacha watu wachache wenye roho ngumu, wakishuhudia tumbo la yule kibaka mteja, likiwa wazi kabisa na kuruhusu utumbo wa kijana huyu, kutawanyika kama mbuzi alie pasuliwa, dakika chaahe baadae polisi walifika mahali pale, na kuuliiza kilicho tokea, wakaelezwa jinsi tukio lilivyo kuwa, mala moja polisi waka elekea kule aliko tokea yule kibaka, kwa kufwata michilizi ya damu, wakiamini wata mkuta huyo mwanamke aliekuwa anawakimbiza, huku wakionganisha na tukio la mauwaji ya jana usiku manzese, lakini walipo fika eneo la tukio, walistaajabu walicho kikuta, walikuta miili ya vibaka wanne ikiwa imelala kwenye madimbwi ya damu, huku majalaha makubwa shingoni mwao yakione kana kwa uwazi kabisa, tayari walikuwa wamesha kufa, na muuwaji akuonekana,
*** wakati wao wana wana shangaa kule kwa vibaka, Jackline alikuwa ameshafika msibani, kanisani kwa malehemu mch Chilumba, na kujichanganya na waombolezaji, akikaa upande wa wakinamama, huku macho yake ya kiwa kule walikokaa wanaume, akijaribu kufananisha sura aliyoiona kwenye gazeti, yani ya mchungaji Kileo, pale msibani zilisikika sauti za musiki kwenye maspeeker makubwa, zikipiga nyimbo za maombolezo, na matangazo ya hapa na pale, Jackline akatazama sana sehemu walipokaa wanaume, asa wenye umri mkubwa, alishuhudia waandishi wa habari mbalimbali, pamoja na vituo vya redio na tv, wakiwahoji wazee waliokuwa eneo hilo, aliweza kuwaona wazee wengi sana, lakini akuiona ile ya sura ya kwenye gazeti, ya mchungaji Kileo, muda mfupi baadae, yaliingia magari matatu, mawili yakiwa madogo meusi aina ya Range Rover, na moja basi dogo aina Toyota Coster likiwa na dereva peke yake, ubavuni limeandikwa na jina la kanisa moja lakilokole Daraja la uokovu, (jina la kubuni) walishuka watu watatu kwenye gari la pili, aina ya Range Rover, wakiwa wame valia suit nyeusi, mmoja akiwa ni mzee wa makamo, na wawili vijana walio jengeka kimazoezi, wakionekana ni walinzi wa huyu mzee wa makamo, moyo wa Jackline ulichanua kwa furaha na tabasamu la matumaini, ni baada ya macho yake kutua usoni kwa yule mzee wamakamo alie shuka kwenye gari, ambae alikuwa amevalia mewani nyeusi ya jua, alikuwa ni mwanajeshi mstaafu sajenti Kileo, ambae sasa anaitwa mchungaji Fredrick Kileo, Jackline alimwona mchungaji Kileo akielekea walipokaa wazee wenzake, ambao nao walionekana kuwa ni watu wenye uwezo wa kifedha, mchungaji Kileo akasalimiana nao, kwa kushikana mikono na kila mmoja, huku wakipeana pole, mwisho akakaa jirani na wazee mmoja alie valia suit kama yeye na miwa ni nyeusi, lakini yeye alivalia na kufia kubwa nyeusi ya duara, Jackline akawaona wakinong’onezana jambo, na dakika chache baadae Jackline alimuona mchungaji Kileo, akiinuka pamoja na yule mzee mrefu mweusi alie valia kofia kubwa ya duara, wakasogea pembeni, huku wale vijana wawili shupavu, wakiwa sogelea kidogo na kusimama pembeni yao wakiwaachia atuwa chache, ili waongee bila wao kusikia walikuwa wakiongea nini, inaonyesha ni walinzi makini wa mchungaji Kileo, Jackline aliwaona wale wazee wawili wakiongea kwa muda mrefu, wakijadiriana jambo, Jackline akaona atumie muda huo kusogea eneo hilo, pengine angesikia na kugundua jambo ambalo lingemsaidia katika kazi yake, ya kuwa saka na kuwa maliza wabaya wa baba yake, Jackline aliinuka na kuelekea pale walipo simama wale wazee wawili, akijifanya kama anatafuta kitu flani, lakini wakati anawakaribia, ghafla alishangaa amesukumwa kwa nguvu sana, nusu ya kuanguka chini, alisaidiwa na wepesi wake kutokana mazoezi aliyo kuwanayo na uimara, kujizuwia kuanguka, aligeuka haraka na kumtazama yule aliemsukuma, alikuwa ni kijana mlinzi wa mchungaji Kileo, “usisogee huko, pita kule” ilikuwa sauti kavu yakuchukiza toka kwa yule kijana shupavu, huku wale wazee wawili, pamoja na watu wengine wengi pale msibani, waliona tukio lile, waombolezaji wengi walisikitika sana,kwa tukio ile ambalo walilichukulia kama ni tukio la kinyanyasaji, “namana vijana walio jengeka kimazoezi, wakijichukulia ujiko, mbele ya bossi wao, kwa kumnyanyasa mwanamke dhaifu, aliejitolea kuja kwenye msiba wa mchunagaji Chilumba” hayo yalikuwa ni mawazo ya waombolezaji walio wengi pale msibani, ilawale wazee wawili akiwepo mchungaji Kileo, waliangalia kisha wakatabasamu, alafu wakaendelea na maongezi, Jackline alishikwa na hasira kali sana, ikamjia hamu ya kuuwa, japo akupanga kufanya hivyo mapema kiasi hiki, kama alivyo elekezwa na baba yake, maana ilikuwa ni mapema sana toka ya fanyike mauwaji ya mchungaji Chilumba, siku moja iliyo pita, yani jana, ndio maana leo aliiacha silaha yake kubwa, aliwatazama wale wazee akawaona wakiendelea na story zao, akawatazama wale vijana wawili, ambao nao walikuwa wakimtazama, nakufanya macho yao yagongane, Jackline akaachia tabasamu baya sana, ambalo tena adimu kulitoa, linapooneka ilo tabasamu uwa ni ishara mbaya sana, ata baba yake akiionaga ilo tabasamu uwa makini sana mda huo, maana kuna kitu kinaweza kutokea, ni tabasamu lililo wastua wale vijana, walinzi wa mchungaji kileo, kisha Jacklin akamwambia yule alie msukuma, alikuwa bado yupo karibu yake, kwa sauti ya chini sana “kaa tayari kaka” kisha Jackline akakunja sura na kuirudisha ile ya upole, akageuka na kuanza kurudi alikokuwa amekaa mwanzo, na kumtazama Mchungaji Kileo, ambae ndie wakatika katika ile picha kwenye gazeti, na ndie aliekusudiwa kuwa anaefwatia kufa, baada ya mchungaji Chilumba, maongezi ya wazee awa wawili hayakutumia mda mrefu sana wakarudi walipo kuwa wamekaa mwanzo, kisha wakamwita mmoja kati ya walinzi na kumpa maagizo flani, nayeye akaenda kwa mzee mmoja ambae alionekana kuwa ni muusika kwenye ule msiba, akamnong’oneza jambo, kisha yule mlinzi akarudi sehemu yake, karibu na mwenzie wakisimama nyuma ya kocho alilo kalia mchungaji kileo, dakika chache baadae likasikia tangazo, toka kwenye maspika makubwa ambayo yalitumika kupigia nyimboza maombolezo “yeyote anaetaka kwenda hasptal ya Muhimbili, anaweza kungia kwenye coster, tuungane na mchungaji kileo, ambae anaenda kuuangaia mwili wa mchungaji Chilumba” hapo Jackline aliachia tabasamu, huku akiwa mmoja kati ya watu wachache walio inuka na kuelekea kwenye basi