DADA MDUNGUAJI EPISODE 14

DADA MDUNGUAJI


EPISODE 14


STORY NA Mbogo Edgar


ILIPOISHIA EPISODE 13 :  akimwonyesha kidole mama Jackline, aliyekuwa ana muweka Jackline vizuri, wakati huo Jackline alikuwa ameshaitoboa ile drip, nakuanza kuinywa, kiukweli yalikuwa ni maji flani yaliyo andaliwa kwaajili ya kumpa nguvu, baada ya kumeza ule unga mweusi, mama Jackline alistuka kidogo baada ya kumwona yule doctor akimtazama kwa tahadhari, wakati huo Jackline aliwatazama kwa macho ya kuibia, huku akijifanya kuwa, bado amezidiwa, endelea ..........

 Huku wote wawili, yani Jackline, na mama yake, lengo lao likiwa moja kwenye ile bastora, iliyokuwa chini ya kitanda, kwenye mchago, “hoooo! doctor Magreth, habari za saa hizi” alisema yule doctor, ambae alionekana kisoma jina kwenye ki name tag, alicho kivaa mama Jack shingoni, “safi doctor karibuni” aliongea mama Jackline, yani mke wamzee Nyati, huku akimwacha Jackline, na kuwatazama doctor na yule polisi, “samahani doctor, nime mruhusu huyu kamanda, aingie kwa muda huu, maana anaitaji kujuwa kinacho endela, juu ya mgonjwa wao” alisema yule doctor wa kiume alie valia koti kama yeye, “nisawa doctor, wacha mimi nirudi ward ya wazazi, maana nili wasaidia kumpokea huyu mgonjwa, ila huyu kamanda, asikae sana humu ndani, siunajuwakuwa huyu ni mginjwa wakike, japo mwalifu lakini anastahili haki zote za kijinsia” alisema mama Jack, “ndio maana nilishangaa, kukuona hapa, kumbe hupo maternity?” aliongea yule doctor wakiume, huku akimsogelea Jackline pale kitandani, “ugua pole mgonjwa, nazani hapa utapata hewa nzuri sana, maana tuna madilisha mazuri na makubwa” alisema mama Jackline, kisha akatoka nje ya chumba hicho, akimwacha doctor, yule aki mkagua Jackline kwenye macho, huku akionyesha wazi kustaajabu uzuri wa binti huyu, ambao nitofqauti na habari aliyo wai kuisikia mala kwamala, “awa madoctor wa wazazi wana uwezo mkubwa wakufikili, kutokana na kesi ya mgonjwa huyu, yani hii drip aliyo mpatia ita msaidia sana, tena kwa njia ya kunywa inaoneka inampa nguvu kwa haraka sana” alisema doctor yule, huku akimwacha Jacline na kuchukuwa sindano kwenye kabati, aka mchoma kwenye mshipa wa mkono, kisha akanyonya kihasi flani cha damu, alafu akaichomoa ile sindano, ikiwa imejaa damu kiasi flani, “kamanda, wacha kwanza tupate vipimo zaidi, alafu tuta kujulisha kinacho endelea, unaweza kusubiri hapo nje” alisema Doctor yule huku akimtazama Jackline, kwa macho ya kuto kuamini, kama kweli huyu mwanamke anemtazama, ndie yule mwanamke alie tikisa jiji na nchi kwa ujumla, tena kipindi cha nyuma, aliwai kuuwa doctor mmoja bingwa wa kina mama, hapa hapa muhimbili, ni doctor Joseph Ndilane, wakati huo aliingia yule nesi wakike, aliye tumwa drip, na Anitha, au mama Jackline, mke wa mzee Nyati, “ok! nesi wacha kwanza atumie hili drip analokunywa, mpaka majibu yake yakija, kaa hapa mtazame, mimi naenda mahabara” alisema yule doctor, na yule kamanda wa polisi, akaongeza neno, “usimwogope huyu, awezi kufungua hiyo minyololo, napia nje kuna polisi wengi sana, kama ulivyo ona” wote wakacheka, lakini yule nesi alionekana wazi kujawa na uoga, “hali yake ikibadirika nijulishe mala moja” alisema yule doctor, huku akitoka na yule kamanda wa polisi, wakimwacha nesi akiwa amesimama akitetemeka, akageuza kichwa chake na kumtazama Jackline aliekuwa ameikamatia drip, kwamikono yake, iliyo fungwa na pingu zilizo unganishwa na minyololo iliyo kuja mpaka miguuni, nesi akamwona Jackline Nyati akimaliza kuinywa ile drip, na kisha akalidondosha lile fuko la maji ya drip, kisha akamwona akijikuna kichwani, kwenye nywele zake, hapo Nesi akamwona Jackline nikama anatoa kibanio kidogo kwenye nwelezake, huku akimtazama yule nesi na usoni mwake ameachia tabasamu mwanana, kabisa ungeambiwa huyu dada ni muuwaji wakutisha, usinge kubari, “au wame msingizia dada wawawt” aliwaza yule nesi, huku anaenda kuliokota lile fuko la drip, na kwenda kuli weka kwenye chombo cha takataka, kilichopo mle ndani ya kile chumba **** “ok! kazi yako nime imaliza, sasa unawaza nini?” alisema mama Jackline baada ya kuingia ndani ya gari la mume wake na kuvua koti la kidoctor, “bado zamu yangu kuingia ndani, nataka nikaongee na Masinde” alisema mzee Nyati kwa sauti tulivu kabisa, “mh! kwanini tusi shuudie kwanza Jackline akitoka, ndiyo uanze huo mpango wako mpya” alishauri mama Jack, “tatizo wewe kuna kitu ukijuwi, muda mfupi ujao polisi wote wataamia mtaani kumsaka Jackline, wakati huo macho na hakili yote itakuwa mtaani na hapa patakuwa sehemu tulivu kabisa, ambapo mfanya usafi ataingia wardini kufanya usafi, akitumia lift na ngazi, akiwa nan doo ya kufanyia usafi, hapo vipi?” alimaliza mzee Nyati na kumfanya mke wake acheke kivivu, “we mzee balaha, yani sikuwezi kabisa” **** wakati huo Insp alikuwa ndiyo anaingia kituo kikuu cha polisi, kilicho mshangaza ni kwamba, tofauti na alivyo dhania kuwa, atakuta shamla shamla za waandishi wa habari na viongozi mbali mbali, wakija kumtazama muuwaji wakike, insp alikuta kituo kikiwa kimya kabisa kama akuna kilicho tokea, insp akakimbilia ofisini kwa mkuu wa idara ya upelelezi, ambae alimsimulia juu ya kilicho tokea kwa Jackline, kuanguka ghafla akiwa amezidwa na homa, yani kitu kinacho zaniwa kuwa ni malelia, pia alielezwa juu ya CGP alivyo chukizwa kwa kitendo cha yeye kwenda hospital, akiacha kikao pale kituo kikuu, wakati kazi yake imekwisha, mwisho akaambwa asubiri mpaka Jackline atakapo pata na fuu, ili waanze vikao mbali mbali, leo hii, hivyo insp akatoka zake na kuelekea ofisini kwake ambako, alipata nafasi ya kuandika report, ya upeleleezi mzima mpaka kumkamata Jackline, insp alianza kuifanya kazi yake, huku anawaza juu ya homa ya ghafla ya mwanamke huyu hatari, nandipo alipo kumbuka kuwa, jana usiku awakuzipata silaha, zilizo tumiwa na muuwaji huyu wakike, akarudi kwa Chief CID, nakuomba kibari cha kwenda kufanya ukaguzi kwenye nyumba ile, akaruhusiwa kufanya hivyo, kwa shariti la kurudi haraka sana pale ofisi, mala akimaliza kazi hiyo, na Johnson akaondoka na askari wapatao kumi na tano na magari mawili polisi, kuelekea huko, **** ilisha timia saa sita mchana,  Denis akiwa ametulia kwenye bar moja iliyopo kona ya kwanza ya muhimbili, akinywa pombe yake taratibu huku France akipata supu ya kuku akisukumia soda, yake orange, “kwanini huyu mwanamke ananifanyia hivi jamani” aliwaza Denis, ambae aliutambua upendo wakweli wa mke wake, juu yake, “kwanini sasa alikubari kukamtwa, sasa mimi nitaishi nanani?” aliwaza Denis kiasi cha kutamani kulia kabisa, lakini akakumbuka kitu kimoja ambacho ambacho kilimfanya cheke kidogo, “nilikuwa na mwona lofa, hivi siku moja tunge gombana ingekuwaje?” aliwaza Denis akiachia kicheko kidogo, mala simu ya Jackline iliyo kuwa mfukoni mwake ikaita, akaitazama, alikuwa baba ndie mpigaji, akaipokea nakuiweka sikioni, “ndiyo mzee” alisema Denis, “sikia kijana, we! nenda nyumbani kwako, ukatulie hapo subiri simu kutoka kwangu, asijuwe mtu yoyote kama tunawasiliana” ilisikika sauti ya mzee Nyati upande wapili wasimu, hapo Denis akamalizia bia yake, akamnawisha mwanae, kisha huyooo! akaingia kwenye gari nakuondoka zake, akiwa na mwanae Fransis, ****** mzee Nyati alikata simu, wakati huo huo Jackline, alikuwa akiingia kwenye gari, seat ya nyuma, akiwa amevalia mavazi ya mhuguzi wakike, “nasikia mzee Masinde bado mzima” iliuwandiyo kauri ya kwanza, ya  Jackline baada ya kuingia kwenye gari, “doctor wako nimesema wewe pumzika kwanza, kazi hiyo ataifanya mganga mkuu na mimi, hapo baadae” alisema mama Jack, aliekaa seat ya dereva, huku akimwonyeshea mzee Nyati, wote wakacheka, wakati huo huo mama Jack