SIKU ISIYO NA JINA
NA: Emmanuel Charo
WhatsApp: +25496273110
Sehemu ya kwanza
Upepo mwanana unaouvuma Kwa mwendo wa Kobe, sauti ya mawimbi ya bahari hindi haikuwa sababu ya kijana huyu aliyeegemea chuma zilizo katika fukwe fiche za bahari hindi viungani mwa jiji la Mombasa, kutomsikia binti aliyekuwa akimunyemelea Kwa hatua za kinyonga. Ukweli ni kwamba hata huenda sauti za mawimbi pia alikuwa hazisikii.
Binti hatimaye alifika mahali hapa aliona ni dharau za wazi wazi kijana huyu kutotambua uwepo wake mahali hapo, alidiriki Hadi kupitisha mikono yake mbele ya macho yake lakini akagundua kuwa kijana huyu hapepesi hata macho yake.
"Au amelala huku amesimama" aliwaza binti huyu.
"Ama amekufa, mmmh! Wa Aina yetu hatuwaezi kufa kizembe namna hii" aliendelea kuwaza binti huyu.
"Hivi atakuwa hanioni au"
Kwa mara ya pili alipeleka mikono yake katika uso wa kijana huyu na kugusa mapua yake, hii ilimshtua kijana huyu
"Ooh! Umenishtua kweli"
"Ulikuwa unaota nini? Maana ni nusu saa tangu nimefika hapa"
Mmmh! Acha uongo basi nusu saa na ndio umefika sasa hivi"
"Hali niliyokukuta nayo hapa imenifanya hadi ni kabadili mawazo"
"Kabla mawazo yako hajabadilika yalikuwa yepi maana mie hufanyia kazi mawazo original" kisha akaachia kicheko hafifu kijana huyu.
"Kwanza niseme umependeza sana" binti ilimtoka kauli hii na kuanza kumzunguka kijana huyu aliyekuwa amevaa track suit nyeusi , yenye nembo ya nyota ya rangi ya njano karibu kiunoni kwenye mguu wake wa kushoto na juu akiwa amevaa t-shirt ya rangi ya maziwa yenye maandishi meusi kifuani yaliyosomeka "BIG BRO" kweli nguo hizi zilimkaa vyema kwenye mwili wake uliojengeka vizuri bila shaka ni mtu anayependa mazoezi ya viungo.
"Nilikupenda, nilivunja misimamo yangu ya kazi Kwa ajili yako", binti machozi yalianza kumtiririka na kulowanisha mashavu yake.
"Lakini malipo yake ukanifanyia haya, au dhumuni lako katika penzi letu lilikuwa hili?" Aliuliza binti huyu
Kijana huyu alimtazama binti huyu bila kutoa kauli yoyote,
"Labda huelewi nazungumza nini au natumia lugha ngumu ambayo huelewi maana upo kimya tu."
"Ni kweli sikuelewi kamwe", alijibu kijana huku akiweka mkono wake wa kushoto mfukoni mwa Ile track suit yake.
"Ningekushauri uende moja Kwa moja Kwa kile kilichokuleta hapa, sikuwa na miadi na yeyote yule Leo hii, na nimefanya wema kusikiliza sentensi zako zisizo na mantiki hadi sasa" alihitimisha.
"Sitaki nifanye makosa tena, Acha misingi ya kazi yangu iniongoze" alisema binti huyu ambaye mashavu yake yanazidi kulowa Kwa machozi.
"Hebu nisikilize Nuru, ni nini shida hasa, umefika mahali hapa hata sijui nani kakwambia Niko huku na huongei vitu vya kuelewaka ni wewe tu na kulia,
"Nambie basi mamii shida nini" kijana huyu kwa mara ya kwanza analitamka jina la binti huyu; Nuru, kisha mkono wake wa kushoto unaibuka kutoka mfukoni ukiwa na kitambaa cheusi chenye nyota ya njano katikati na kumsogelea Nuru kwa nyuma na kumshika kiuno kwa mkono wake wa kulia huku mkono wake wa kushoto ulioshika kitambaa ukitambaa kwenye ubavu wa kushoto wa Nuru kuelekea usoni na kumfuta machozi Nuru. Mkono wake wa kulia ukiwa na kazi ya kukibinyabinya kiuno cha Nuru.