dogo aina ya Toyota coster, “lazima kieleweke, nikipata mwanya mdogo tu! nita wafundisha adabu awa vijana” aliwaza Jackline muda mfupi tu! baada ya kuingia kwenye basi, na kukaa kwenye seat, **** inspector Johnson David aliinia ndani ya Ofisi ya kitengoo cha uchunguzi, kinacho simamiwa na madoctor toka jeshi la polisi, ambao wali mpatia majibu ya uchunguzi katika mwili wa malehemu Chilumba, “malehemu ameuwawa kwa kupigwa na risasi, aina ya hE exprosive, 7.62 mm, ya silaha aina ya sniper mugnum rifle, toka ussr, toka umbari wa mita mia mbili na hamsini, alama za vidole hakuna” aliongea Doctor wa polisi, ambae alikuwa aisoma kwenye karatasi, kisha akafunga lile karatasi na kuchukuwa jingine, “kuna hii report ya miili ya wale vijana watatu, kama ungependa kujuwa majibu yake,” alisema yule daktari, akimtazama Inspector usoni, “ni vyema ningefahamu pia” alijibu inspector Johnson David, na yule Doctor akaendelea kusoma, “vipimo vinaonyesha kuwa muuwaji alikuwa mmoja tu, alietumia kisu kikari chenye upana zero mills mpaka tatu, na meno kama ya msumeno yenye urefu wa cmm moja, ni visu ambavyo viliwai kutumika nchini, miaka ya 1985 mpaka 1990, na askari maalumu wa jeshi la ulinzi, vilivyo tengenezwa nchini islael, mwaka 1978, pia kuna arama za vidole bahadhi ya sehemu zao za miili, lakini hazija fnana na mtu yoyote ambae arama zake zimesha wai kupatikana, licha ya hivyo kuna alama za upigwa na vitu vizito, ambavyo vina mwoekano wa ngumi lakini uzito ambao umetumika ni wa nyundo ya chuma, iliyo sukumwa kwa uzito wa kilo mia moja” alimaliza yule Doctor wa polisi, report hii ya pili ndi iliyo mstua inspector Johnson David, kuliko ile ya kwanza, maana ile report, ili onyesha kuwa muuwaji wa wale vijana wabakaji, alikuwa ni zaidi ya hatari, ambae yeye alifahamu kuwa ni mwanamke toka shamba, ndie alie toka pale Mapambano guest and bar, eti ngumi yenye msukumo wa kilo mia moja, “naweza kwenda kuona miili ya hao marehemu?” aliuliza inspector Johnson David, “bila shaka afande, tuna weza kuongozana” alijibu Doctor, wakainuka na kwenda kwenye sehemu ya kuifazia miili ya marehemu, dakika chache baadae walikuwa wamesha fika eneo la mutual, ambalo lipo kwenye ya bara bara kuu mle ndani ya hospital, hapo shughuli zote zika sitishwa, wakimpisha inspector Johnson David, aikague miili ya marehemu, **** saa tano na nusu magari matatu yalikuwa yanaingia ndani ya hospital kuu ya taifa, yakiwa ni mawili madogo aina ya Range Rover, moja likiwa mbele moja kati kati ya coster lenye watu wengi sana ndani yake, liliuwepo nyuma, kati ya magari hayo matatu, yalienda moja kwa moja na kusimama kwenye maegesho ya pale mutual, kisha watuwengi wakaanza kushuka kwenye magari yale, wakati Jackline na waombolezaji wengine wakishuka toka kwenye basi dogo, mchungaji Kileo na walinzi wake walishuka toka kwenye Range Rover Jeusi, akaelekea mapokezi pale pale mutual, akiongozana na wazee wawili watu walio onyesha kuwa ni wazee wenye busara zao, wakaomba kuingia ndani kwaajili ya kuuona mwili wa mpendwa wao, laini wakaambiwa kuwa wasubiri kidogo, maana kuna inspector Johnson David ndani ya sehemu hiyo, akikamirisha mambo ya kikazi, mch Kileo akuwa na ujana akarudi kwa waumini wenzake, na kutulia akisubiri inspector atoke ili na yeye aingie akamwone Rafiki yake bwana Chilumba, huku mmoja kati ya wazee aliongozana nao mapokezi, akiwa tangazia waombolezaji kuwa, wasubiri kidogo polisi wamaize kazi zao wao pia wata ruhusiwa kuingia, pale alipo kuwa ame kaa bwana Kileo aliwaza mengi sana, juu ya kifo cha mchungaji mwenzie, “inamaana alikuwa ana ugomvi na watu flani” yalikuwa ni mawazo ya mchungaji Kileo, kabla aja banwa na mkojo, na kuwaomba walinzi wake wamsindikize kwenye choo cha jumuia kilichopo umbari wa mita miamoja toka pale walipo kuwepo, hapo walinzi wa mchungaji kileo, waliwai kwenye mlango wa choo na kuzuwia mtu yeyote hasiingie mle ndani, huku wakiwaondoa watu walio kuwepo mle ndani ya choo, baada ya kuingia ndani ya choo, mchungaji kileo alimkabidhi simu zake zote mbili, mlinzi wake mmoja, na kuingia kwenye choo kimoja, kati ya vingi vilivyomo mle ndani, ya jengo kubwa la vyoo, akiwaacha walinzi wawili nje wakiangalia usalama wake, huku nako Jackline akiwa amejitanda kanga zake vizuri kabisa aliwafata nyuma, mpaka alipo waona wakiingia chooni ndipo na yeye alipoongeza mwendo na kuingia choo cha kiume,***** baada ya kumalizana na matajiri wao wa kihindi, maeneo ya upanga karibu na ofisi za wizara ya ulinzi, Denis na Mahadhi wakaonelea watafute sehemu nzuri ya kupata chakula kidogo wachangamshe matumbo, “unajuwa toka asubuhi hatuja pata chochote” aliongea Mahadhi huku akiendesha gari taratibu, akifwata bara bara ya diamond jubilee, uelekeo wa muhimbili, “umeona hen, sema atuna haraka sanaaaaa! mimi nita gonga ata bia mbili ksha ukaniache ofisini” alisema Denis ambae alikwa anatamani sana bia, huku moyoni akipania kwenda kumweleza yule mwanamke alie mwacha nyumbani kuwa anampenda, ikiwezekana awe mke wake, jambo hilo alilifanya kuwa siri moyoni mwake, “ina maana leo atunywi pamoja?” aliuliza Mahadhi huku anakata kona, na kuifwata bara bara ya fire, “leo na wai home kidogo” aliongea Edgar, akionyesha kuto taka maswali zaidi, Mahadhi hakuoji lolote zaidi alikata kona upande wa kulia kuelekea tena muhimbili, kisha akasimamisha gari nje ya bar moja kubwa sana, ijulikanayo kama hoster, karibu kabisa na hoster za chuo cha madoctor wa muhimbili, ***** moja wale walinzi wa mchungaji Kileo, walishangaa kumwona mtu anaingia kule chooni, wakati wao walisha zuwia watu wasiingie kule chooni mpaka boss wao atakavyo maliza haja zake, kilicho washangaza zaidi ni kwamba mtu mwenyewe alikuwa ni mwanamke, tena kwenye vyoo vya kiume, walipo mtazama vizuri, ni yule mwanamke wa liemzuwia kusogea eneo alilosimama mchungaji Kileo, “we mwanamke ume tuchokoza tena?” aliongea mmoja wa wale walinzi, yule alie msukuma kule msibani, safali hii walimwona, alikuwa anawasogelea kwa mwendo wa haraka sana, huku akishika gauni lake na kulinyanyua kwa juu, na kuyahachia mapaja yake manene kuonekana, yule mlinzi aliepewa simu na mchungaji ashike, alimwona mlinzi