aliwasha gari na kuliondoa taratibu sana, kuelekea geti la kutokea, ***** majibu ya vipimo vya Jackline yalikuwa tayari, akakabidhiwa yule doctor wa kiume alie shughulikia swala lile, akayasoma kwa umakini sana, yakamshangaza, aka kimbilia kwenye chumba cha mgonjwa yule, ambae vipimo vilionyesha akuwa na tatizo lolote, alipo karibia mlango wa chumba alimo lazwa mgonjwa, akawaona askari wakiwa makini sana wanaendelea na ulinzi, na yule afisa kiongozi alie onekana ndie mwenye jukumu la uasimamia swala lile la usalama na ulinzi, alipo mwona doctor anakuja, nae akamfwata, “ndiyo doctor, vipimo vinasemaje?” aliuliza kwa shahuku yule, afisa wa polisi, lakini doctor alioneka kuwa katika hali ya sinto fahamu, “ebu twende ndani, hapa vipimo vinaonyesha positive positive” aliongea doctor akitembea haraka haraka, kuelekea kwenye chumba alicho lazwa Jackline, wakaingia ndani na kutazama kitandani, wote wakaduwaa, maana walimwona yule muuguzi wakike alie kuwa na Jackline mle ndani, akiwa amelala kitandani, ame valishwa nguo zile za Jackline, yani suluali nyeusi na tishet nyeusi, amefungwa ile minyororo na pingu alizokuwa amefungwa Jackline mwanzo, akionganishwa na kitanda, kiasi cha kusindwa kufurukuta, huku akifungwa kitambaa cheupe usawa wa mdomo wake, yule polisi aka msogelea haraka, na kuktoa kile kitambaa mdomoni, “imekuwaje we! mwanamke” aliuliza yule polisi, kwa hamaki ya hali ya juu, “ata mimi sielewei, nilimwona kwanza kitoa kitu kishwani mwake, nikajuwa ni kibanio, lakini baadae kiamwona akini kamata kwanguvu, huku anatoa bunduki chini ya godoro” alieleza yule mwanamke, huku anatetemeka, “baada ya hapo, alifanyaje?” aliuliza yule afisa ambae alionekana kuchanganyikiwa, “akaniambia nikipiga kelele ata nifyetua akaniambia ni vue nguo zangu na yeye akavua zakwake, alafu na mimi akaniambia nivae za kwake, alafu aka nifunga hii minyororo, hapa kitandani, alafu akaniziba mdomo, na yeye akapitia hapo dirishani” alieza yule nesi, huku akionyesha dirisha pana lililo zibwa kwa vioo pasipo nondo, ambalo kwa sasa lilikuwa wazi kabisa, hapo yule afisa wa polisi alitokambio mbio nje ya chumba kile, “Jackline ametoroka, samba nje tumasake haraka sana” alipayuka yule afisa kama alie pagawa, na askari wakaanza kusambaa ovyo, pasipo kujuwa wanae msaka kwa sasa amevaaje, na ametoka saangapi?” 



  Wakwanza kufika nyumbani kwa Denis, alikuwa ni insp Johnson, na askari wake, ambao waliwakuta wakina Mahadhi, boss na Janeth, wakiwa nje ya nyumba ya Denis, wameegesha gari lao, wakimsubiri mwenzao, licha yakujaribu kupiga simu yake, lakini akuwa anapokea simu yake, wakajuwa kuwa mwenzao amechanganyikiwa na tatizo ambalo lime mtokea, kiukweli walisha sikia taalifa ya kukamatwa kwa mke wake, aki tajwa kuwa Jackline Michael Nyati, ndie Jambazi la kike lililo kuwa lina uwa kila kukicha, taalifa hiyo iliwastua sana, maana ni miezi michace hiliyopita waliliona garila Denis kwenye eneo la tukio kule jengo la wajasiliamali, akini kilicho washangaza nikwamba, jinsi mama Frank alovyo mpole mzuri na mstaalabu kwao, tena mnyenyekevu, pia historia yake na Denis wana ifahamu, na ndicho kitu pekee kinachowa shangaza, maana Denis alimkuta Jackline au mama France, akiwa anauza mama ntilie, wakiwa wanaendela kujadiriana, namana ya kumsaidia mwenzao kukabiriana na swala hili, na waliamini kuwa mwenzao alikuwa anashukuru kugunduwa kuwa alikuwa anakaa na muuwaji, wakiwa wamebeba kato za bia kwaajili ya kumliwaza mwenzao, mala walistuka kidogo baada ya kuyaona magari mawili ya polisi, yakiingia pale nyumbani kwa rafiki yao, lakini awakuogopa sana wakiwa na uakika siyo wao tu, ata rafiki yao Denis, akuwa anajuwa lolote juu ya mauwaji aliyo yafanya mke wake, ambae pengine ikitokea bahati mbaya akaachiwa, basi Denis asinge weza kuishi nae, kwani ata wao wasinge subutu kumkaribia yule mwanamke, “naitwa insp Johnson, wa kituo kikuu cha polisi, mnaweza kujitambulisha nyie ninani na mnafwata nini hapa?” aliongea insp Johnson baada tu! yakushuka toka kwenye gari, huku polisi wengine wakishuka haraka, sana na kuizunguka nyumba hile, “mimi ni bwana James, ni boss wa bwana Denis, kwenye kampuni yetu ya usanifu wa majengo, huyu karani wangu anaitwa Janeth, na huyu ni Mahadhi, ambae ni sawa na bwana Denis, ni wataalamu wangu, wa michoro ya majengo” aliongea boss wao wakina Mahadhi, “na hapa mmefwata nini?” aliuliza Johnson, “tokea tulipo pata taalifa ya kulicho mtokea mwenzetu, tukajaribu kupiga simu lakini apokei, hivyo tumekuja hapa kumtazama, na tunamsubri mpaka arudi” alifafanua boss James, “ok! kwahiyo huyu bwana hayupo?” aliuliza insp, huku akisikia simu yake inaita, “hayupo tumesikia ametoka mapema” alionge boss, lakini wakati huo Johnson akumsikiliza tena, sababu tayari simu yake, ilionyesha kumstua baada ya kuliona jina la mpigaji, akaipokea ile simu haraka, nakuanza kuongea pasipo kusikika upande wa pili, “ndiyo afande ..... ndiyo nipo kibamba.... kuna lolote mkuu ......mama yangu nini?..... hapanaaaa! hapana! sitakik kuamini, hapanaaaaaaa!” alipayuka insp kwa sauti ya ukari na yajuu sana, huku ana rudi kwenye gari lake mbio mbio, “twende muhimbili  haraka” aliongea insp, kwa sauti ambayo ilikuwa ikikaribia kuangua kilio, hapo askari wakarukia kwenye magari, yaliyo kuwa yanaondoka, eneo lile, na kuwaacha wakina Mahadhi, wakishangaa, kinacho tokea, wakati huo huo wakaliona Toyota Noah, linalo milikiwa na Denis, likiingia pale nyumbani, “karibuni jamani, mbona amkuni julisha ujio wenu?” aliuliza Denis, mala tu! baada ya kushuka toka kwenye gari, akimwacha France ndani yagari, “tungekujulisha endapo unge pokea simu” alisema boss James, hapo Denis akakumbuka kuwa, leo akusikia ata mala moja simu yake ikiita, aka jipapasa mifukoni lakini wapi, akuona simu yake, zaidi ni simu ya mke wake pekee, ndiyo aliyo kuwa nayo, akarudi kwenye gari ambako bado France alikuwa ndani yake, akapekuwa kwenye mikebe yote ya kwenye dash board, lakini apakuwa na simu yake, akavuta kumbukumbu, “hoooo! nitakuwa niliiacha asubuhi” aliwaza Denis huku ana mchukuwa mwanae France toka kwenye gari, na kuelekea mlangoni, akafungua na kuwakaribisha wageni wake ndani, ambao walishusha katoni za bia toka kwenye gari lao “pole sana kwa matatizo bwana Denis” alisema boss James, wakiwa wamesha tulia sebuleni na kuanza kushambulia pombe, wakidai wana mliwaza mwenzao, “kwakweli siwezi kupoa mpaka nijuwe mwisho wa mke wangu,” hapo boss James na Mhadhi wakatazama, wakati huo Janeth, alikuwa jikoni na na Fransis, akipika chakula kwaajili ya mchana na jioni, France akiendelea kuchezea vigari vyake, pembeni ya Jen,  huku wakati mwingine akienda kumtazama baba yake kule sebuleni, “yani bado una mwita mke?, hivi akiachiwa utaweza kuishi nae kwa amani?” aliuliza Mahadhi kwa sauti ya mshangao, huku akimtazama Denis, “Mahadhi, Jackline akuwa mbaya kwangu, akuwa mbaya kwako wala kwa mtu mwingine, labda umesahau kuwa nyoka akuumi mpaka umkanyage mkia” alisema Denis, kwasauti tulivu na taratibu, iliyo jawa na uchungu mkubwa sana, Mahadhi na boss wakatazamana Denis, kwamacho ya mshangao, kisha wakamtazama Denis, “inamaana umeongea na Jackline baada ya kukamatwa?” aliuliza boss James, Denis akakataa kwa kutikisa kichwa, “wamenizuwia kabisa” alisema Denis, alafu nikama  kunakitu Denis akakumbuka “ila kuna magari ya polisi mawili, nimepishana nayo hapo kwenye kona, walifwata nini?” aliuliza Denis, na Mahadhi akasimulia ilivyokuwa, “lakini nashangaa mkubwa wao amepikiwa simu, na aliondoka ghafla huku amechanganyikiwa, sijuwi kuna nini huko?” “tena walisema wanaelekea muhimbili” alidakia boss James, “labda yule mgonjwa alie shambuliwa jana, atakuwa