MSICHANA YULE

MSICHANA yule macho yake malegevu,

Mie kwake nikawa mpumbavu,

Hadi nikatamani kumla mkavu mkavu,

Ila kajitia uvumilivu kutaka kula mbivu,

Nikajikuta namtekenya kwenye mbavu,

Nalo domo likawa zege ile mbaya mbovu

Badala ya kuwa simba kajikuta nakuwa ndovu,

Moyoni nikajiacha na kovu,

Kabakia tu kusema MSICHANA YULE,


MSICHANA YULE fundi wa kucheza kwaito,

Mwendo wake wa batobato,

Alifanya niachane na mseto,

Nilokula nikiwa bado mtoto,

Hata nikilala alinijia kwenye ndoto,

Huko akinipa mahaba mazito,

Yaani huwa raha mpwito mpwito,

Wallah ningekuwa na uwezo ningempa kito,

Ila sina nabakia kusema tu MSICHANA YULE,


MSICHANA YULE sura yake mashalah!

Meno yake meupe kama maziwa lalah,

Mapaja yake meupe yaani walalah!

Dodo zake nzuri na hazija lalah,

Nyuma kichuguu yani ukimuona utataka kula lah!

Ni mzuri kila mahalah!

Kila kitu kwake amepewa mbasharah!

Ni kweli tabakia kusema MSICHANA YULE,


MSICHANA YULE hata jina lake silijui,

Maana sikumpa hata Hi!

Ila natumai kule yuko bado yuko hai,

Kusema kweli aliniacha hoi,

Nikawa sijijui sijitambui,

Nikajikuta naropoka MSICHANA YULE.


NA : Emmanuel Lee

© 2019

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.