mwenzie ambae ata kule msibani ndie alie msukuma huyu dada, akimfwata tena yule dada kwenda kumzuwia, huku akiwa ametanua mikono yake, na kuandaa ngumi kwa ajili ya kumtandika yule dada, ambae mda wote walizani kwamba, huyu mwanamke amepotea njia na kungia choo cha kiume, “leo utakuwa mfano kwa wajiga wenzako” alisikika yule mlinzi, ambae alimchukulia Jackline kuwa ni dhahifu, ilikuwa tofauti, wote walishangaa kumwona yule dada, bado alikuwa akija kwa speed ile ile, akiwa amekunja sura kwa hasira, lakini alizidi kuwa mzuri, muonekano wa mwanamke huyu uliwafanya walinzi awa watambue kuwa huyu dada safari hii, akuwa na utani atakidogo, na wala ajapotea mlango kama wa livyozani, alikusudia kuingia kule chooni, hapo yule mlinzi aliinua mkono wake na kurusha kofi kumwendea yule dada ambae ni Jackline Michael Nyati, yule mlinzi alishangaa mkono wake ukidakwa na kubanwa kwa nguvu ikifwatiwa na ngumi kali iliyochomoka kwa mkono wa kushoto wa Jackline, na kutuwa sawia kwenye mbavu changa za yule mlinzi, akifwatia sauti kama ya kuvunjika kwa kijiti kikavu, kisha ya kafwatia maumivu makari ya kuvunjika kwa mbavu zake akataka kupiga kelele za maumivu, lakini alipigwa ngumi ya shingo, iliyo tuwa kwenye koo lake, iliyomfanya ashindwe ata kuvuta pumzi kwa sekunde kadhaa, huku akiongezewa ngumi ya shavu na kujibwaga chini kama mzigo, kilikuwa ni kitendo cha haraka sana, kilicho tumia sekunde kama sita mpaka saba, yule mlinzi mwingine aliona tukio zima, la kushangaza, kwa mwanamke mrembo kama huyu, kupiga ngumi nzito za kijambazi kama hizi
Akaona bora akamsaidie mwenzie, ambae alikuwa amelala chini akijishika kooni kwake, lakini Jackline akusubiri mpaka yule mlinzi wa pili asogee kabisa, aliruka juu na kumtwisha kifuti cha kifuani, sambamba na kiwiko cha usoni, kilicho mchana pua yake, na kusababisha damu kutapakaa usoni kwa yule mlinzi wa pili, ambae alipepesuka huku akijishika puani, wakati akishangaa damu zake mwenyewe,alistuka akiongezewa ngumi tatu mfululizo za uzoni, zenye uzito mkubwa, kwa speed ya umeme, akimaliziwa na teke mzunguko la kichwani, lililo mrusha mpaka ukutani, na kujibamiza kisogo, kisha akatuwa chini kama furushi, hapo hapo yule mlinzi wapili akapoteza maisha, kisha Jackline akarudi alipolala yule mlinzi wa kwanza ambae bado alikuwa amelala chini, akishindwa kuinuka kutokana na mamivu ya kuvunika mbavu, huku amejishika kooni, akikaza misuri ya shingo akionekana kukosa pumzi, “unakumbuka nilikuambia nini pale msibani” aliuliza Jackline baada ya kuchuchumaa pale chini alipo lala yule jamaa “sa...sa..…” alikoroma yule mlinzi wa kwanza akijaribu kusema samahani, kwa sauti ambayo Jackline alijuwa kuwa, ingeweza kumfikia mchungaji Kileo kule ndani ya choo, hapo Jackline akachomoa kisu kwenye usawa wa paja leke, na kukididimiza shingoni kwenye koo la yule jamaa, ambae alipoteza maisha pale pale, kule chooni mchungaji Kileo alishasikia vishindo vya vurugu, nje ya choo, akajuwa kuwa walinzi wake wanazuwia watu kuingia mle chooni, lakini wakati anajiandaa kutoka, akiwa ameshamaliza kujisaidia akasikia sauti ya kike ikiongea kwa kunong’ona, huku mlinzi wake moja akikoroma, akahisi kuna tatizo, lakini alipo kuwa ameisikia ile sauti yakike, akaona kuwa hakuna tatizo yaweza kuwa ni binti mmoja amepotea choo, maana tokea alipo gunduwa kuwa muuwaji wa mchungaji mwenzie alitumia silaha aina ya Magnum Sniper Rifle, yeye na wenzie walitilia mashaka uwepo wa Michael Fransis Nyati, askari ambae walimpiga risasi wakiwa mission za kivita huko nchini Congo, nasiyo mwanamke kama alivyo sikia nje ya choo, mchungaji kileo akafungua mlango na kutoka nje, cha kwanza kuona ni mwili wa yule mlinzi alie mpatia simu, akiwa amelala chini, damu zimemtapakaa usoni na kisogoni, mlinzi wa pili na yeye kama mwenzake alikuwa amelala chini damu zimetapakaa, hukuzinyine zikiendelea kutokaa kwenye jelaha shingoni kwake, wakati anashamngaa tukio lile, mchungaji akagundua kuwa mle ndani ayupo, peke yake, kuna mwanamke, tena alishakuwa amemsogelea karibu kabisa na kisu mkononi, tena bado kikiwa kinavuja damu, kitendo bila kuchelewa, mch Kileo alirusha ngumi ya maana, kumpiga yule dada, ambae aiikwepa kwa kusogea pembeni kidogo, na kufanya ile ngumi ya mchungaji, ipite hewani kama anafukuza nzi na kugonga ukutani, karibu na nguzo ya mlango, lakini Kileo akusikilizia maumivu, akarusha mateke matatu mfurulizo, yote ya kapita pahewa, yule dada aliyakwepa, Kileo akaona kuwa akifanya mchezo ya tamkuta yaliyo wakuta walinzi wake, muda mchache uliopita, akaona wacha ajikumbushe umaili wake wa kipindi yupo jeshini, “ mzee Kileo, leo auna ujanja” ilikuwa sauti tamu ya Jackline ambae muda huu alikuwa ameachia tabasamu baya sana, na kufanya ashindwe kujulikana kama anacheka au amekasirika, “unataka nini kwangu we! mwanamke” aliuliza Kileo huku akionyesha kuzidiwa na uoga, baada ya mashambulizi yake kushindwa kufanya kazi, “umesaau mlicho kifanya mwaka 1988 misitu ya Kanaluchina nchini Congo” aliuliza Jackline kwa sauti ya chini “lakini alikuwa ni major Masinde, sisi wengine unatuonea tu!” aliongea Kileo akijiandaa kuchomoa bastora kwenye mfuko wa ndani wakoti lake la suit, kitendo kilicho onekana wazi machoni kwa Jackline, Kileo alimshuhudia yule mwanamke akiwa hewani ametanguliza magoti yote mawili kisu mkononi, alishindwa kumkwepa, magoti yakatuwa kifuani kwake, ikifwatiwa na kisu kuzama shingoni kwake, mchungaji akaanguka chini kama gunia lililo tupwa toka begani kwa kuli, Jackline akifwatia juu yake, magoti ameyatanguliza kifuani kwa mchungaji, jackline alichomoa kisu shingoni kwa mzee Kileo, akimwacha mchungaji akiwa katika atua za kukata roho, Jackline aliendea sink la kunawia mikono, akaafungua bomba la maji taratibu, kama yupo nyumbani kwake, kisha akanawa vizuri ili iwe rahisi kwake kupita nje bila kustukiwa na mtu yoyote, **** Nje nako inspector Johnson David baada ya kumaliza uchunguzi wake, akatoka na kukutana na kundi kubwa la waombolezaji, waliokuwa wakimsubiri amalize uchunguzi wake, na wao wakamwone mpendwa wao, inspector Johnson David alikuwa ameshajulishwa uwepo wa watu awa nje, kilichomvutia ni uwepo wa