amesha kufa” alisema Denis, wakatti huo vinywaji vikiendelea kunyweka, **** ndani ya ofisi ya kituo kikuu, makamanda wanadhimu wajeshi la polisi walikuwa ndani ya ofisi ya CGP, wakijadiri juu ya swala la kutoweka kwa mwanamke yule hatari, ambae nchi nzima wanajuwa kukamatwa kwake, “naagiza askari wote wa hapa dar es salaam, waingie kwenye operation hii ya kumsaka huyu, mwanamke” alisema CGP, kwasauti kari, iliyo onyesha kuwa ni amri inayo itaji ukelezaji wa haraka sana, “ndiyo afande, naomba ni nianze utekelezaji” aliongea mkuu wa idara ya Fild Force, “endelea na kazi, ila mshilikishe insp Johnson, anafahamu ujanja mwingi wa huyu mwanamke” alisema CGP, kisha Chief FF, akapiga saruti na kutoka nje ya ofisi ile, wakati huo CGP likuwa ana mgeukia msaidizi wake, “akikisha magari yote ya vituo vyote vya hapa dar, yanapata mafuta, kisha amri kwa Chief of Treaning, and Op’s, akikisha askari wote wa vituo vyote akuna ane baki nyumbani, kuanzia sasa, mpaka mwanamke huyu apatikane, isipo kuwa insp Johnson na kikundi chake, wao watafanya kazi kivyao” zilikuwa ni amri kubwasana za kuvita, toka kwa CGP, kwa ufupi mambo yalikuwa ni mtafaruku, ndani ya ofisi ile, wanadhimu walitawanyika na kwenda kutekeleza majukumu yao, ***** saa nane insp Johnson alikuwa pale hospital akichukuwa maelezo toka kwa doctor na nesi walio kuwa wakimhudumia mgonjwa Jackline Nyati, kati ya maelezo yaliyo msaidia kuanza kupata mwanga wa tukio hili, ni maelezo ya nesi, alie tekwa na Jackline, ni baada ya kusema kuwa, Jackline alichukuwa bastora chini ya godoro la kitanda alilo lalia Jackline Nyati, “doctor hiyo bastora iliingiaje humu ndani ya ward?” aliuliza insp akimtazama yule doctor wa kiume, ambae alikuwa amekaa karibu kabisa na nesi, wakati huo yule afisa mwenye cheo kikubwa kuliko insp Johnson, alikuwepo tokea mwanzo, alikuwa amesimama pembeni, akitokwa jasho mpaka kwenye meno, maana kupotea kwa Jackline, ilikuwa ni janga la taifa, “kwakweli afande mimi sijuwi, sababu humu ndani niliingia na huyu afande, labda ange ulizwa doctor Magreth, ambae alimpokea mgonjwa na kuanza kumhudumia” hapo ikaagizwa, akaitwe huyo doctor Magreth wa kitengo cha wazazi, lakini ilitumia lisaa lizima kumtafuta doctor huyo, ambae licha ya kutazama kwenye orodha ya madoctor wote wa kitengo cha wazazi awa kumpata doctor mwenye jina hilo, ikaagizwa itazamwe orodha ya madoctor wote wa hospital hiyo ya rufaha, ikitumia saa lingine lizima, mpaka saa kumi jioni, awaku mpata huyo doctor Magreth, ikaagizwa waitwe madoctor na wauguzi wote wenye majina kama hayo, ilikuwa tanbua, kutokana na ukubwa wa jengo hili na uwingi wawatu humu ndani, ili waghalimu lisaa nanusu kuwakusanya wakina magreth wote waliokuwepo huku wakicuuwa na majina ya madoctor waliotoka zamu siku ile,  walipatikana wauguzi na madoctor ishilini tu!, wenye majina ya Magreth, lakini kati yao akuonekana yule doctor alie mpokea mgonjwa, alieletwa na polisi, ambae ni Jackline Michael Nyati, mpaka hapo insp akajikuta anatabasamu, “Nyati yupo mzigoni” aliongea insp Johnson, huku akiinuka na kupiga saruti, kwa mkubwa wake aliekuwepo mle ndani, “afande wacha niende juu nika mtazame mgonjwa, kisha niingie mzigoni,” alisema insp na kutoka mle ndani ya ofisi aliyo itumia kufanya mahojiano, aka pandisha ngazi kwa mbio kwenda kumtazama baba yake, wenye ward ya pekee, aliyo kuwa amelazwa, akiwapita wakina koplo Mashiba na walinzi wake tisa, kwenye kolido, “mashiba kuweni makini, nazani mmesikia kilichotokea hapo chini” alisema insp akisisitiza ulinzi kwa mzee Masinde, ambae walizni wale toka jeshi la polisi awakujuwa kuwa ni baba wa insp, **** mida hiyo, Denis, na wakina Mahadhi walikuwa, wamesha pata chakula na sasa walikuwa wanaendelea kulewa, huku Janeth nae akiwa tayari amesha jiunganao, wakiendelea kunywa pombe, France yeye akiendelea kucheza, kama akuna kilicho tokea, wakati wote wa kupombeka, denis alikuwa ana lalamika juu ya mke wake, “ungekuwepo mke wangu tungekuwa tunakunywa mvinyo” alisema Denis, kwasauti iliyo kuwa imekolea kilevi, “ila unajuwa mimi nahisi nipo ndotoni, sababu siamini kama shemeji, ndie yule mwanamke tuliekuwa tuna msikia” huyo alikuwa Mahadhi ambae pia alikuwa ameanza kukolea kinywaji, **** gholofa ya tatu ya jengo kubwa la wagonjwa wa dharula, kwenye korido moja safu ya vyumba vya ward za VIP,  walionekana askari kumi wakiwa wame tanda na silaha zao, huku wamevalia mavazi mahalumu ya kuzuwia risasi, mala mlango wa chuba alicho lazwa mzee Masinde ulifunguliwa, akatoka insp Johnson na doctor mmoja, ambae aliteuliwa kumtibu mzee huyu, “doctor naomba ieleweke, akuna mtu mwingine kuingia humu, zaidi ya huyo nesi na mfanya usafi, na watakaguliwa kabla ya kuingia ndani” alisema insp kwa msisitizo, huku wale askari wakisikia, “kwa upande wetu akuna tatizo, labda waambie askari wako wawe makini, maana kilichotokea hapo chini kimetushangaza sana” alisema doctor huku wakishuka chini, kwakutumia ngazi maana mala zote lifti utumiwa na wazee, au wagonjwa maututi, pia kwa wafanyakazi wenye mizigo mikubwa, insp alipofika chini aliagana na doctor, kisha akaingia kwenye gari, pamoja na askari wake kumi natano, walio ingia kwenye magari yote mawili, kisha safari ikaanza, “inamaana Jackline akuwa anaumwaa, au kunakitu aliingia nacho mahabusu?” aliwaza insp huku redio call ya insp iki sikika kiita, “hallow Siera Bravo, ujumbe toka kwa Charle charle Delta, over” hapo insp akajuwa kuwa mwito ule unamhusu, akachukuwa redio ya kwenye gari na kujibu, “Charle Charle tuma over,” hapo maongezi yaka endelea, “Siera Bravo, taja loc (location, uelekeo) yako” ilisema sauti ya kwenye redio call, “Charle, loc yangu ni mhumbili, kaliakoo dubble kilo over”(KK yani Kituo Kikuu) alisikika insp huku wakati huo magari mawili ya polisi, yalikuwa anatoka nje ya geti kubwa la hospital ya muhimbili, ‘siera bravo jitaidi kutoa taarifa kila atuwa unayo piga over” iliskka sauti toka kwenye redio, “imenakiliwa over” mita miambili toka kwenye gati la hospital ya muhimbili, ndani ya Toyota V8, lililo kuwa lime egshwa muda mrefu sana maali hapo, toka saa tano asubuhi, likuwa limepandishwa vioo mpaka juu, na kuachwa nafasi kidogo ya hewa, Familia ya mzee Nyati, ya baba mama na mtoto, wao wapekee, wakiwa ndani ya gari hilo, waliweza kushuhudia magari mengi mengi ya yapolisi yakiingia na kutoka pale hospital, na sasa walishuhudia magari mawili yaliyo sheheni polisi wenye silaha za kivit yani SMG, na mavaazi ya kuzuwia risasi, huku akionekana insp Johnson kwenye gari lililo tangulia, wote wakacheka kidogo, kisha mzee Nyati akaonekana kuwaza jambo, “hivi Jack kwa mfano wewe ungekuwa ndie insp, ungefanya nini, kumkata Jackline Nyati, baada ya kutoroka?” hapo Jackline akatumia dakika sekunde chache sana kufikili, kisha akajibu, “ninge washikilia watu muhimu wa Jackline, nazani angeitaji maongezi hapo ninge futa ushaidi, kwa risasi nyingi sana” alisema Jackline, kisha Jackline na mama yake wakaheka kidogo, kabla ya kusitisha kicheko chao kwa ghafla, alafu wakatazamana, “baba lete simu, lete simu niongee na Denis” aliongea Jackline kwa pupa, akianza kumsachi baba yake simu, “sububiri wewe, Tanzania nzima inajuwa bado hupo chini ya polisi, alafu unataka kuongea na chapombe, siatawaleta mpaka ulipo” aliongea mzee Nyati, huku anachukuwa simu yake toka mfukoni na kuipiga, akiweka loud spikeer huku anatazama pad yake, iliyo onyesha kuwa Denis yupo Nyumbani kwake kibamba, “ndiyo. ndiyo mzee... mh! ndiyo mzee, za mida hii” wote ndani yagari walisikia sauti ya Denis iliyo zidiwa na kilevi, akionyesha kutoka sehemu yenye kelele na kwenda kwenye utulivu kidogo, “umesha toka