Kijana huyu kwa vitendo vyake hivi ni kama alichochea moto kwani Nuru muda huu aliangua kilio Kwa sauti, Kisha aligeuka na kumkumbatia Kwa nguvu kijana huyu na kuendelea kuangua kilio.
Kijana huyu alipata kazi ya kumnyamazisha Nuru huku akimpigapiga mgongoni.
"I love you Manu, nakupenda sana licha yote ulionifanyia bado nakupenda"
"Ujue unanichanganya Nuru Mimi na wewe hatuja kosana , unapoongea haya unanishangaza na sielewi unaongea nini"
"Manu acha kujitia hamnazo wewe ni m...
"Nuru acha kupoteza muda, muda ndio huu" sauti hii ilimkatiza Nuru alichokuwa anataka kumwambia Manu, ilitokea katika kidubwasha alichovalia kwenye sikio lake la kulia
" Nisikilizeni nyie wehu, japo kayafanya haya lakini pendo langu kwake bado lipo pale pale bado nampenda na sioni sababu ya kutekeleza mpango wenu. Acha sheria ichukue mkondo wake maana ushahidi upo." Alipomaliza kusema hayo alivua kidubwasha hicho na kukirusha baharini.
*********
"Hey Nuru unasikia hello! Hello!"
"Mkuu ni kama Nuru ameenda kinyume na mpango wetu" sauti hii ilitoka Kwa kijana mmoja aliketi kwenye kiti cha chuma kwenye jengo chakavu pembezoni mwa makupa police station jijini Mombasa akiwa na kompyuta mpakato mapajani mwake
"Ok plan B ifanye kazi" ilisikika sauti mbovu na Kavu toka Kwa kompyuta ya Yule kijana
Alibofya nambari kadhaa Kisha akatoa agizo
"Abdul time for plan B"
"Ok but it's too late maana hadi navyozungumza na wewe wako mita Mia tano wakiwa Kwa boti wakielekea kaskazini"
"Abdul mbona hukunijulisha"
"Hey boss sheria ni kuwa wewe ndio unanitafuta"
"Mkuu target inaelekea kaskazini Kwa njia ya boti"
"Najua anaelekea wapi, Kwa iyo achana naye nawakabidhi wenzenu waendeleze mlipoachia"
Kisha kompyuta mpakato ilijizima yenyewe
"Dah! Afadhali Acha niende zangu mama Ngina nikajitulize aliwaza kijana huyu.
********
"Kutoka hapa hadi visiwa vya Pemba ni kilomita kumi, hivyo nitakuacha hapa"
"Nuru unawazimu hapa tupo katikati ya bahari sijui tulikotoka ni wapi wala hapa ni maji ya nchi gani" Manu alitahamaki
"Ruka na uanze kuogelea kuelekea magharibi huko ndio muelekeo wa visiwa vya Pemba, muda haupo upande wangu Fanya kuruka basi"
"Nuru nambie ni nini hicho nilikufanyia hadi utake niliwe ni papa"
"Manu acha kupoteza muda ruka na uogelee kuelekea magharibi"
Manu alisita kuruka , Kwa Kasi ya ajabu Nuru alimsukuma Manu ndani ya bahari na kuitoa boti Kwa mwendo wa umeme.
******
WIKI TATU KABLA
Jioni hii Angel alikuwa pembezoni mwa kibarabara kilichotokea hospital kuu ya kaunti ya Siaya "Siaya county referral hospital" Angel alikuwa mfanyakazi katika hospital hiyo kama "Occupational therapist." Kila mtu ana bahati yake baada ya kuhitimisha tu masomo yake ya "diploma in occupational therapy" toka chuo cha Ugunja KMTC alipata ajira katika hospital hii.