rafiki mkubwa wa marehemu, ambae ni mchungaji Kileo, licha ya kuwa maarufu samna sana mzee huyu pia anamfahamu toka siku nyingi sana, akaambiwa mch Kileo yupo chooni, akaona aitakuwa vibaya akamsubiri, maana ukiachilia kufahamiana kwao, pia ange weza kuoji mambo mawili matatu, yatakayo msaidia wenye uchunguzi wake, inspector Johnson David alisimama pamoja na waombolezaji, macho yake kule kilipo choo alichoingia mchungaji Kileo, ulipita mda mrefu pasipo kumwona mchungaji akitoka chooni, wala kuona mtu mwingine akielekea huko, maana ilisemekana walinzi walizuwia watu wasiingie kule chooni, tofauti ni kwamba walionekana wakina mama pekee wakienda na kurudi toka chooni, inspector Johnson David na askari wake wakiwa na kundi la waombolezaji walisubiri sana pale nje, pasipo kumwona mchungaji, akitoka, ilisha pita nusu saa toka inspector Johnson David, akae pale nje pamoja na waombolezaji, “kwani aliingia saa ngapi huko chooni?” aliuliza inspector Johnson David, macho akiyaelekeza chooni, wakati huo akamwona mtu mmoja anaelekea kule chooni, kwenye vyoo vya kiume, akumjari akamgeukia yule mtoa matangazo, akiashiria anataka jibu “nikama nusu saa hivi, imepita” alijibu yule mtowa matangazo, wakati wanaendelea kuulizana juu ya kuchelewa kwa mchungaji Kileo kutoka chooni, mala wakasikia kelele toka upande wa chooni, zikifwatiwa na yule jamaa alieingia muda mfupi uliopita, kule chooni, akitokea chooni huku akikimbia, “mauwaji!.... jamani..mauwaji ..kuna watu wame kufa chooni” aliongea yule mtu mwanamume, akiwa amejawa na kiwewe cha hali ya juu, hapo kengere ya hatari ikagonga kichwani kwa inspector Johnson David, akatowa amri kwa askari kulizunguka eneo zima la hospital pasipo kuruhusu mtu kutoka, na wengine kuziwia watu kutoka na kuingia chooni, huku yeye na wazee wachache pamoja na yule askari wake mwenye cheo cha Sgt, wakielekea chooni, walipoingia chooni walikuta wale vijana wawili walinzi wa kileo, wakiwa wamesha kata roho, lakini mchungaji kileo likuwa bado ameshikilia shingoni, damu ziki churuzika kwa wingi huku akitapatapa, “mnyanyueni tumwaishe ndani, anaweza kupona bado mzima huyu” alisema inspector Johnson David, kitendo cha haraka sana, walimnyanyua juu juu mchungaji Kileo, wakiongozwa na inspector Johnson David, wakaanza kuelekea ndani kwenye chumba cha emergence, lakini wakiwa njiani wamembeba mchungaji kileo, inspector Johnson David aliona kama mchungaji Kileo alikuwa anataka kusema neno flani, lakini akashinda kutokana na maumivu aliyo ya pata kooni, pamoja na mwili wake kuzidi kuishiwa nguvu, kuli sekunde, inspector Johnson David akazidi kusogeza sikio lake karibu na Kileo, pengine ange ambulia chochote, huku safari inaendelea “nya.. nya.. nya.. nyathiii” ndilo neno pekee aliloweza kutamka kileo, lika sikika masikioni kwa inspector Johnson David baada ya hapo Kileo akatupa mikono huku na huko, kisha akatulia kabisa, atawalipo mfikisha ndani, tayari alikuwa amesha fariki, inspector Johnson David aliuma meno kwa uchungu, na kupiga ngumi ukutani kwa hasira, maana licha ya kuwa mch Kileo alikuwa ni mtu anae mfahamu sana, lakini pia alikuwa mtu muhimu, katika uchunguzi ule ukizingatia ndie alie onana na muuwaji uso kwa uso, inspector Johnson David, akakumbuka kitu, hapo hapo akapiga simu kituo kikuu, kuomba msaada wa askari ishirini kwa ajiri ya kuzunguka eneo la hospital, hii kubwa ya muhimbili, ili waweze kumkamata mwuaji, ambae aliamini kuwa bado alikuwepo eneo lile, wkati huo askar polisi walio kuwepo walikuwa wametawanyika mle ndani ya eneo la hospital wakizuwia mageti ypte ya kuingilia na kutokea, hakna kuingia hakuna kutoka, **** kumbe baada ya kumaliza kazi yake, Jackline alinawa vizuri na kutoka nje pasipo kuwa na arama yoyote ya damu, wala sura ya mbuzi kama ilivyokuwa mle ndani, wakati akiwashugulikia wakina Kileo, akapita upande wapili wa jengo akiwa kwepa waombolezaji wenzake, na kutokea kwenye chuo cha sayansi na tiba, kisha akajipenyeza kwenye majengo ya chuo adi kwenye hostel za chuo, akaona uchochoro mwingine mbele yake, alipo uchungulia akagundua mbele ya uchochoro ule kuna bar, hivyo akaenda na kutokea kwenye choo cha bar hiyo, hapo akaingia chooni na kijifanya kama mteja aliepo pale bar, alizuga kwa sekunde chache kule chooni, kabla ya kutoka na kuelekea upande wa bar, ile Bar ilikuwa na watu wengi kiasi, wakipata soup na wengine wakipata vinywaji mbalimbali, ila wachache wakinywa pombe, Jackline akiwa anapita kati kati ya ile bar, alikuwa makini sana, huku akiangalia kama kuna mtu anaye mtilia mashaka, aka waona vijana wawili pembeni kidogo ya ukimbi wa bar, mmoja amegeukia upande wake na mwingine amemgeuzia mgongo, wakiwa wame kaa meza moja kule pembeni ya ukumbi wa bar, mezani kwao kulikuwa kuna chupa ya maji na chupa mbili za bia, moja ikiwa imesha kwisha, na nyigine ina bia nusu, kilichomvutia kwenye ile meza, ni nguo aliyoivaa yule kijana ambae alikuwa amemgeuzia mgongo, ilikuwa ina fanana na aliyo vaa mwenyeji wake Denis asubuhi, na sasa alimwona yule kijana alievaa nguo kama ya mwenyeji wake mlevi, ambae amesha mjuwa jina anaitwa Denis, akiinua chupa ya bia na kuiweka mdomoni, anaigugumia kisha anaiweka chini ikiwa robo, wakati anaendelea kumwangalia yule kijana vizuri akagongana macho na yule aliegeuikia upande wake, akamtambua kuwa ni yule aliekuwa na Denis jana yake, pale Mazao building, wakati Denis akimtafuta yeye, Jackline akageuza shingo mbele, ili yule kijana aliekuwa na Denis, asije akamkalili, muda wote alikuwa akitembea kulifwata geti la kutokea nje ya bar, alipo jaribu kuangalia tena ile meza, sasa alimwona vizuri Denis, wakiwa wamesimama na yule mwenzie huku Denis akigugumia chupa ya bia, na yule mwenzie akijaribu kumwonye kitu kule upande alipo yeye Jackline, akuna mwingine aliye onyeshwa ni yeye Jackline, hapo moyo wa Jackline ukalipuka kwa hofu, akijuwa kuwa mwenyejiwake anaweza kumwona, na endapo Denis akimwona lazima amuuwe, maana lazima ataambatanisha matukio, Jackline akageuka tena kuangalia mbele na kuongeza mwendo, akawai kutoka nje ya geti, akiwa na uwakika kuwa Denis ajamwona, Pale nje alishuhudia magari manne ya polisi, yaliyo