kwenye kelele?” aliuliza mzee Nyati, akijizuwia kucheka, kutokana na Denis, kuonekana kujitaidi kuongea kwa ukakamavu, ili ulevi usionekane, kwenye  sauti yake, “ndiyo... mhhhh! siiii nipo nyumbani hapa” aliongea Denis akijitaidi asioekane amelewa, hapo mzee Nyati akaiziba simu kwa kiganja cha mkono, ile sehemu ya kuongelea, kisha akawmtazama mke wake, “mkwe amelewa,” alisema mzee Nyati huku akijizuwia kucheka, kiukweli Jackline alionyesha kuchanganyikiwa, lakini kabla ajaongea lolote,baba yake akaendela na maongezi, “Denis sikia kuwa karibu na simu, utapigiwa sasa hivi na mama yake Jackline, atakacho kuambia usimwambie mtu yoyote, itakutia matatizoni ikigundulika unawasiliana na sisi, sawa?” alisema mzee Nyati kwa sauti nzito na tulivu “sawa sawa, aina tatizo, mi nipo na France” alijibu Denis, kisha mzee Nyati akata simu, “amaelewa sana awezi kuendesha gari, na leo atakunywa pombe nyingi sana, maana siyo jambo dogo, unaambiwa mkeo kipenzi, tena mrembo kama mwanangu Jack, ati ni kajambaazi” aliongea mzee Nyati, na wote wakacheka, **** insp Johnson baada ya kufika kituo kikuu, akaagiza aitwe mtu wa zamu aliekuwa mapokezi toka asubuhi, akaja askari mmpja wa kike, constable, baada ya kufika pale, akamkumbuka kuwa ata yeye alipofika asubuhi alimkuta yule yule, “WP nazani unakumbukumbu nzuri ya watu walioingia humu ndani kuwaona mahabusu, ebu niambie mtu aliekuja kumwona Jackline Nyati yupoje” aliuliza insp kwa sauti ya ukari na kitisho, “ni kijana tu alikuwa na mtoto, alisema ni mume wake” alisema yule polisi wakike, huku akionyesha kutetemeka kidogo, maana ilisakata lilikuwa zito, “alitumia muda gani kuongea na mkewake?” aliuliza insp, akiwa anaandika kwenye kijitabu chake, “alitumia muda mwingi zaidi ya masaa mawili, aliondoka wakati yule mwanamke anachukuliwa kupelekwa kwenye ukumbi wamikutano” alieleza WP, nahapo Johnson akapata mwanga flani, akakurupuka haraka sana, na kukimbilia nje, “haraka sana kwenye magari, shenzi tungekuwa tumelijuwa swala hili mapema, pale pale tulipo pisha nae tunge mkamata” alisema insp huku wakiondoka kueleka Kibamba njia panda ya shule, **** jiji la dar es salaam likuwa limezizima, polisi walitapakaa kila kona ya jiji la hili, wakimsaka Jackline Nyati, alietoroka Hospital, japo ilipangwa kuwa ni kazi ya siri, lakini taalifa zilianza kusambaa taratibu, zikianzia hospital ya muhimbili, na kwa polisi wenyewe, na kuwafikia wananchi, kumbuka mdau mpaka sasa, akukuwa na chombo chochote cha habari kilicho onyesha sura ya mwanamke huyo hatari, zaidi ya watu kulijuwa jina lake, kuwa ni Jackline Michael Nyati, huku idadi kubwa ya polisi hao walimsaka mtu wasie mjuwa ata kwasura, saa kumi na mbili ikiwa inaelekea saa moja, brig gen msaafu Soud Hassan, alikuwa ameganda kwenye Tv yake toka asubuhi, akisubiri kuona binti wa mzee Nyati akionyeshwa, kukamatwa kwake, lakini mpaka inaingia saa kumi na mbili akukuwa na taalifa ya ziada, zaidi ya ile ya asubuhii, kuwa muuwaji wakike amekamatwa, lakini akukuwa na mwendelezo wahabari hiyo, kiasi mzee Soud akaingiwa na shaka, pengine kuna jambo lime tokea, kamasiyo kuuwawakwa binti huyo ilikuficha uovu wa mzee Masinde ambae mpaka sasa inasemekana yupo polisi, basi huyo binti atakuwa ameshatoroka, ***** saa moja narobo kagiza ndiyo kwanza akalikuwa kana lifunika hanga la dunia, mitaa ya mbezi luis karibu na sheri ya chuo, lilionekana Toyota V8, la mzee Nyati liki yoyoma kuelekea kibamba ccm, japo lilikuwa speed kali, lakini lili pitwa na gari mbili za polisi, kama vile lilikuwa limesimama, gari hizo za polisi zilikuwa ni msafara wa Johnson ambae alisha ona kuwa Denis anausika naupotevu wa Jackline, maana ile asubuhi kuna ujanja umefanyika, hivyo moja kwa moja ilikuwa ni kwenda kumkamata Denis, kwa kumsaidia mkewake kufanya ualifu, 


 Wakati huo huo Kibamba njia panda, Denis alikuwa nyumbani kwake, akiendelea kunywa pombe na rafiki zake wakina Mahadhi, lakini licha yakunywapombe nyingi sana, akusahau maneno ya mkwe wake mzee Nyati, “kuwa awe karibu na simu yake sababu mama Jackline atampigia simu muda wowote, ni kweli akiwa katika maongoezi ya kilevi na unywaji wa pombe, mala akasikia simu ile ya Jackline ikiita, akaitazama mpigaji, iliandikwa mama, hapo Denis akapokea simu mala moja huku anatoka pale sebuleni na kuingia chumbani kwake, “shikamoo!!..... Shikamoo mama! aliamkia Denis huku akijitaidi kuongea vizuri asimkosee adabu mama mkwe, lakini akasikia suti ya upande wapili ikicheka, huku inaitikia, “marahaba mwanangu, bado hupo nyumbani?” Denis alistushwa na sauti hiyo ambayo kwakiasi kikubwa sana ni kama ya mkewake mama France, “ndio ..... ndio, nipo na rafiki zangu wamekuja kunitembelea .......” alijibu Denis, kisha akaongeza “yani kama mke wangu angekuwa huru ningesema niyeye naongea nae, mmefanana sauti vibaya sana” awakina Mahadhi walimsikia DENIS akiongea na huyo mama yake huku anainuka na kuelekea chumbani kwake, ambako alitumia muda sana, wakina Mahadhi walimwona Denis akitoka chumbani na kuingia sebuleni, na kuwakuta wao wakiendelea na vinywaji, wakamwona Denis akachukuwa kopo moja jipya la bia, na lile alilokuwa analinywa mwamanzo, kisha akamyanyua mwanae France, na kuelekea upande wa jikoni, wao awakujuwa chochote, waka endelea kunywa pombe lakini azikupita dakika tano, wakasikia mungurumo wa magari yaliyo ingia kwafujo pale nyumbani kwa Denis, wote wakaenda kuchungulia madirishani, wakawaona polisi wenye silaha, wakiizunguka ile nyumba ya Denis, “mh! mwenzetu shida anayo” aliongea Boss James, huku anatazama mlangoni, ambapo walimwona insp Johns akiwa ameongozana na askari wawili wenye silaha, akaiwata redio iliyo kuwa inatoa burudani mle ndani, na kuchomoa waya wa umeme kwa kuuvuta, “watu wote mliopo humu ndani njooni hapa sebuleni,” aliongea insp Johnson, kwa kujiamini kabisa akiwa na uwakika kuwa Denis mume wa Jackline amesha mnasa, Mahadhi, Janeth na boss James, wakatazamana, kama awaja mwelewa insp, anaongea nini, “inamaana amjanielewa, nita watowa izo pombe zote mlizo kunywa sasa hivi, nasema watu wote waliomo humu ndani, mje hapa haraka sana, awezi kutoroka eneo  hili nje kuna askari wengi sana” aliongea insp kwa sauti kari kuliko ile ya kwanza, “Denis! Denis!” aliita Mahadhi kwa sauti ya kilevi iliyo changanyika na uoga, wote wakatazama upande wa jikoni, wakitegemea kumwona Denis akija sebuleni kutokea jikoni, lakini awakuona mtu, “mnauakika alielekea huko jikoni?” aliuliza Johnson, huku akimkazia macho Mahadhi, ambae alionekana kuwa ni muoga kuliko wenzie, “ndiyo... ndiyo tena ameenda sasa hivi” alisema Mahadhi akitaka kuinuka kwenda kumtazama Denis, kule jikoni alikoelekea na mwanae France, “we! unaend wapi ebutulia hapo” alisema polisi mmoja huku akisukuma Mhadhi arudi kwenye kochi, kama alivyo kuwa amkaa mwanzo, Mhadhi akajibwaga pwah!, nusu amwangukie Janeth aliekuwa amekaa jirani, kisha yule  askari akiwa na silaha yake, aina ya SMG, akaelekea jikoni, ambako alitumia kama nusu dakika hivi, akarudi peke yake, “akuna mtu afande” alisema yule askari, “inamaana nyie mnadanganyasiyo, Denis yupo wapi?” aliongea insp kwa sauti ya ukari sana, “mzee atuwezi kuku danganya, Denis alikuwa amekaa hapa sasa hivi” aliongea boss James, huku akionyesha kocho la pembeni yake ambalo kwa sasa lilikuwa tupu, “akapigiwa simu na mama yake, akainuka na kumchuwa mtoto akaelekea jikoni, sasa atujuwi ameelekea wapi” aliongea boss James kwa sauti tulivu lakini lionekana wazi amelewa, hapo insp akaagiza askari waongozeke toka nje na kuikagua nyumba nzima, kitendo kilicho tumia dakika kuminzima, mpaka wale askari kurudi na kusema awajaona kitu, “amesha toroka huyu mshenzi”  