Angel alikuwa msichana mwenye urembo wa kipekee. Nywele zake ndefu na maridadi zilikuwa kama shirika la mapambo asilia. Macho yake yalikuwa ya rangi ya bahari ya kina, yakisimulia hadithi zisizojulikana, na tabasamu lake lilikuwa kama jua lenye joto la kutosha kumtuliza yeyote aliyemzunguka. Lakini urembo wake haukuwa tu kwa nje, bali pia kwa ndani.
Angel alijulikana kwa moyo wake wa dhahabu. Alikuwa na uwezo wa kusikiliza, kusaidia, na kuhudumia wengine kwa upendo mkubwa sifa kubwa Kwa mtu wa afya. Alikuwa mcheshi na mwenye hisia za kipekee, na watu wote waliokuwa karibu naye walijisikia wakipata faraja na furaha kwa uwepo wake.
Si kawaida yake kusoma gazeti hasa kwani aliamini hupata kila taarifa aliyohitaji kupitia simu yake janja lakini jioni hii alijikuta akivutwa hasa kusogelea kibanda cha muuza magazeti kilichopo karibu na chuo cha Siaya kmtc gazeti maarufu nchini Kenya JABA PLANET EVENING NEWS ukurasa wa mbele ulikuwa umepambwa na picha kubwa na kijana mwenye tabasamu pana aliyevalia shati la kijani lenye mikono mirefu iliyokolezwa rangi nyeusi huku kichwani akiwa ana chepeo cheusi.
Angel moyo ulianza kumuenda mbio sio kawaida
"Ni yeye kwani asharudi lini mbona hajanijulisha" alijisemesha, Angel alidhani ameongea Kwa sauti hafifu lakini kumbe sauti ile ilimfikia muuza magazeti
"Hey mrembo unataka gazeti nini au umeshangazwa na utanashati wa jambazi nini?"
"Jambazi gani" aliuliza Angel
"Si huyo umemkodolea macho, Jina jambazi hata halimfai ni muuaji, hebu soma headline kwanza wewe unaona utanashati unapagawa utaba..."
"Nyamaza basi" alisema Angel na kulichukua gazeti lile alichokisoma hakuamini alitarajia kuona amepokelewa kama shujaa lakini amepokelewa kama muuaji
"DAKTARI MUUAJI AWASILI NCHINI" Taarifa ilianza hivyo
Emmanuel Charo Kahindi mshukiwa wa mauaji ya aliyekuwa mkuu wa idara ya ujasusi hapa nchini Frankoo Sari awasili..."
"Noooo!" Angel alipiga kelele na kuanza kuvuruga kibanda kile cha muuza magazeti.
Muuza magazeti alibaki kinywa wazi.
"Si bure umerogwa wewe"
"Samahani kaka" Angel alimuomba radhi muuza magazeti kisha akamtolea kibunda cha elfu tano za Kenya
"Samahani Kwa kukuharibia zitakusaidia",
halafu huyo akaendelea na safari yake.
Jioni hii iliharibika Kwa msichana huyu.
"How is it possible?" Alijiuliza, ndio maana hajanitafuta, Kisha alifurukuta mkoba wake na kuibuka na simu na kulitafuta jina "Manu" na kupiga nambari ile. Tunasema simu inaita lakini haikujibiwa.
"Ooh my God kichwa kinaniuma" alijishika kichwa chake mrembo huyu.
"Acha nifike nyumbani nione nini nitafanya, haiwezekani ndiye alimuua Frankoo. Kifo cha Frankoo kilitokea Manu akiwa bado Urusi mbona sasa ashukiwe yeye, hii haiwezekani hata kidogo"
Angel alijikuta amefika nyumbani kwake. Nyumba aliyoijenga Kwa pesa yake, kweli kila kijana ana ndoto kama ya Angel kufanikiwa wakiwa bado na umri mdogo.