beba askari wengi, ya kiwa katika mwendo wa kasi sana, huku ya kipiga ving’ora ya kielekea hospital, Jackline akatabasamu huku anaelekea kituo kidogo cha daladala, na kujichanganya na Abiria wanao subiri magari yaendayo sehemu mbalimbali, japo aliyakuta magari mawili ya endayo mbezi, lakini alitulia kwanza kuona kama wale vijana wawili watatoka, na kama wakitoka je watamfwatilia?, akiwa pale kituoni aliweza kuwaona Denis na rafki yake wakitoka bar na kuanza kuangalia huku na huku, kisha wakaingia kwenye gari Toyota IST nakuondoka zao, wakaingia barabarani, wakielekea upande alipo yeye ilikuikamata barabara ya fire, Jackline akusubiri tena akaingia kwenye gari lililo andikwa mbezi muhimbili, akatafuta seat na kukaa, akiliona gari la kina Denis likipotelea upande wa fire **** Nikweli Mahadhi alimwona Jackline, lakini akuwa akimfahamu, alimwambia Denis amwangalie yule mwanamke, jinsi alivyo na umbo na sura nzuri, lakini Denis alikuwa busy na chupa yake ya bia, ata alipo geuka na kumtazama akuweza kumwona, adi walipo gutushwa na ving’ora vya polisi, muda huo walikuwa wamesha pata soup na kupumzika kidogo pale bar, huku Denis akinywa bia mbili akidai na towa lock, baada ya kusikia ving’ora vya polisi, walisimama na kutoka nje, baada ya kuangalia kama wangemwona yule dada, ambae Mahadhi ana msifia kuwa mzuri sana,lakini awakumwona, walipo mkosa wakaamua kuingia kwenye gari na kuondoka zao, wakiikamata barabara ya fire, kisha morogoro road kuelekea upande wa magomeni,**** inspector Johnson David alikuwa anawapanga askari walio ongezeka kutoka kituo kikuu, wakati huo alikuwa akijaribu kulipambanua lile neno, alilo kuwa akijaribu kulitamka chungaji Kileo, waandishi wa habari walisha anza kusogea eneo la tukio wakapewa utaratibu wakuingia, pale hospital, msako mkari uliendelea ndani ya eneo lote la hospital, “nyathi, anamaanisha nini?” alijikuta akiongea kwa sauti kidogo, kiasi cha yule askari wake mwenye cheo cha SGT aliye simama pembeni yake akasikia, “vipi afande, umeongea na mimi?” aliuliza yule, SGT, inspector Johnson David akamsimulia yale maneno ya mwisho ya mchungaji Kileo, kisha wakajadiriana mambo machache, inspector Johnson David, alikuwa anafahamu kuwa, awa marehemu wawili, kabla ya kuwa wachungaji walikuwa wanajeshi wajeshi la ulinzi, na kitengo chao kiliusika na nakazi za siri, ndani na nje ya nchi, na walikuwa wadunguwaji, pia ni muuwaji katka kitengi hicho cha siri, ambao walikuwa ni wataalamu wa kutumia silaha ya kudungua toka mbali, na ndiyo silaha iliyotumika kumuuwa mchungaji Chilumba, baada ya hapo walipata jibu, waende kikosi kikuu cha mission za siri, ambacho wakina Kileo walikuwepo wakifanyia kazi, kabla ya kuhacha jeshi, kutokana na muda kuwa umekwenda sana, la zima wausika wanao kusudia kuwaona ofisini, watakuwa wamesha ondoka, wakapanga waende kesho mapema, hivyo inspector Johnson David akatoaa maagizo kwa doctor mchunguzi, akisema kuwa kesho atapitia pale kupata majibu ya vipimo vya kileo na walinzi wake, maana masaa yalisha tembea sana pasipo kumpata muusika wa mauwaji, zaidi ya kukamata watu waliokuja kutazama wagonjwa wao na kutibiwa, *** Ilisha timia saa mbili usiku, akiwa ame valia gauni lake refu ndani kikaptula cha jinsi chenye zana za kazi, Jackline alikuwa amesha maliza kupika na kuwasiliana na baba yake, na kumpa report ya kazi aliyo mtuma, japo alisha pitiliza malengo, na kumuuwa kabisa mchungaji Kileo, sasa Jackline alikuwa amejilaza kwenye kochi kubwa akitazama tv, ambayo ilikuwa na onyesha taharifa ya habari, na tukio lililo onyeshwa muda mrefu, ni la mauwaji ya mchungaji kileo, ikiwa ni mauwaji mfurulizo ya wachungaji wawii, ambao ni marafiki, chakula kikiwa mezani karibu na kochi dogo la mtu mmoja, licha ya kuwepo na sebule ya chakula, lakini Jackline aliamua kuweka hapo, kwa ajiri ya mwenyeji wake, sababu alijuwa lazima angekaa kwenye makochi na siyo kwenye viti vya ukumbi wa chakula, wakati anaendelea kutaazama TV, mala akasikia sauti ya muungurumo wa gari, nje ya nyumba, moja kwa moja akajuwa ni mwenyeji wake mlevi, baada ya dakika chache alimwona Denis akiingia ndani, huku akiburuza begi kubwa, kwa mkono mmoja, huku mkono mwingine amebeba mifuko mitatu, midogo meusi, inayonukia nyamaza kuku na chips, akiyumba yumba kwa kuzidiwa na pombe, mwanzo Jackline alizani kuwa Denis alikuja na mgeni, kengere ya tahadhari ikagonga kichwani kwake, sababu akutaka mtu mwingine aongezeke mle ndani, ingekuwa ni hatari kwake, kwani ange bainika mapema sana, akabaki amemtazama huyu kijana mlevi, akimwona akiingia peke yake ndani na kuweka beg chini, kisha akamkabidhi Jackline vile vimifuko vya chips na kuku, “ume..umeee..shindaje hapa nyumbani?” alisalimia Denis kwa sauti ya kilevi huku anakaa kwenye kochi tofauti na lile la chakula, Jackline akacheka kimya kimya, akimtazama mwenyeji wake jinsi alivyolewa “salama kabisa, umeniacha peke yangu, yani leo umechelewa sana kurudi” aliongea Jackline akijifanya kudeka, kumzuga mwenyeji wake, huku akifungua vile vimfuko alivyo kuja navyo Denis, akakuta kuna vyakula, akashangaa akamtazama mwenyeji wake, kwa mtazamo wa pekee, huyu kijana mlevi, kuwa anaonekana kumjari sana, Jack akaenda mbari zaidi na kuwaza labda anamtega ili ampende, “mh! kaka kwa nini umenibebea chakula” aliuliza Jackline akimtazama Denis, ambae sasa alikuwa akilegeza tai shingoni kwake “kwani .. wewe.. ni robot? Siiiiiii..... nimekuuuu ..bebea ili ule” aliongea Denis kwa sauti ya kilevi, akimalizia kuitoa tai shingoni, “si ulihacha ela ya chakula, mimi nimesha kupikia chakula hiki hapa” aliongea Jackline akiwa anasogeza chakula alicho kiandaa kwa ajiri ya mwenyeji wake, Denis ana stuka na kumwangalia Jackline usoni, macho yao yana gongana, nikama Denis amekumbuka kitu “hoooo! Kweri nimekumbukaaaaa..” jinsi alivyo mtazama na maneno aliyoongea ya limstua Jackline akamkazia macho Denis, “umekumbuka nini kaka yangu” aliongea Jackline akimsogelea Denis karibu, mkono wake wa kulia akiwa ameshika gauni, na kuanza kulipandisha juu taratibu, mpaka usawa wapaja, bado kumalizia kidogo afikie kwenye zana za kazi (kisu), macho ya Denis yalituwa kwenye paja la