alisema insp Johnson kwa ghadhab huku akionyesha ishara kwa askari wake waondoke zao, wakina Mahadhi wakatulia wakiwatazama walepolisi wakitoka nje, na ikifwatia miungurumo ya magari, kisha yakatokomea, “duh! jamani hapa apatufai” alisema boss James kwa sauti ya kukata tamaa, huku akijiinua kwenye kochi, “sasa nyumba tunaiachaje?” aliuliza Janeth, akiwa bado kwenye Kochi, huku Mahadhi nae akiwa tayari amesha inuka, “kama mwenyewe ameikimbia wewe utaiweza vipi?” alijibu Boss James, ambae alikuwa anachukuwa bahadhi ya bia toka mezani, “basi tuifunge alafu akirudi atatutafuta” alishauri Janeth, huku akiinuka, na kuchukuwa makopo mawili ya bia, Mahadhi nae akainua Katon moja ambalo alikufunguliwa kabisa, kisha wakatoka nje na kufunga mlango, giza lilisha kuwa jingi sana, **** baada ya kuwa wameongea na Denis na kuona kuwa asingeweza kuondoka mwenyewe pale nyumbani, kutokana na kulewa sana, ndipo mzee Nyati ambae alikuwa anajukumu lakumalizia pale Hospital, akashauri Jackline aende akawawai mwanae na mume wake, wakampatia gari, silaha na simu, wao wakibakia na bastora, kila mmoja ya kwake, na Jackline akaondoka kuwai kibamba, Jackline ambae alishuhudia polisi wengi sana, wakiwa katika mavazi ya kazi na wengine kiraia, wakiendelea kumsaka yeye alie valia vazi lake la kiuguzi, alili liiba leo mapema kwa yule nesi, ndio wakati alipo pitwa na magari mawili ya polisi yakielekea anako elekea yeye, siyo kwamba alijuwa kuwa yale magari yana elekea nyumbani kwa mume wake, ila aliingiwa na wasi wasi kwamba uenda mume wake atakuwa katika matatizo, ndipo alipo amua kumpigia kwakutumia simu aliyopewa na mama yake, na leo ndio siku pekee aliyo pokea salamu ya shikamoo, tokwa kwa mume wake na kujikuta akicheka mwenyewe, kabla ya kuitikia, akishindwa kijitambilisha, akiofia chapombe kufichua siri, akaongea kama mama yake, wakati huo na yeye alikuwa amesha fika maeneo ya shule ya msingi Kibamba, na kuliegesha gari karibu na barabara ***** “ndiyo mheshimiwa, nikweli ametoroka, lakini mpaka sasa atuja watangazia wananchi, sababu tuna fanya juhudi za kumkama tena” aliongea CGP, kwa sauti ya unyenyekevu mkubwa, akionyesha aliekuwa anaongeanae kwenye simu ni kiongozi mkubwa sana wanchi, kisha akasikiliza upande wapili, ambao wenzake awakuusikia ulichoongea ila walihisi, kutokana na maongezi ya CGP, ambae aliendelea kuongea, “ndiyo mheshimiwa, tutajitahidi kwa kila njia atapatikana, kabla ya juwa kuchomoza” maongezi yalihisia hapo na simu ikakatwa, CGP najopo lake bado walikuwa ofisini kwa CGP, wakiendelea na mjadala, ambao kiukweli ulikuwa unawaumiza vichwa vyao, huku bahadhi yao wakiwa na methodopa (dawa za kushusha mapigo yamoyo) pembeni wakizi bugia kila baada ya masaa kadhaa, wakishusha pressure zao,ambazo zilikuwa zinapanda ovyo ovyo, “jamani hii simu inatoka kwa raisi, ebu nielezeni nikwanini huyu mshenzi anafanya mauwaji kwa awa wastaafu?” kiukweli wanadhimu awa walimwona mkubwa wao akiwa amekasirika kweli kweli, hapo wote wakatazamana, ikiashiria akuna mwenye jibu la swali hilo, “inamaana tokea mwaka juzi mpaka leo atukujuwa chanzo cha mauwaji?” alikoroma CGP, wote kimya, “naagiza mala moja, yuu mzee kama amepata nafuu, akahojiwe juu yahili, nazani itasaidia kupata mwafaka” japo ulikuwa ni ushauri lakini ni amri kwa mkuu wa upelelezi, “ndiyo afande itatekelezwa” alijibu Chief  Cid, na kuinuka kuelekea ofisini kwake, ambako alichukuwa simu yake ya mkononi, na kumpigia insp Johnson “ndiyo afande nakusikiliza” ilisikia sauti ya insp ambae alionekana kuwa yupo njiani, maana muungurumo wa gari ulisikika kwa fujo, “unatokea wapi mida hii” aliuliza mkuu wa upepelezi, “nipo njiani natokea kibamba, tumegundua kuwa kuna mtu alikuja kumtazama Jackline Nyati mahabusu, ndie alie mpatia dawa iliyo msababishia aonekane kuwa mgonjwa” aliongea insp, akieleza mkasa mzima, kuhusu Denis na mwanamke, aliejifanya doctor Magreth, ambae inasadikiwa kuwa ndie alie msaidia kutoroka kwa Jackline Nyati, Johnson alimaliza kusimulia mkasa mzima, na Chief Cid, akapata lakusema kwa Chief General of Polisi, “imeagizwa yafanyike mahojiano na mzee Masinde, ili kupata chanzo cha yeye na mwenzie kuwindwa na muuwaji” hapo Chef Cid akasikia sauti ya kushusha pumzi nzito ya Johnson ikisikika, “afande nilienda kwaajili hiyo, lakini nilimkuta akiwa na hali mbaya kidogo, sikuweza kufanya nae mahojiano” alijitetea Johnson, sababu mimi nawewe mdau tunajuwa kuwa mzee Masinde amesha mweleza kila kitu mwanae, “ok! tembelea mala kwa mala, ilikujuwa hali yake akiweza kuongea, fanya hivyo haraka” alimaliza Chief Cid, na kukata simu, kisha akarudi kwenye ofisi ya CGP, akapiga saruti na kuanza kutoa report, “afande, insp Johnson alienda hospital leo asubuhi ma kujaribu kuhoji maka ulivyo agiza, lakini hali ya mgonjwa ilikuwa bado siyo nzuri, akashindwa kupata maelezo” aliongea Chief Cid, akiwa amesimama mbele ya kiti chake, akajikohodha kidogo, akiwapa wenzake nafasi ya kuandika anacho kiongea, Chief Cid akaendelea, “pili katika uchunguzi wa mwanzo, insp amegnduwa kuwa kuna watu wawili wameshiriki kumtorosha Jackline” Chief Cid, aliwekatena kituo akimtazama CGP, ambae alikuwa ametulia akimtazama kwa umakini, huku wengine wakendelea kuandika kwenye vijitabu vyao vidogo vya kumbukumbu, mkuu wa kitengo cha upelelezi akaendelea, “wakwanza ni wakiume ambae imefahamika ni mume wake, ambae mwanzo inasemekana akuwa anajuwa lolote juu ya mke wake, ambae amezaa nae mtoto mmoja, anaejulikana kwa jina la Denis, lakini wameenda kumkmata nyumbani kwake kibamba wamekuta ameondoka mdafupi kabla ya wao kufika” alieleza Chief Cid, na kuwaduwaza wanadhimu wote mle ndani, **** mzee Nyati na mke wake, walikuwa ndani ya viwanja vya hospital ya muhimbili, watu waikuwa niwachache sana, ni baada ya kuwa muda wakutazama wagonjwa umesha pita wana ndoa awa wali likuwa wame tulia kwenye canteen ya le ndani, ya hospital, wakitazama kwenye jengo kubwa la wagonjwa maalumu wa dharula “wacha nikamalize zoezi, wewe wasiliana na wakina Jackline” alisema mzee Nyati huku, anamakabidhi mke wake simu yake na kofia yake ya mduara, anainuka, “sawa nakutakia mafanikio, mimi utanikuta nje, alijibu mama Jackline huku na yeye akiinuka, wakaachana njia, wakati mama Jackline akielekea wenye geti la kutokea nje ya hospital, mzee Nyati yeye alielekea kwenye kibanda kidogo, kinacho tumiwa na watu wanao usika na wafanya usafi pale hospital, akaingia ndani ya kibanaa hicho na kukaa humo kwa dakika chache kisha akatoka akiwa amevaa nguo cover loly, na kofia ya mkeka kichwani nan doo maalumu ya kusafishia sakafu yenye ffagiao ya mshiuko mrefu ndani yake, akatoka na kuelekea kwenye sehemu ya maegedho ya magari, ambayo ilionekana kuwa na magari machache sana, nyingi zikiwa ni ambulance, tano, magari machache ya kawaida binafsi, na gari mbili za polisi, ambayo ayakuwa na mtu yoyote ndani, akaonekana mzee Nyati akielekea kwenye magari hayo ya polisi, alipo yafikia akachuchumaa karibu na tairi lanyuma la gari hilo,