Lakini kwa Angel si ndoto bali yeye ashayatimiza.
Nyumba ya Angel ilikuwa ni ngome ya ndoto zake. Kila asili ya nyumba ilijengwa kwa kufuata maelezo ya kina ya usanifu na mapambo ya kipekee. Paa lake la nyumba lilionekana kama skuli ya fumbo, na milango yake ilionyesha kama lango la kuingia ulimwengu wa kimalaika.
Mazingira yake yalikuwa kama paradiso, na katika bustani yake, maua yalikuwa yakichanua kwa rangi za kuvutia. Kila mmea ulikuwa umepambwa kwa umakini, na njia za kupendeza zilikuwa zikiongoza kwenye maeneo ya siri ya nyumba yake.
Ndani ya nyumba yake, kila chumba kilikuwa cha kipekee. Vyumba vilikuwa vimewekwa kwa rangi zenye kupendeza na mapambo ya kuvutia. Samani zilikuwa zenye ubora na kila kona ilionyesha ustadi wa usanifu.
Uzuri wa nyumba yake ulikamiliishwa ni yeye mwenyewe Angel alikuwa mrembo kweli. Lakini yeye aliamini nyumba hii ilikosa kitu kimoja "Manu."
Aliingia ndani na moja Kwa moja akaelekea katika chumba chake cha siri kama alivyokiita, kilichojaa vitabu vingi vinavyohusu masuala ya afya Kisha na kuifikia meza moja wapo ilikuwa imebeba tarakilishi ya kisasa
Alichukua namba ya Manu na kuiweka kwenye tarakilishi na kidoti chekundu kilitokea kwenye skrini pale
"Mombasa" aliguna Angel
"Lazima niende Mombasa"
Angel alimpigia mkuu wake wa kazi bwana Adongo na kuomba likizo ya wiki mbili kwani amepata dharura
Adongo amfahamu vyema Angel hivyo alimwambia hakuna shida ya yeye kupewa likizo hiyo lakini lazima afike hospitali asubuhi ili aweke sahihi.
Hilo kwake lilipita pia pia akaingia katika mtandao wa Kenya airways na kujikatia tiketi kituo cha kuabiri ukiwa ni Kisumu kwani Siaya county haina uwanja wa ndege.
*****
PRESENT/SASA
NAIROBI, KENYA
IKULU
Raisi wa awamu ya kumi wa jamhuri ya Kenya mheshimiwa Willy Baro na naibu wake Rihadh Gahag walikuwa chumba cha mipango ya nchi wakimsubiri kaimu wa idara ya kijasusi; Mafaa Henessa anayeshikilia wadhifa huo kufuatia kifo cha aliyekuwa mkuu wa idara hiyo Frankoo Sari.
Kimya kilitawala chumba hicho na kila mmoja aliwaza yake
Wawili hawa ni marafiki wa muda mrefu hadi kufikia kuingoza nchi yenye nguvu afrika mshariki.
Walipatana mara ya Kwanza katika chuo kikuu cha Oxford nchini uingereza. Yaliyobaki ni historia kwani waliporudi nchini Kenya walijitosa siasani na wakafanikiwa kuchukua ngazi ya juu nchi hii; Uraisi na unaibu raisi wakiwa na matumaini watashinda tena awamu ijayo Kisha baada ya hapo Rihadh Gahag apiganie Uraisi baada ya kukamilisha
miaka kumi kama naibu raisi.