Jackline, likamchanganya, “duu! Ndiyo maana mimi naamini kabisa yani, daah! hujuwe ukiambiwa kwa haraka haraka uwezi kuamini wala kusadiki” aliongea Denis kwa sauti ya kilevi akijaribu kukwepesha macho yake, ya sitazame paja la mgeni wake, ambalo aliamini kuwa ameinua ile nguo kwa bahati mbaya, huku mapigo ya moyo ya Jackline ya kizidisha speed, alikuwa bado amesimama karibu ya mwenyeji wake mkono bado nchi chache kukamata kisu na kumwaga damu, “mbona sikuelewi kaka kunanini?” aliuliza Jackline, akizuwia asionekane kama yupo kwenye hali gani, “Mahadhi aliniambia lakini sikuamini, daah! sasa nimeamini” alitulia kidogo Denis akavuta pumzi kidogo ile ya kilevi levi, huku akifunua chakula, hapo Jackline alikumbuka kuwa wakwanza kumwona pale bar, alikuwa ni rafiki yake ambae atajana walikuwa pamoja, akahisi ndie mahadhi, hapo akaona akuna namna tena, zaidi ya kupoteza roho ya mwenye jiwake. kisha atafute sehemu ya kwenda kuishi,
“kweli.... kabisaaaaaaa ...ni ...nimeamini, mkiwa wawili... ndani yaaaa... yaaaaa, ya nyumba, yani ata maisha...... yanakuwa safi sanaaaaaaaa, mimi nilijuwa niiiiiii maneno yake ya kizinzi tu! kumbe yana ukweli ndani yake” aliongea Denis kwa sauti ya kilevi, hapo Jackline alishusha pumzi kwa nguvu, kama mtu alie kuwa amebeba mzigo mzito, “yani .. yani leo nimekuta.. chakula kizuriii..alafu…ala.. ahhhh” alibabaika Denis, huku macho yake yakiwa yameganda kwenye paja zuri, lilo jaa vizuri la Jackline mgeni wake, hapo Jackline akagunduwa kuwa bado alikuwa amepandisha gauni lake, akaliachia haraka, “ho! Samahani.. siku.. siku kusudia kuangalia” aliongea Denis kwa sauti yake ya kilevi huku akigeuza kichwa chake na kutazama mezani, Jackline akamtazama Denis, kisha akatabasamu, kidogo huku moyoni akijisemea “una bahati, ungekuwa umesha chinjwa” aliwaza hayo akimwangalia Denis, ambae alikuwa akifunua hot pot la chakula, akamwoana mwenyeji wake, Denis anataka kuchota chakula kwenye hot pot, iliaweke kwenye sahani, anasita kidogo “henheee!, nimekumbuka chukua funguo nenda kwenye gari nimesaau mzigo wangu.... pale kwenye seat ya pembeni kwa dereva” aliongea Denis kwa msisitizo wa kilevi, huku akimpatia Jackline funguo za gari, Jackline alizipokea funguo kisha akatoka nje, huko nje aliwaza sana juu ya tukio alilotaka kulifanya dakika chache zilizopita, ni tukio la kutaka kumchinja mwenyeji wake, tukio zima lilipita kichwani kwake adi tukio la Denis kushangaa paja lake, hapo aliinua gauni lake nakuangalia paja lake, kisha akacheka kidogo, “inabidi niwe makini na huyu mlevi, maana naweza kumchinja bila sababu” Jackline aliwaza hayo, huku akifungua mlango wa gari upande wa seat ya abiria, akakutana na carton ya bia za kopo, na soda nne za kopo kwenye mfuko, akaduwaa akatikisa kichwa kama anasikitika, huku tabasamu likichanua mdomoni kwake, “baba anakunywa pombe, lakini huyu kazidi, zile za jana bado zipo leo kabeba nyingine” alijisemaea Jackline huku akichukua lile carton la bia na soda, na kufunga mlango wa gari, kisha akarudi ndani, “hivi kaka unaitwa nani alafu kwanini unakaa peke yako?” aliuliza Jackline kwa sauti tamu sana, huku akifunga mlango kwa ufunguo, akizuga kuwa amjuwi jina yule kijana mlevi mwenyeji wake, lakini akujibiwa kitu, zaidi alisikia sauti ya mkoromo, akageuka kumtazama mwenyeji wake, alikuwa ameegemea kochi amesha lala, Jackline akatabasamu kidogo, akitikisa kichwa kwa masikitiko, akasogea kwenye meza na kuziweka bia mezani, na soda akaziweka kwenye friji, akamtazama tena mwenyeji wake alikuwa amesha lala kabisa, chakula mezani kikiwa wazi, akija guswa kabisa “mgeni siku yapili, analala sebuleni” alijisemea Jackline, kisha akazima Tv na taa za ndani alafu akajilaza kwenye kochi kubwa, alichelewa sana kupata usingizi, akiwaza hili na lile, kuhusu watu wanne waliobakia kuuwawa, pia aliwaza atakuwa amewauwa watu wangapi mpaka atakapo maliza kuwauwa wausika wanne waliobakia, maana mpaka sasa amesha uwa watu wenginekumi, tofauti na wausika walio kusudiwa, Jackline aliwaza sana mpaka akapitiwa na usingizi, ilisha timia saa tano na nusu za usiku, **** Usiku saa tano, ikiwa inaelekea saa sita kasoro, ndani ya nyumba moja kubwa ya kifahari mitaa ya kinyelezi mwisho, walionekana wazee wanne wakiwa katika mjadara mkubwa sana, “sikiliza Alex ninacho kueleza niukweli huyu siyo mwingine ni private Michael Nyati” aliongea lieutenant (luteni) Kaijage, akimwambia capten Alex Mwasaga, ambaye akuamini kabisa kuwa Michael atakuwa bado mzima, wazee awa wau wazima, ni major Dvid Johson Masinde, na wenzake, wakina capten Alex mwasaga, luten James Kaijage, na sajint taji Mathayo GK, “jamani mimi naona tujadiriane, tumpate adui wa kweli, maana tukisema tumfikirie mtu ambae tumeshuhudia akipigwa risasi na kuporomoka, kwenye makorongo, tutakuwa tuna poteza muda” aliongea kwa msisitizo capten Alex, “mh! Alex umesaau kitu kuhusu swala la risasi, kumbuka kuwa wote tulikuwa tumevaa body amour (bullet proof), alafu risasi yenyewe ilikuwa ya bastora” alikumbusha major David Masinde, na wote wakatulia na kuvuta kumbukumbu, kisha wakaanza kukubari ukweli huo wa major Masinde, kwa kutikisa kichwa juu chini, kasolo Alex yeye akuamini kabisa, kwamba Michael Nyati atakuwa hai, “lakini kama ni yeye, kwanini alikaa kimya mda mrefu, leo hii imepita miaka ishilini na kitu, ndiyo aanze kututafuta?” Alex kiukweli bado alikuwa haamini kabisa, kama kweli vifo vya wakina Chilumba na Kileo, vinausiana na tukio walilo lifanya mwaka 1988 huko nchini congo, “labda Alex umesaau kuwa private Michael Nyati, ni mtu ambae anatumia akili nyingi sana kwenye mambo yake” aliwakumbusha ssgt Mathayo, akiwasimulia baadhi ya matukio na mipango aliyowai kuisuka Michael, akiwa askari mdogo, wa cheo na umri, na kuwaokoa kwenye matukio mbari mbari ya hatari, na kutoa mipango iliyo wasaidia wafanikishe mission, “jamani mimi naona tuwe makini kuanzia sasa, tujuwe kabisa kuwa tunawindwa, na pengine tukaitwa na kuhojiwa na polisi au vyombo vya habari, kwa hiyo tuwe makini na majibu yetu, maana endapo tutakubari kuwa muuwaji ni Michael, lazima tutaje sababu ya yeye kufanya hivyo, kwa hiyo hapo swala ni kukataa tu, kwamba