La polisi, la upande wakulia, akiwa aijulkani acho kuwa anakifanya, alipomaliza akainuka na kulifwata gari lapilli, nail akafanya hivyo hivyo, **** insp Johnson baada ya kumkosa Denis nyumbani kwake na kuongea na mkubwa wake wakazi akapata wazo la  kwenda hospital ya muhimbili, kuonana na baba yake, ili kumzuwia asije akaongea ukweli juu ya kile walicho mfanyia mzee Nyati, nchini congo mwaka 1988, akamweleza dereva wake, aelekee mhimbili, nae akafanya hivyo, huku gari lingine la polisi lii wafwata nyuma yao, likiwa limesheheni askali walio kuwa tayari kivita, Johnson akiwa pembeni ya dereva wake, akaanza kukumbuka bahadhi ya mambo ambayo, yalitokea katika kipindi hiki chote, akamkumbuka Jackline jinsi aliyo mtoroka pale Paradise Tower, “huyu mwanamke ni hatari sana,” alijikuta akiropoka Johnson, kabla maneno ya Jackline ayaja mjia kichwani mwake, “insp mimi siyo muhimu kwako, achana na mimi, muwai baba yako hospital, pengine akakueleza machache ambayo akuwai kukueleza, pia msaidie kuficha ushaidi wa yule mwanamke kahaba, wa hotelini, waliotaka kumchinja” ni maneno ambayo aliyaongea Jackline leo asubuhi pale mahabusu, “alijuwaje kama baba ataniambia aliyo niambia” aliwaza Johnson bila kupata jibu, **** “mama hileeee” ilikuwa ni sauti ya France aliekuwa amebebwa na baba yake begani, akitazama walikotoka, “hivi we mtoto leo umekunywa pombe kama mimi” aliuliza Denis, kwa sauti yakilevi, huku mkono mmoja akiwa ameshikilia kop la bia analoendelea kulinywa na mkono ulio mshikia France ulikuwa na kopo ambali akuwa lime funguliwa,  akiendelea kutembea kwa kuyumba yumba, wakati huo walikuwa wanaingia kwenye eneo la shule, “mamaaa!” akasikika tena France ambae safari hii alianza kujipapatua toka kwa baba yake, akitaka kushuka chini, “wee acha kuhota, kabla ujalala, nitaoekana nimekunywesha pombe” aliongea Denis akianza kupepesa macho, maana akujuwa alichokifwata maali hapa, “baba France, wacha nikusaidie mtoto” ilisikika sauti toka nyuma ya Denis, nisuti ya mkewake kabisa, “mamaaaaaaa!” alistuka Denis kwa mtuko mkubwa  sana, ni baada ya kugeuka na kumwona mke wake akiwa amevaa nguo nyeupe, Jackline akwai na kumziba mdomo, “nini sasa mume wangu?” aliuliza Jackline huku bado amemziba mdomo mume wake, kisha akaanza kumwachia taratibu, “huuffff! nilizania mzimu, ha! wamesha kuachia?, na hii nguo yeupe umeitoa wapi?” aliuliza kwa pupa Denis, huku akihema kwa nguvu, kama ametoka kukimbizwa, “ebu elekea kwenye lile gari jeupe, tutaongea kwenye gari” alisema Jackline akimchukuwa France toka kwa baba yake, wakaelekea kwenye gari huku Denis akionyesha wazi kufurahishwa na kitendo cha kumwona mke wake, France ndiyo usiseme, utazani alikuwa anajuwa kilicho mtokea mama yake, walitembea haraka na kuingia kwenye gari “sasa tunaenda wapi?” aliuliza Denis mala baaada ya kuona gari linaelekea upande wa barabara kuu na siyo nyumbani kwao, “nyumbani siyo salama kwako, muda wowote polisi wanakuja kukukamata, nambaya zaidi wata kupiga sana wakulazimishe useme vitu ambavyo uvijuwi” alisema Jackline, ambaae alikuwa anaendesha gari kuisogelea bara bara kuu, ya dar moro, “ninge komaa tu! kwani sikama viboko vya shule tu!” aliongea Denis kwa majigambo, wote wakacheka, mpaka France asiye juwa chochote, kiukweli walionyesha furaha, “mh! vya shuleni?, yani ungetoka huko unge sababisha nikose utamu” alisema Jackline akikamata barabara kuu ya lami, kuelekea mjini, hapo hapo wakasikia simu ya Jackline ikiita, Denis akamtazama mpigaji, alikuwa ni mzee Nyati, akaipokea, “hallow mzee nipo na komando hapa” aliongea Denis mala tu baada ya kupokea simu, “hallow mwambie Jackline awa haraka sana, tunaitaji” ilisikika sauti ya mama Jackline kwenye simu, “hoo! kumbe siyo baba” ***** ndani ya jengo lefu la ghorofa saba, la emrgence, hapa muhimbili hospital, kwenye kolido la ghorofa ya tatu, walionekana polisi kumi ambao sasa walioneka kuzidiwa na uchovu wa hali ya juu, ni kutokana na kushinda mahali pale, wakimlinda mzee Masinde, maana kwa kawaida uwa kuna mapokezano ya askari, kila baada ya saa kadhaa, “unajuwa huu ni usumbufu, yani kwa gharama za vyakula hapa, ukipata milo mitatu kilasiku, kwa wiki nzima si watoto awaendi shule?” alilalamika askari mmoja, alafu usikute wenyewe wamekorofishana kwenye umabiashara yao, alilalmika mwingine, kisha maongezi yakaendelea, huku kila mmoja akilitoa lake la moyoni, wakati wanaendelea na mlalamiko yao, mala wakaona lifti ikionyesha ishara kuwa inapandisha juu, ikiwa na namba tatu, maana yake kuna mtu ana kuja kwenye flow hile, ni nadla sana lift hii kutumika, wote wakaacha maongezi na kuitazama ile lift, ilijihesabu na kusimama, kisha wakaona lango wa lift ukijifungua, alafu ikawa kimya, yani akutoka mtu, wote wakashangaa, na kuanza kuusogelea ule mlango kwa tahadhari kubwa na silaha zao wame zielekeza kwenye lift, tayari kumfyetulia mtu aliemo ndani, endapo ataoneka siyo mwema kwao, walipo ufikia wakashangaa kuona kuwa akukuwa na mtu zaidi ya ndoo ya kudekia na fagio yake, wakatazamana kwa mshangao, huku wanashusha silaha zao, kwakujuwa zilikuwa hofu zabule, lilikuwa kosa kubwa sana, kwani waliskia kishindo cha wenzao wawili wakianguka kwapamoja, ile wanageuka kushangaa, wakamwona mtu mmoja alievalia sale za wafanya usafi, nas kofia a mkeka, akiwa anajivilingisha wa srakasi ya chini, kama tairi, huku bastora yake yenye kiwamba sauti, ikiwa mkononi mwake, ikitema risasi kwa umahiri mkubwana, zilizo tuwa kwenye vichwa vyao na kuwa dondosha chini, nikta chache wote walikuwa chini akuna aliwai kufyetua ata risasi, mzee Nyati akatoa kimkebe cha risasi toka kwenye bastora yake, na kukitazama, kisha akatabasamu, “risasi kumi watu kumi, inapendeza” alisema mzee huyu huku anachukuwa kimkebe kingine na kukiweka kwenye bastora yake, akaikoki bastora yake na kuiweka mfukoni, na kuokota kofia yake iliyo mvuka, wakati ana jivilingisha, akaivaa kichwani kwake, alafu akauendea mlango wa chumba cha mgonjwa, akajariu kuufungu, nao ukakubari, **** wakati huo mzee Masinde alikuwa amelala kitandani, huku akiwaza atimayake, maana ukiachilia kunusulika kuuwawa lakini pia alikuwa amepoteza kiungo muhimu sana katika maisha, akufikilia vijana wake waliouwawa pale hotelini, yeye aliwaa juu ya dudu yake, hapo alivuta picha ya mkewake akitoka nje yandoa, kuifwata dudu, hapo mzee Masinde akamkumbika Nyati, ambae alimwona miaka mingi iliyo pita, Nyati akiwa kijana mdogo sana, ambae licha ya upole wa kijana huyo pia alikuwa mwenye mahalifa mengi katika mapigano na mipango ya kimapigano, Masinde akakumbuka moyo safi wa kijana huyo wakupatia vipande saba vya almas, kwa lengo la kukagawana, hapo Masinde akajichukia kwa roho aliyo ionyesha kwa kijana huyo, ambae mategemeo yake, ni mkumpoteza duniani kabisa, “haaaaah! sijuwi kachawi kale kakijana” aliwaza mzee Masinde, na wakahuo huo akaona mlango wa chumba kile ukifunguliwa, akaingia mtu moja alie valia sale za wafanya usafi, kichwani amevalia kofia la mkeka, “major David Johnson Masinde , pole sana” alisikia mzee Masinde, ambae bado alikuwa anamtazama mtu huyu, na sasa mzee Masinde alionyesha mshangao, maana mfanya usafi huyu alionyesha kuwa anamfahamu toka siku nyingi, “habari za siku nyingi afande” alisema yule msafishaji, huku akimsogelea pale kitandani, “kwani tulisha wai kuonana au kufahamiana?” aliuliza mzee Masinde, ambae akuweza kujiinua atakidogo, kutoka pale kitandani, “sidhani kama unaweza kunisahau katika maisha yako” alisema yule mzee mfanya usafi huku akitoa kofia la mkeka kichwani mwake, mzee Masinde akaduwaa, “mama yangu Nyati?” alisema mzee Masinde, huku ametoa macho kama aliona MV Mapinduzi (meli) inapita barabarani, “ndiyo mimi, nimuda mrefu sasa toka mwaka 1988, kule Nyilagongo” alisema mzee Nyati, huku akiwa ameachia tabasamu, “umefwata nini hapa, sema unacho taka nikupe, niafedha nyingi sana” aliongea kwapupa mzee Masinde, huku wasi waasi mwingi ukiwa ume mtawala, kabikira mbele ya wauni sita wanao taka kumbaka, mzee Nyati alitabasamia pembeni, “kamanda unakuwaje uoga hivyo, ule ujasiri wako huko wapi major?” aliuliza mzee Nyati, huku akitabasamu, “hapana Nyati, naomba unisamehe, hadhabu niliyo ipata natosha, nipo tayari kulipa chochote unacho taka” aliongea mzee huyu alie tamani kunyanyuka na kupiga magoti aombe msamaha, lakini ndiyo hivyo