Ushindi wao uligubikwa na mashaka mengi sana lakini idara ya uchaguzi ulitangaza wawili hawa kama washindi, majaribio ya upinzani kupinga matokeo haya yaligonga mwamba baada ya mahakama kuu nchini humu kusema walichopeleka kortini ni "hot air"
Hali ya wasiwasi Kwa nchi wa Kenya ulianzia pale
Mgombea wa uraisi Willy Baro kumchagua Rihadh Gahag kama mgombea mwenza kwani Gahag ana asili ya kihindi, alizaliwa India mji wa Goa, baada ya kukutana na Willy Baro nchini uingereza ndio akafika Kenya. Kwa mjibu wa sheria Mgeni yeyote yule atakuwa mkenya baada ya kuishi miaka saba ama zaidi lakini wale wa kufukua taarifa waligundua Rihadh Gahag ameishi miaka mitano tu kabla ya uchaguzi lakini katika hali ya kushangaza idara ya uchaguzi iliwapitisha na hatimaye wakashinda uchaguzi.
Bila kuficha, siku ya kuapishwa naibu raisi Rihadh Gahag alikuwa kituko, wakati wa kula kiapo alikosea hata kile alichokuwa ameandikiwa ni yeye asome Tu au labda asili yake eti.
Wengine wakagundua Raisi alipewa katiba na Ile sword Kwa wakati mmoja ajabu ni kuwa aliuinua juu u sword ule wakitarajia pia ataiinua juu katiba, la hasha lakini haikuwa hivyo badala yake alikenua meno na kuendelea kuuinua u sword ule takribani dakika tano. Makubwa hayo madogo yana nafuu Naibu raisi Rihadh Gahag alikejeli wazi wazi raisi aliyekuwa akitoka madarakani Ruhuru Mewatta akisema amechangia maisha magumu Kwa nchi Kwa kukopa madeni makubwa ambayo hayakufaidi wanachi badala yake kunufaisha watu binafsi, pia akadai wana kazi kubwa kuirudisha Kenya mahala raisi wa awamu ya nane Raisi Mui Kabaka alipoachia.
Hata hivyo wananchi walikuwa na matumaini na utawala huu mpya.
Labda usichokijua Raisi Willy Baro ndiye alikuwa Naibu raisi wa Ruhuru Mawatta; Raisi wa awamu ya tisa.
"Unadhani hii itaishia wapi" Willy Baro alivunja ukimya chumbani mule
"Tusubiri Henessa atakuja na nini, maana ni mapema kusema chochote" ilimtoka kauli hii Rihadh Gahag
"Mimi nadhani haikuwa sawa kumsukumia jumba bovu kijana Yule maskini" alinena Raisi
"Raisi kama nilivyosema acha Henessa afike tusikie upande wake" Naibu raisi alishikilia kauli yake.
Kisha kuupeleka mkono wake wa kushoto mezani na kunyanyua kikombe cha Dhahabu kilichojaa kawaha thungu na kupiga mafunda kadhaa
"Yakimwagika hayazoleki, ulimwengu mzima unajua ndiye mhusika, Kwa hivyo futa mawazo ya kulisafisha jina lake"
"Mmmh!" Aliguna Willy Baro
"Oooh nimechelewa lakini nishafika sasa samahani Kwa hilo wakuu" aliingia na kauli hiyo aliyekuwa akisubiriwa Kwa hamu Henessa Kaimu wa idara ya ujasusi.
