SALAMU ZIMFIKIE
Salamu nawandikia , mlokuwa Viragoni,
Naanza naye Sophia , Alisi Tedi ✳Iani✳,
Nuru na Patricia , kisha Sababu Rudeni,
Salamu zimfikie , toka kwangu Manueli,
Wazee wa ukulima , kina Juma wa kanyama,
Naye Mohamedi Rama , Dama Brenda Halima,
Na hedigirl Neema , na yuno Mzungu Juma,
Salamu zimfikie , toka kwangu Manueli,
Kuna Karisa Riziki , pia Karisa Safari,
Demu aitwa Riziki , na yuno Pendo Shikari,
Naye Thomas miswaki , sawa na Mody Bacari,
Salamu zimfikie , toka kwangu Manueli,
Naendeleza salamu , ziende kwake Kauli,
Pia kwake Mariamu , Joy na ndiguye Neli,
Rashid na Mariamu , naye Magreti Ali,
Salamu zimfikie , toka kwangu Manueli,
Kukutaja so makosa , we Tatu mwana wa Charo,
Pia Thomas Karisa , lifisi ndani ya daro,
Hakosi Pendo Karisa , kwao huko kanairo,
Salamu zimfikie , toka kwangu Manueli,
Kunaye Rehema Mweni , Zawadi Thinga na Baraka,
Mapenzi kiwa miyani , kusoma na kuzunguka ,
Kuna Kazungu Rubeni , eti naye kaongoka,
Salamu zimfikie , toka kwangu Manueli,
Bibie Zawadi Ngonyo , asinaye na kinyongo,
Wenzake aliwapa onyo , kina Rashid Chengo,
Asoitaka ponyonyo , mwana wa chonjo mapengo,
Salamu zimfikie , toka kwangu Manueli,
Tatu kazungu Japheti , Mkuuu Ngumbao Ngala,
Kiongozi wa kamati , ya wapendao kulala,
Dole mlinzi wa geti , Kahaso mpenda kula,
Salamu zimfikie , toka kwangu Manueli
Salamu hazijaisha , bado zinaendelea ,
Kuna Ali pia Masha , Nyevu na Dama Kayaa,
Yuko Pili pia Musha , Manu nawasalimia,
Salamu zimfikie , toka kwangu Manueli,
Tamati nimeshafika , Manueli ninatua,
Beti kumi zimefika , bado tu kupiga dua,
Kisha ninapumzika , uchoovu kuutoa
Nyote ni nawasaluti , mlosoma Viragoni.
✳Ian✳ Ian pascal Ringoma aliaga dunia mwaka wa 2020 Mola ni aendelee kuilaza roho yake mahala pema peponi
Na: Emmanuel Charo
Shairi tulivu kweli
ReplyDeleteYour Thoughts