tena, “Masinde ulishindwa kunilipa kwa kusna asante, ukanilipa kwa risasi ya kifua, leo utanipa nini kitacho futa dhambi yako?” alisema mzee Nyatii kwa sauti tulivu kama anaongea na rafiki yake walio kwaruzana kidogo, “lakini ... lakini kama hadhabu umesha nipa Nyati,  kuwa na huruma” maneno hayo ya Masinde yali mfanya Nyati acheke kidogo, “unaona lahisi kumsamehe adui kuliko kumsamehe alie kutendea wema?’ aliuliza Nyati, na hapo Masinde akuweza kujibu zaidi alitoa macho ambayo yalikuwa yana ashilia kuomba msamaha kwa Nyati, “ulishindwa kuni samehe, kwakuwa uliona hasara kuniachia kipande changu kimoja cha almas kati ya saba ambavyo nilivitoa kwenu, una ahisi ni lahisi mimi kukusamehe wewe, ulie jaribu kuyachukuwa maisha yangu?” alisema mzee Nyati huku anaitoa bastora yake kutoka mfukoni, na kumlenga mzee Masinde kichwani, “tafadhari kijana...” aliongea mzee Masinde lakini kabla ajamalizia akatulizwa na risasi tatu za kimya kimya, zilizo topa kwenye paji lake la uso na kufumua kisogo chake, na kuchafua mashika meupe ya kitanda kile cha wagonjwa, “pumzika major” alisema Nyati, kisha akatoka mle chumbani na kushuka ngazi, akiziruka zile maiti za askari kumi, kuelekea chini, ile anafika ngazi ya mwsho akakutana na muhuguzi akiwa anaanza kupandisha ngazi kuelekea juu alikotoka, hapo mzee Masinde akajuwa anaiyajika kutoka haraka sana, kabla yule nesi ajapiga kelele, za kuona maiti za askari pale kwenye gholofa ya tatu, mzee Nyati ambae alitoka akiwa amevaa nguo za wafanya usafi, alienda moja kwa moja mpaka kwenye lango kuu la kutokea nje, akawapita walinzi wakampuni binafsi ya ulinzi, akaapungia mkono, na kupita zake, lakini wakati huo huo akayaona magari mawili ya polisii yakiingia pale Hospital, yakipitia kwenye lango la kuingilia, yeye akatabasamu huku ana mtazama mke wake aliekuwa amesimama mita kama mia moja kutoka pale langoni, akamfwata, “wasiliana na Jackline mwambie tukutane njiani” alisemamzee Nyati huku wakianza kutembea kuelekea Fire, mama Jackline akachukuwa simu, na kumpigia Jack, ***** magari hayo Mawili ya polisi yalikuwa ni yale, ambayo yapo kwenyemsafara wa insp Johnson, yalienda moja kwamoja mpaka kwenye lile jengo la wagonjwa maalumu wa dharula, wakasimama nje ya jengo lile wakimshuhudia nesi mmoja akitoka nje ya jengo hili, mbio mbio huku akipiga kelele, utazani anakimbizwa na mzimu, “nakufaaaaa” alipiga kelele yule nesi, kiukweli muda huo eneo hili alikuwa nawatu kabisa, hapo insp Johnson akashuka haraka toka kwenye gari, wakati huo wale askari waliokuwa kwenye magari yote mawili, walikuwa wamesha ruka atakabla magari ayaja simama vizuri, na kukaa tayari kimapigano, insp akamkimbilia yule nesi, ambae nae baada ya kuona polisi wakiingia eneo lile, akawakimbilia, “tulia nieleze kunanini?” alisema insp Johnson, baada ya kumshika yule nesi wakike, “polisi.. polisi wote wamekufa” alisema yule nesi kwapua, “baba” alisema insp Johnson, huku akiwa ameganda, macho akiyaelekeza safu ya gorofa ya tatu, askari wote waka mtazama insp, wakisubiri amri, lakini insp alionekana kama sanamu lisilo na hisia yoyote, akuna aliejuwa ni kwanini, mala wakamwona ana anza kukimbia kuufwa mlango wa kuingilia wa jengo lile, ***** kituo kikuu cha polisi, mambo hayakuwa mazuri, maana bado walikuwa awajapata taalifa ya kupatikana Jackline au washirika wake, ambao ni mama aliejifanya doctor, na mume wa Jackline aliekuja kumtazama mahabusu, wakati huo huo, ikaja taalifa kutoka hospital kuu ya muhimbili, taalifa amayo ili mfikia mkuu wa kitngo cha upelele, na kuzidi kuwachanganya wanadhimu awa ambao walikuwa bado wapo ofisini, nyumbani akuendeki, “jamani kuna taalifa ya kushangaza na kustusha kidogo” alisema Chief Cid, wote wakatega masiko yao, kusikiliza hizo taalifa, “kwanza kabisa mzee Masinde, yani yule mgonjwa alie nusulika jana, amesha uwawa kwa risasi ndani ya ward aliyo kuwa amelazwa” aliongea Chief Cid, na CGP kahamaki, “nini, yulemgonjwa kauwawa?” ilikuwa ni sauti iliyo jawa na mshangao mkubwa sana, “ndiyo afande, ila kingine ni kwamba ajafa peke yake, walio uwawa kwenye tukio hili ni pamoja na askari kumi waliokuwa wanamlinda” maneno hayo ya Chief Cid, nusu yachomoe roho zawatu, maana pressure zao zilipanda kwa kiwango kikubwa, hapo ungewaona wakiangaika kubugia vidonge, vya kuzuwia mapigo yao ya moyo, yasipande sana, “ila afande kitu cha kushangaza, kumbe Marehemu Masinde, ni baba mzazi wa insp Johnson” hapo ofisi nzima ikazizima kwa ukimya wa hali ya juu, wakatazamana kwa mishangao, “jaribu kutofutisha wakati wa utani, CC, inawezekanaje hilo jambo?” aliuliza CGP, kwa sauti ya taratibu iliyo jaa mshangao mkubwa sana, 

.

“afande imebainika, kuwa ni baba yake baada ya insp kuingia kwenye chumba ambacho mzee Masinde alikuwa amelazwa, na kumkuta mzee huyu amesha pigwa risasi, insp akaanza kulia akitaja baba! baba!, kisha insp akapoteza fahamu hapo hapo, na hivi sasa yupo hospitalini hapo anapatiwa huduma yakwanza” hapo wanadhimu wote, na CGP mwenyewe wakashusha pumzi kwanguvu, “ok! insp Johnson atolewe katika uchunguzi huo, apewe mapumziko ya msiba, na achaguliwe mwingine wakushika nafasi yake” aliagiza CGP, kisha akamalizia CGP, mwisho ichunguzwe zaidi uenda kuna mambo mengi tusyo ya fahamu juu ya mwenendeo mzima wa uchunguzi wamwanzo, sababu bado atuja juwa sababu ya mauwaji kwa awa wastafu” ***** mzee Nyati na mkewake Anitha, au mama Jackline walikutana na Jackline aliekuwa na wakina Denis, kisha wakaingia kwenye gari na safari ikaendelea, “naona mkwe amepumzika” alisema mzee Nyati akitazama DENIS aliekuwa ameuchapa usingizi na kopolake la bia mkononi, France akicheza mapjani kwa baba yake, wote wakacheka kidogo, “sasa tunaenda wapi?” aluliza mzee Nyati, “nina promise ya diner kwa insp, wacha nikamsubiri, najuwa sasa hivi atakuwa anamlilia baba yake” wote wakacheka mle ndani ya gari, “babu njoo ukae na mimi” aisema mzee Nyati akimchukuwa France na kukaanae seat ya nyuma, karibu na mama Jack, ***** shughuli ilikuwa kwa insp Johnson, ambae alirudiwa na fahamu, nusu saa baadae, akaganda aki wazajambo flani, “Jack umeniweza, Jack umenikomesha” alijisemea insp huku madoctor na bahadhi ya askari wenye silaha wakiwa wamezunguka kitanda alicho kuwa amelazwa, wakihisi kuwa insp amechanganyikiwa, kumbe insp aliongea kitu alicho kijuwa kabisa, insp alivuta sura ya Jackline, Japo mala ya kwanza alipo mwona alimwona kuwa ni mwanamke mrembo na mzuri sana, lakini sasa aliona kuwa ni shetani mkubwa, la mguu mmoja, insp akajilahumu kwa kuwai hospital asubuhi, kuliko kubaki kituo kikuu kuakikisha huyu mwanamke afanyi ujanja wowote, “mimi siyo muhimu, wai kamatazame baba yako, pengine analolote la kukuambia” ilijirudia kauri ya jackline, kichwani wake, “kumbe alikuwa anajuwa kunamtu akuja kumletea hiyo dawa” aliwaza insp ambae alikuwa amewekewa drip mkononi mwake, ghafla insp akaonekana kustuka, kisha waka msikia akijiuliza kwa sauti ya chini, “chakula, usiku, nyumbani kwangu, alikuwa na maana gani?” wote waliokuwa mle ndani wakatazamana, kwa mshangao, “hapana, mama Betty na Betty” alipiga kelele insp huku akiinuka pale kitandani, huku akichomoa ile sindano ya drip, akakusanya kila kilicho chakwake,koti lake (yani shati la juu la kipolisi, na buti zake, alizoenda kuvalia kwenye gari, basipo kusahau bastora yake, na kofia, huku nyuma akifwatiwa na askari wake aliokuwa nao mle ndani alikokuwa anapatiwa huduma ya kwanza, ile kutokea nje askari wengine nao waka panda kwenye magari, kisha safari ikaanza kuelekea mbezi bichi, nyumbani kwa insp, huku insp akichukuwa simu yake na kumpigia mkewake, simu iliita sana pasipo kupokelewa, mpaka ikakatika, “baba ume mponza