"Karibu hatuna muda wa kupoteza" alisema raisi
"Nachotaka kujua Kwa nini jumba mbovu mkamsukumia kijana mdogo kama yule, wakati hata hakuwa nchini" aliongea Kwa ukali Raisi
"Kwanza kabisa punguza jazba Raisi, upande wetu haikuwa rahisi wa kumuangushia lawama Ile, si kweli kuwa Manu alikuwa Urusi wakati kifo cha Frankoo bali alikuwa ndani ya nchi hii kenya, mnashangaa na bado na cha kushangaza zaidi alikuwa eneo la tukio alinaswa kwa picha ni maofisa wetu waliokuwa wanafuatilia zoezi hilo Kwa ukaribu kuhakikisha linakamilika Kwa ustadi zaidi. Zoezi lilikamilika bila kikwazo chochote lakini shida ikawa ni nani muuaji" Henessa alinyamaza Kisha kuwaangalia wawili hao
"Endelea" raisi akamuamuru
"Aliye muua Frankoo ni nani? Jibu tukalipata Manu ndiye muuaji wa Frankoo maana ndiye mtu ma mwisho kuongea na Frankoo na alikufa pembeni yake, mavazi Ya Manu yalijaa damu ya Frankoo yote hayo yalinaswa na maofisa wetu, jumba bovu likamuangukia kijana huyu" Kisha Henessa akapiga funda la maji Kisha akaendelea
"Muda huo hatukuwa tunajua huyo ni nani, hivyo tukaweka picha zake katika kitengo ya utambuzi wa sura kwenye idara yetu na majibu yaliyotokea tukabaki vinywa wazi, taarifa iliyotokea ni kuwa jina lake kamili ni Emmanuel Charo Kahindi mzaliwa wa Bombululu mjini Mombasa ana stashahada ya "Occupational therapy" aliyosomea chuo cha Ugunja KMTC Siaya county. Hadi muda huo ni kuwa alisafiri kuelekea Urusi miezi miwili kabla ya uchaguzi wa mwaka 2027. Na hili kuwa hakuwa nchini mnalifahamu.
Hadi mwisho wa taarifa Emmanuel Charo Kahindi alikuwa bado nchini Urusi" alihitimisha Henessa
"Inawezekanaje" alishusha pumzi raisi Willy Baro
"Kama watu wa usalama hii ilitupa tahadhari kuwa huyu Emmanuel maarufu kama Manu si mtu wa kawaida" alisema Henessa na kuwatazama
"Una maana gani" aliuliza Rihadh Gahag
"Hadi kudanganya idara nyeti kama hii wewe si mtu wa kawaida hivyo tukaanza kumfuatilia pole pole, mashaka yetu zaidi ni kuwa huenda hadi hakuenda Urusi. Hilo Hadi sasa hatujalidhibitisha. Tulichokugundua na kutupa ushindi upande wetu ni kuwa Manu anauhusiano wa kimapenzi na Afisa wetu wa usalama wa taifa ambaye pia ni mtoto wa marehemu Frankoo."
"Una maana ya Nuru? Alishangaa raisi
"Nuru bila shaka" alitikisa kichwa Henessa
"Hivyo tukamufuata Nuru na kumwambia Mpenzi wake ndiye alimuua Baba yake, hilo alilikataa pia kwani yeye alijua Manu yuko Urusi, tukamuonyesha hadi picha lakini akakataa katakata."
"Kwa iyo mkafanyaje" aliuliza Raisi
"ikabidi tuendelee kumfuatilia Manu kupitia kitengo cha utambuzi wa sura. Baada ya mauaji hayo kule Murang'a hatimaye kamera zetu zilimnasa jijini Mombasa baada ya wiki moja, ilibidi tumujumuishe Nuru kwa timu yetu akijua tunachunguza wanaohusika katika kifo cha babake, na tukamsisitiza kuwa Mpenzi wake ndiye aliyemuua babake, hivyo tukapanga mpango wetu."
"Mpango gani huo ambao hatuna taarifa yake" aliuliza Kwa hasira raisi
"Raisi hebu kuwa mpole ujue jukumu hili uliniachia mimi hadi ukasema niliendeshe ninavyotaka bora majina yenu yasiingie doa, ukaahidi nikilimaliza basi nitakuwa mkuu wa idara hii rasmi , nakushangaa unaponifokea" alihamaki pia kijana Huyu Henessa.