atujuwi lolote, zaidi ya kwamba Michael alitoweka tukiwa mission (missing in action) Congo, huku tukiendelea kujilinda sisi wenyewe” aliongea major Masinde, akionyesha umakini mkubwa sana na kikao kilifungwa, wote wakatawanyika, alibakia Major Masinde ambae alikuwa mwenyeji wao, walichagua hapo kwa major Masinde, kwa sababu, kwanza nyumba ilikuwa sehemu ambayo aina msongamano wa nyumba, hivyo maongezi yao ya singe sikilizwa na mtu yoyote wa jirani, pili wenzake wangeweza kufika kwa ulahisi kutokana na kuwa, wawili kati yao wanakaa mbezi na kimara, mmoja alikuwa ana kaa mbezi beach, hivyo wangetumia barabara ya malamba mawili, la mwisho kabisa, mke wa major Masinde alikuwa amesafiri kwenda kwao musoma, kusalimia ndugu, na watoto wa masinde wote ni wakubwa wanamaisha yao, hivyo pale nyumbani alibaki yeye mwenyewe **** Asubuhi na mapema siku ya pili, ilikuwa ijumaa, kama ilivyokuwa jana yake, Jackline alikuwa amejilaza kwenye kochi akijifanya amelala, aliweza kumshuhudia mwenyeji wake akijiandaa kwenda kazini, leo alivalia shati la blue na tai nyekundu, ya kipepeo na suruali nyeusi na viatu vyeusi, “mh! huyu kaka ni mlevi, lakini anajipenda sana” aliwaza Jackline, huku amejifanya kulala, ikwa ni mala ya kwanza katika maisha yake, Jackline kuona kuwa mwanaume kapendeza, akuwai kuona mwanaume anavaa alafu akaona eti! amevaa vizuri, alichukia sana wanaume, pasipo sababu ya wazi, zaidi ya kuambiwa na baba yake awachukie wanaume, akiwa amejilaza juu ya kochi Jackline alimwona mwenyeji wake, ambae siku ya pili leo anamlaza sebuleni, sababu ya ulevi, akiingia chumbani, baada ya dakika chache akatoka akiwa amebeba shuka jingine, siyo lile la jana, Jackline alimwona mwenyeji wake akija moja kwa moja mpaka alipo lala, akamfunika vyema kabisa, kisha huyo, cha pombe akaelekea kwenye friji akafungua na kuchukua kopo moja la soda ya baridi aina ya cola, akalifungua na kuligugumia mpaka alipo maliza, akachukua jingine, kisha akafunga mlango wafriji, akaenda mezani akachukua makopo mawili ya bia, kisha atowa fedha mfukoni mwake kiasi cha elfu selathin, na kuziweka mezani akika ndamizia na kopo moja labia kati ya yale yaliyopo mezani kisha huyo, akaelekea nje, Jackline akasikia muungurumo wa gari, likiwashwa na baada ya dakika chache likaondoka, na kutokomea, Jackline baada ya kuakikisha gari limesha ondoka akanyanyuka toka juu ya kochi, akavua gauni lake na kubaki na kikaptula cha jinsi na tishert akaanza kwa kufanya mazoezi, ni kwaida yake siku zote za maisha yake, **** Asubui ya leo ilimkuta insp Johnson David akiwa mwenye mwazo mengi sana, nahii yote nikutokana na mauwaji yanayo endelea kutokea mfurulizo, usiku kucha alikuwa akiwaza juu ya kesi hii nzito, ambayo amekabidhiwa yeye, kati ya mambo aliyo ya waza, ni neno alilo tamka marehemu Kileo, “nyathi” alikuwa anamaanisha nini, “nitapata jibu nikienda kuwaona watu wa MSM, (Military Secret Mission),” alijisemea Johnson akiinuka toka kitandani na kumwacha mke wake na mwanae mdogo, wakiendelea kuuchapa usingizi, akaanza kujiandaa kwa ajiri ya kwenda kazini, ***** Saa moja na robo, Denis ndio alikuwa anaingia kazini, akaegesha gari lake kwenye maegesho mbele ya Mazao Building, kabla ajashuka akakamata kopo la bia, akalifungua na kulimiminia mdomoni kama mtu mwenye kiu kali ya maji, alifanya hvyo kwa kurudia rudia, mpaka alipo maliza, kisha aka iliweka lile kopo pamoja na makopo mengine tupu ya bia na soda mle ndani ya gari, akatulia kidogo ndani ya gari akijisonya sonya kila mala, alijilaumu sana kwa kushindwa kuongea na mgeni wake, kumweleza kwa anampenda “leo lazima nitaongea naye, lakini mbona jana kama niliongea nae kidogo, ata sikumbuki niliongea naye nini, haaa! niujinga, kwani na yeye mwenyewe ajuwi…. ” mawazo ya Denis yalikatishwa ghafla, baada ya kufunguliwa kwa mlango wa gari lake, upande wa abiria, “kaka vipi na kuona umefika alafu umeganda kwenye gari” alikuwa Mahadhi, ambaye alisimama nje ya gari akishindwa kuingia ndani ya gari kutokana na makopo matupu ya bia na soda kujaa pale chini ya siti ya abiria, akacheka kidogo, kisha akaenda kwenye gari lake na kuchukua mfuko wa Rambo, na kuyaweka yale makopo, kisha wakatoka na kuongozana, kuelekea ndani ya jengo wakiyaacha yale makopo kwenye dust bin, “Denis, leo ni melikologa mbaya” aliongea Mahadhi wakati wana pandisha ngazi, kuelekea ofisini kwao, “nini tena mwanangu” aliuliza Denis wakati wanapandisha ngazi kuelekea ofisini kwao, wakasimama kidogo na Mahadhi kuanza kusimulia “ndugu yangu jana si nime litoba, baada yakutoka hapa, nika pita buguruni, yule demu wangu wa chama alinistua, ni kakaa pale mpaka saa saba usiku, ndio nikaenda home, nikamkuta wife kavimba, nikajaribu kujichekesha wapi, nika mdanganya kuwa niliku sindikiza wewe nyumbani, sababu ulizidisha pombe ukazima, hapo kidogo akaelwa, lakini amepanga kukupigia simu akuulize” alimaliza Mahadhi kusimulia, “pumbavu, ngoja apige usikie nitavyo kukataa, ukuwa na sababu nyingine, zaidi ya kuni taja mimi kuwa mlevi?” aliongea Denis akianza kupandisha ngazi, akionyesha kuto kupendezwa na kitendo kile, “sikia Denis, mimi na wewe tuta malizana pale Jambo, nakurusha na carton moja la bia” alisema Mahadhi huku akiendelea kuongea “nikitoka hapo naenda kumnunulia wife mdori wenye maandishi mazuriiiii, lazima atulie” ilo neno lamwisho likamvutia Denis, “umesema mdori inamana shemeji anapenda midori?” aliuliza Denis kwa shahuku “tena na mauwa pembeni, hapo umemaliza, ata kama alinunaje, atapoa tu!” aliongea Mahadhi kibabe, Denis akatabasamu, **** Magari mawili ya polisi, ya likuwa ya mesimama nje ya jengo moja kubwa la ghorofa mbili, ndani ya kambi moja kubwa la Jeshi, akashuka insp Johnson, akapokelewa na askari mmoja wajeshi la ulinzi mwenye cheo cha kopro, na kumuongoza mpaka kwa kwa mkuu wakitengo cha mission za siri jeshini, baada tu ya kuingia ndani ya ofisi hile, Insp Johnson akapiga saruti kwa mkuu wakitengo hicho, mwenye cheo cha brigedie, na kwenye shati lake kifuani upande wakulia, alikuwa amevaa kidari cha jina kimeandikwa Rodrick DM, “karibu insp… nani vilie” aliongea yule Brig akimpa mkono Insp Johnson, “Johnson David” aliongea