mke wangu maskini....” alisema insp huku akishindwa kujizuwia kulia, akiamini kuwa Jackline alisha fika nyumbani kwake na kufanya yakwake, “endesha gari haraka sana” alipiga kelele Johnson, akimpiga dereva begani, kiasi cha dereva mwenyewe kushangaa, maana mwendo aliokuwa anatembea, aukuwa wanchi hii, na barabara zetu, Johnson akajaribu tena kumpigia simu mkewake, zaidi ya mala tatu, lakini aikupokelewa, mpaka hapo insp Johnson David Masinde, akajuwa amesha poteza familia, “kwanini sikukumbuka mapema jambo hili, na mtu alisha niambia kabisa” alisema insp kwa ghadhabu, akijishushia lawama kubwa sana, wakati wana pita makongo,  akastuka kuona simu yake ikiita, akaichomoa mfukoni, na kuitazama akaona mpigaji kuwa ni mke wake, “haaaaa! Jackline” alijikuta Johnson amelopoka pasipo kujielewa, maana alijuwa kuwa simu ile ya mke wake, itakuwa mkononi kwa Jackline, ni baada ya kumaliza kuwa chinjilia mbali, “akaipokea kwa unyonge na kuweka sikioni pasipo kuongea neno lolote, mapigo ya moyo yakamwenda mbio, “hallow baba Bitte,” ilisikika sauti ya mkewake ikiwa na mng’amu ng’amu ya usingizi, insp akashusha pumzi kwanguvu, “mke wangu mpo salama hapo nyumbani? kwanini uliacha kupokea simu?” maswali mfululizo yalimtoka insp, “nilikuwa nimepitiwa na usingizi, vipi salama huko?” aliuliza mama Bitte, akionyesha kutia shaka juu ya Jambo flani, “salama tu nakuja huko nyumbani” alisema insp akijitaidi kuficha majonzi aliyo nayo, “saw nakusubiri, maana nimekuwekea chakula, nikajuwa utarudi mapema” aliongea mke wa insp Johnson akionekana aninuka toka kitandani, “sikia mama Bitte, usi fungue mlango mpaka nitatumia funguo yangu” alisema insp, ambae uwa nautaratibu wa kutembea na funguo yake ya ziada asa inapotokea kuwa na kazi za usiku, wali maliza maongezi na kukukata simu, kisha insp aka achia tabasamu pana sana, **** Chief Cid alipata taaliafa kuwa insp amesha zinduka na sasa anaeleka nyumbani kwake kuiwai familia yake, ambayo inaweza kuingia matatizoni, hapo Chief akampigia simu insp ilikumjulisha kuwa kuanzia muda ule alikuwa likizo fupi, na kumwuliza kama angeitaji msaada zaidi, lakini kili alipo piga simu ilikuwa inatumika, mpaka alipo amua kumpigia mtu mwingine aliekuwa karibu na insp, ilikufkisha ujumbe, na kwabahati mbaya alikuwa gari jingine, wakapanga kumjulisha watakapo fika, nyumbani kwa insp huyo, ***** saa tano usiku, magari mawili ya polisi yalitililika kwa mwendo wa speed ya kuzima moto, na kujikuta wakipiga bleck za nguvu, ndani ya kiwanja cha nyumba ya insp Johnson, huku askari wakiruka na kuizunguka nyumba hiyo, insp nae Johnson akashuka faster, na kufwata mlango wa nyumba yake, huku akiutoa funguo mfukoni mwake, akafungua mlango nakuingia ndani ambako kulikuwa nagiza, nikawaida kuzima taa zandani, nyakati za usiku, insp akapilitiliza mpaka chumbani kwake anako lala na mke wake, akamwona ndio kwanza anaonekana kupitiwa na usingizi, akumstua akaelekea chumbani kwa mwanae Beatrice, nae akamwona amelala fofofo, hapo insp akatabasamu kwanguvu, nakurudi sebuleni, akatoa kavua kofia yake na kuiweka juu ya meza ndogo ya kioo, kisha akaitoa bastora yake ambayo ilikuwa na risasi zilizo jaa, maana akuwa amitumia siku hile, nay o akaiweka juu ya ile meza ndogo ya kioo, iliyo zungukwa na makochi ya kisasa, akatazama kwenye meza kubwa ya chakula, japo kulikuwa na giza, lakini akaona hot pot za vyakula, ni kawaida ya mke wake kumwekea chakula,  ata akirudi usiku sana, lazima angekuta chakula mezani, insp akatoka nje na kuongea na msaidizi wake, mwenye cheo cha sajenti, “nyie nendeni, mimi siwezi kufanya lolo kwa sasa, tutakutana kesho kituo kikuu” alisema insp, na yule sajent akamwambia, “ila afande kuna ujumbe toka kwa chief, amesema umepewa likizo fupi, kwaajili ya kufanya taratibu za mazishi” maneno yale ya sajent, insp aliyapokea vyema, maana atainge kuwaje, lazima ange chukuwa likizo hiyo, kwaajili ya mazishi ya baba yake, baada ya kuagana na asakari wake, na wao kuondoka zao waka mwacha insp akizunguka nyuba yake kuikagua, na alipo ona kuwa ni salama, akaingia ndani, safari hii akawasha za sebuleni, ile mwah! macho yake yaka tuwa moja kwamoja kwenye meza kubwa ya chakula yenye viti vitano, huku kimoja kikiwa kimekaliwa na mwanamke, alie valia nguo za wauguzi, yani gauni jeupe, “mungu wangu, Jackline” alisema insp Johnson kwa mshangao na mstuko mkubwa huku akiitazama kwenye meza dogo ya kioo, lakini baastora  aikuwepo,  zaidi aliion kofia tu, “ndio mimi Jackline Nyati, je unaitafuta hii?” aliongea Jackline, huku akimwonyesha insp bastora yake, ambayo muda mfupi alikuwa ameiacha mezani, na sasa ikikuwa mikononi mwa Jackline, ambae alikuwa ame tulia kwenye kiti, pale kwenye meza ya chakula, insp akujibu kitu akakodoa macho kama mwizi alie kwiba sanduku la vitabu vya dini akizani fedha, “muda wa chakula cha usiku, auitaji hii” alisema Jackline kwa sauti ya taratibu kidogo, Johnson bado alikuwa ameduwaa, akimtazama Jackline kwa mshangao, nikama anajiuliza “ajafanya lolote huyu?” insp akatazama mlango wa chumba cha mkewake, ulikuwa umefungwa kama alivyo uacha wakati antoka nje, akatazama mlango wa chumba cha mwanae, nao ulikuwa umefungwa kama alivyo uacha wakati anaenda kuagana na askari wake, “husiwe na wasi wasi insp, sijaja kivita, wala kumdhuru mtu yoyote humu ndani, nimekuja kwaajili ya kile chakula ulicho niahidi” alisema Jackline kwa sauti ile ile ya taratibu, kama ujaja kuni dhuru mimi na familia yangu umefwata nini?” aliongea insp kwa sauti ya chini pia, “nimekuja kula chakula chajioni ambacho uliniahidi, au ulikuwa unanitania?” aliuliza Jackline ambae uongeaji wake, usinge zani kama ni muuwaji mkubwa, insp akujibu kitu, zaidi alijishika kiuno kwa kuchoka na mambo anayo ya shuhudia mbele yake, “ameingia saangapi?” aliwaza insp akiwa bado amesimama utazani ni mgeni pale nyumbani, “mbona ukai Johnson, au unajiuliza nimeingiaje?, niliingia ulipokuwa unazunguka kukagua nyumba, ukasahau kuwa umeacha mlango wazi” aliongea Jackline huku anatabasamu, “mimi mjinga sana” aliwaza insp, lakini Jackline nikama alikuwa anamsoma mawazo yake, “ok! ilo aliniusu sana, chamsingi ni kuwa, nimemekuja kukuambia kuwa, mambo yameisha, tena bahati nzuri ukweli wote umesha ujuwa, siyvyo insp?” aliongea Jaackline akimtazama insp, ambae alikuwa kimya kabisa, “akimsikiliza Jackline” licha ya kujuwa jinsi baba yako alivyo mfanyia baba yangu mwaka 1988, pia ume gunduwa kuwa baba yako alikuwa wewe ba baba yako mmejaribu mala nyingi kuni uwa” alisema Jackline kwakituo, ata kabla ulificha uovu wa baba yako, lakini ukashindwa kumkataza asifanye mahovu” hapo insp akashusha tena pumzi nzito, kuashilia maneno yalikuwa yana mwingia, kuona hivyo Jackline akaendelea, “japo sina uakika kama utaendelea kufwatilia kesi hii, lakini nakuomba kaambali na mimi” ssababu auna makosa yoyote” alimaliza Jackline huku anainuka toka kwenye kiti, alichokuwa amekalia, hku ameibeba ile bastora ya insp, “kwaheri Johnson, asante kwa chakula” aliongea Jackline, ambae safari hii alicheka kidogo, huku anaiweka ile bastora ya insp juu ya meza yakioo, kisha akaanza kutembea kuufwata mlango ambao bado ulikuwa auja fungwa kwa funguo, pasipo kujuwa kuwa nuyma yake, insp Johnson aalichukuwa bastora yake haraka sana, kisha akaikoki, hapo Jackline akasimama, akiwa ameutazama mlango, “simama hapo hapo Jack, ukipiga atuwa moja tu! nakufyetua” ilisikika sauti kali ya insp, ambae alikuwa ameunyoosha mkono wake wenye bastora, kumwelekezea Jackline, ambae alitulia kidogo na kushika kitasa cha mlango, na kufungua mlango, hapo ikasikika itaendelea ........


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.