"Hey Henessa mpango wako na timu yako ulikuwa upi" aliingilia kati Naibu raisi Rihadh Gahag
"Ulikuwa kumuua Manu"
"What" alishangaa Rais
"Mbona uue kijana asiye na hatia" aliuliza Raisi
Henessa aliangua kicheko
"Manu ni nani yako kwani raisi" alinena Henessa na kuendelea
"Sote hapa tunamjua muuaji kama mko tayari apelekwe mbele ya sheria ni sawa maana hadi sasa jaribio la kumuua Manu limefeli"
"Acha utani kijana" alifoka Rihadh Gahag
"Yah! Ni kweli jaribio la kumuua limefeli maana tuliyemtuma Alimtorosha badala ya kumuua"
"Kwa iyo kuna usaliti kwenye timu yenu" alinena Raisi
"Tunaeza sema Yupo aliyemtorosha ni Nuru"
"Dah! Mpango wako mbovu kweli unaezaje kumtuma Mpenzi wake amuue ulitarajia nini" alifoka raisi
"Yote hayo tuliyaona maana Nuru alikuwa hajaamini asilimia Mia moja pia ni kama aligundua baada ya kumuua atakuwa na kesi ya mauaji hivyo tuseme akawa hatua moja mbele yetu"
"Sasa nini kinafuata" aliuliza Naibu raisi Rihadh Gahag
"Kwa sasa tumerudi sufuri ikiwa familia ya Frankoo Sari inataka muuaji akamatwe kabla ya kufanya mazishi ya mpendwa wao"
"Na je mwili wake ushafanyiwa post-mortem"
"Bado hilo liko kifamilia zaidi"
"Dah! Na Nuru Kwa sasa yuko wapi" aliuliza Rihadh Gahag
"Kwa sasa Nuru yupo Kericho Kwa masuala ya kikazi na amejitoa Kwa hiyo kesi ya kumfuatilia muuaji wa babake na kutuambia tumtafute muuaji halisi wa babake na siyo Manu na hadi tulipomuuliza kuhusu alikompeleka Manu alikataa kutujibu"
"Ok Henessa tushasikia upande wako, nini umeamua sasa" aliuliza Raisi
"Kwa sasa kitengo cha utambuzi wa sura bado ndio tegemeo letu maana hatuna hata namba za simu za Manu tulijaribu kufukua lakini tukaambulia patupu hii ikatuongezea mashaka juu yake kuwa si mtu wa kawaida, hivyo tutaanzia chuoni alikosomea tujue alikuwa mtu wa aina gani" Alihitimisha Henessa.
"Kila la heri" kutoka Kwa Naibu raisi Rihadh Gahag
Henessa aliinuka na kutoka chumbani mule. Wakabaki wakubwa wawili.
"Si muamini huyu kijana" aliongea Raisi
"Acha afanye kazi yake" aliongea Rihadh Gahag
"Na vipi yule mwanahabari wa Pakistan" raisi alibadilisha mada
"Muda huu yuko kwenye target za vijana wangu toka India muda wowote anamfuata mwenzake ahera" Kisha aliachia kicheko
"Anastahili lakini anafuatilia yasiyo mhusu" alisema raisi
Mara simu yake Rihadh Gahag ilianza kukiriza kisha akaipokea na kujibizana nayo Kwa muda Kisha akaiweka mezani na kushusha pumzi ndefu
"Tayari amepokelewa mbinguni" akanena
"Vijana wako washapu kweli" raisi aliwapa heko vijana wa Rihadh Gahag kutokea pande za India.
Kisha wote wakainuka na kukiaacha chumba kile.
*******
WIKI TATU KABLA
Saa tatu na nusu asubuhi inampata mrembo Angel akiw ashawasili Jijini Kisumu tayari Kwa safari yake kuelekea Mombasa kumfuata Manu
Ndege yake ilikuwa inafaa kuondoka saa tano. Alirauka, lakini yeye kama mwana afya ni wajibu wake kurauka
Hivyo basi aliamua kulitalii jiji lile la Kisumu
Hivyo akaamua kuelekea maeneo ya Dunga beach fukwe za ziwa Viktoria....
Itaendelea.
Your Thoughts