insp Johnson David akimtajia jina yule mkubwa wajeshi, “ndiyo bwana Johnson, karibu sana, nilipo julishwa ujio wako nikaona bora nikusubiri, vinginevyo usinge nikuta, ninge kuwa nimesha ingia kwenye kikao” alisema yule mkubwa, huku anajiweka sawa kwenye kiti chake, “afande nimekuja kukuona, juu ya awa askari wastaafu walio uwawa mfurulizo, kama labda kuna lolote mnalo lijuwa ambalo linaweza kutusaidia kumpata muuwaji, au chanzo cha mauwaji” aliongea Insp Johnson kwa nidhamu ya hali ya juu iliyo mvutia yule mkubwa wajeshi, “bwana insp ilo swala ata sisi linatuhumiza vichwa sana, maana ata silaha ina yotumika ni ya kijeshi, lakini atuja pata kumjuwa muuwaji ni nani, na sababu ya kufanya hivyo ni nini” aliongea yule mkubwa akionyesha masikitiko, “kwani silaha hizo zipo jeshi zima?” aliuliza insp Jonhson, “mh! hapana zaidi ya ikuru na hapa kwetu, akuna sehemu nyingine zilipo hizi silaha” alijibu yule kamanda akijitaidi kuvuta kumbukumbu, “kwani afande kuna upotevu wa silaha ulishawai kutokea wa silaha kama hiyo,” aliuliza insp Johnson, “ilo ndilo swala ambalo nilikuwa najaribu kukumbuka,” Brigedia Rodrick akamsimulia Insp Erenest kuwa silaha ya aina hiyo ya Magnum Sniper Rifle ilipotea mwaka 1988 nchini Congo ikiwa mokononi mwa Private Michael Nyati, ambae toka kipindi hichi mkuu wa kitengo akiwa brigedia Suod, ambae amestaafu miaka mitatu baada ya tukio hilo, private Michael akuwai kuonekana tena, na Jeshi lina amini alipoteza maisha, insp Johnson alisikiliza kwa umakini sana story ya brigedia Rodrick, huku akiandika kwenye note book yake, insp Johnson akasikia jina la Nyati, aka jumlisha na Nyathiii, akatowa damu mdomoni na maumivu makali ya mchungaji Kileo, akapata “Nyati” akajikuta akiongea mwenyewe huku brigadia Rodrick akimsikia, “vipi ulishawai kupata habari zake huyu mtu” aliuliza brig Rod, “samahani afande, nilijaribu kuunganisha uwezekano wa huyu Nyati, kuusika na mauwaji ya wenzake, labda uelewano wao ulikuwaje kabla ya kupotezana huko porini” aliongea insp Johnson David, “sidhani kama kuauwezekano wa kutambua maelewano yao kwa ipindi hicho, maana ata mimi nilikuwa askari mdogo sana,” alijibu Rodrick, “labda kuna kumbukumbu zozote za watu walio shiriki hiyo operation ya mwaka 1988,” hapo brg Rodrick aliwaza kidogo kisha aka sema, “sidhani kama hiyo kumbukumbu itakuwepo, maana kuna kipindi tuli pokuwa tunaamishia nyraka kwenye computer toka kwenye mafire ya kawaida, nyalaka nyingi zilipotea, ila kwa kukusaidia, chukua alama za vidole za Michael Nyati, tutakupatia toka kwenye file lake la uajili, kisha nenda kwenye matokeo yako ya vipimo vya hao marehemu, uangalie kama vinaendana, ukipata jibu tujulishe na sisi,” aliongea Brg Rod huku akitoa namba zake za simu na kumpatia insp Johnson, kisha akamwita yule kopro, akamweleza ampatie insp Johnson finger print za Michael Nyati, zilizopo kwenye file lake, kisha yule Brg akaondoka zake, walipo baki wawili yule Kopro alimwelezea insp Johnson David juu ya usumbufu uliotokea kwa siku zile mbili, za mauwaji ya askari wale wa staafu, kitu ambacho wanashindwa kuamini nikwamba kwa umri ambao sasa atakuwa nao Michael, kama bado yupo hai ni miaka hamsini kasoro, na mauwaji ya jana yamethibitisha kuwa huyu muuwaji ni kijana mwenye nguvu sana, na siyo mzee, sababu amepambana na wanaume watatu, “ila kama unataka maelezo zaidi mtafute brg mstaafu Soud, yeye alifanya kazi na kikundi hicho kwa ukaribu sana,” alimaliza yule kopro akimpatia nakala ya alama za vidole vya Michael na akamwelekeza maeneo anayokaa mzee Suod, huko kigamboni mji mwema, Insp Johnson akaingia kwenye gari lake pamoja na askari wake, wakaondoka zao na kunyoosha muhimbili, kucheki alama za vidole vya muuwaji, afananishe na za Michael Nyati,**** Jackline alikuwa amesha maliza shuguli zake zote, ikiwa na kuongea na baba yake, ambae alimsisitiza kusitisha mauaji mpaka polisi wajisahau, huku mzee Nyati akiendelea kutafuta habari za wabaya wake wengine, pia Jackline alikuwa amesha maliza kunywa chai na viazi mviringo, na sasa alikuwa ametulia juu ya kochi akiangalia Tv, na soda aina cola, ni moja kati ya soda za mwenyeji wake mlevi zilizopo kwenye friji, ikiwa mkononi, alikuwa amevalia kikaptula kifupi cha jinsi na tishert nyeupe, nguo nyingine pamoja na za mwenyeji wake alikuwa amezifua kwa kutumia mashine ya kufuria, kasoro gauni lake moja lefu chakavu aliyoiweka kwa zarula, muda wote Jackline alikuwa akikumbuka jana jioni, alipo taka kumtowa roho mwenyeji wake, akajikuta anatabasamu, wakati akiendelea kukumbuka matukio hayo, akakumbuka kuwa mwenyeji wake alikuja na beg jana usiku, akanyanyuka na kulifwata chumbani, maana alisha lipeleka huko, sasa alisha kizowea chumba hicho, maana ata kuoga aliogea huko, na nguo alibadirishia huko, nikutokana na mwenyeji wake kuto mwonyesha chumba cha wageni, akalibeba lile begi, na kuja nalo sebuleni, akaliweka juu ya meza, na kulifungua, alichokiona ndani ya begi hilo alijikuta akipatwa na hasira kilicho amatana na kicheko kwa wakati mmoja, zilikuwa ni nguo na viatu vya kike, akatoa kigauni kimoja chepesi “mh! kizuri sana” alinong’ona Jackline, huku anajipimisha kile kigauni, kikamtosha vizuri sana kikiishia kwenye mapaja, “ni chakulalia, sijuwi anamwanamke wake?” alijisemea Jack, kitu kama wivu kili mtaka kumwingia huku akianza kutoa kitu kimoja baada ya kikingine, licha ya kuwa na nguo nzuri za kila aina, lakini Jackline kwake yeye suluwali ndilo vazi analolipenda zaidi, na mle ndani ya begi zilikuwapo mbili za jinsi, zilizobana “nzuri sana, kumbe ana mwanamke huyu” alijisemea Jackline huku akijipimisha, nazo zilimkaa vizuri, “mbona kama ameninunulia mimi” pia magauni na viatu vizuri, per tatu lakini kilicho mfanya atabasamu na kushindwa kumwelewa huyu mlevi, ni nguo za ndani, yani chupi saba za aina mbari mbari, na rangi tofauti, zikiwepo za kawaida na bikini, aina ya chupi ambazo akuwai kuzitumia, katika maisha yake, pia kulikuwepo na tight saba za rangi tifauti, “huyu ananitania ngoja arudi atanitambua” alijisemea Jackline na kuvirudisha vile vitu ndani ya begi, kisha akalifunga na kulipeleka chumbani.
ITAENDELEA...
Tags
Your Thoughts