SIKU ISIYO NA JINA
NA: Emmanuel Charo
WhatsApp: +25496273110
Sehemu ya pili
*******
Ilipoishia
WIKI TATU KABLA
Saa tatu na nusu asubuhi inampata mrembo Angel akiwa ashawasili Jijini Kisumu tayari Kwa safari yake kuelekea Mombasa kumfuata Manu
Ndege yake ilikuwa inafaa kuondoka saa tano. Alirauka, lakini yeye kama mwana afya ni wajibu wake kurauka
Hivyo basi aliamua kulitalii jiji lile la Kisumu
Hivyo akaamua kuelekea maeneo ya Dunga beach fukwe za ziwa Viktoria....
Endelea
Mwendo wake wa aste aste hatimaye alijapata ashawasili Dunga beach, alijichagukilia sehemu pweke na kukaa leo ikiwa jumatatu tena asubuhi basi ufukwe huu haukuwa na watu wengi. Alitoa laptop yake na kubofya namba kadhaa Kisha kidoti chekundu kilitokea kwenye skrini pale
"Bado yupo Mombasa mtaa ni Bombululu, kashakumbuka alikozaliwa" aliwaza mrembo huyu kisha alirudisha laptop Kwa mkoba wake.
"Namshukuru Kwa kunifunza mambo haya ya teknolojia isingekuwa yeye hata nisingejua haya" aliendelea kuwaza Angel hata hakugundua kando yake alikuja kijana na kuketi
"Mrembo unaonekana una mawazo sana" aliongea kijana yule. Angel alimtazama bila kusema neno.
Kijana yule badala yake alinyosha mkono wake
"Naitwa Abdul" Angel aliupokea mkono ule Kwa tabasamu pana kama kawaida yake
"Angel"
"Wow kweli wewe ni malaika, u mrembo ajabu,
Japo mbinguni sijafika
Kwa urembo umewazidi malaika
Mwanaume yeyote rijali akikuona lazima udenda umdondoke"
Abdul zilimtoka kauli mfululizo kumsifia Angel, Abdul alizidi kupagawa Angel aliposimama na kushuhudia urembo wa binti huyu kwa ukamilifu maana Leo hii Angel alikuwa amevaa rinda lililo ishia juu kidogo ya magoti yake hivyo kuacha wazi sehemu ndogo ya mapaja yake meupe yasiyo na doa. Abdul hakushudia hayo Angel alipokuwa ameketi maana alikuwa amejifunika Kwa mtandio wake. Angel alipogeuka na kumpa mgongo Abdul, lahaula! Glasi ya juisi aliyoishikilia ilimdondoka na kubaki ameduwaa. Sijui naye Angel alifanya makusudi maana baada ya sekunde kumi aligeuka tena kumtazama Abdul.
"Samahani kaka mie nawahi ndege naona muda umeenda huenda tutakutana tena"
"Ooh nipe namba yako kama hutojali" Abdul hakusita kuomba namba, kisha akaendelea
"kwani unaenda wapi mrembo"
"hata siendi mbali bado nipo hapa Kenya Tu nafika hapo Mombasa"
"Ooh pia Mimi naenda Mombasa lakini mimi naenda Kwa barabara huwa napenda sana road trip"
"Pia mimi napenda road trip lakini niko na haraka"
"Usijali kwani unaenda sehemu gani uko Mombasa" aliuliza Abdul
"Nyali"
"Ooh sawa mrembo, lakini hujanipa namba yako ujue" alisema Abdul huku aliachia kicheko
Angel aliachia tabasamu lake linayoyeyusha mioyo ya wanaume
"We kaka jamani basi andika basi" Angel alisema na sauti yake kama ameibana hivi
"Yaani wewe ni mrembo si sauti shape yako yaaani dah, yaani mtu hata kama amekasirika akisikia tu sauti yako hasira zinakimbia si kwa ulegevu huo" alisema Abdul naye Angel aliendelea tu kutabasamu
"Wahi basi mrembo usije kuchelewa bure" akamalizia Abdul
Angel aliondoka ufukweni pale akimuacha Abdul akimtazama kwa macho ya tamaa
"Dah! Abdul mie kumbe sijaona warembo hapa nimepata mke walah!" Aliapa Abdul
"Mtoto wa kishua huyu maana usafiri ni wa ndege kisha anaenda Kwa wadosi; Nyali" aliwaza Abdul
"Kazi zetu nazo hazituruhusu kujihusisha na mapenzi ya kweli kumuumiza mrembo kama yule ni dhambi aisee" aliendelea kuwaza Abdul.
Abdul alishtushwa na mtetemo wa saa yake, alibonyeza kitufe fulani kisha saa ile ilitoa maandishi kwenye kioo chake yakimuelekeza afike makao makuu ya polisi hapo Kisumu kwani kuna mabadiliko hapo atakuta helicopter ipo tayari kumchukua kuelekea Mombasa
"Kazi zetu jamani hizi" aliguna Abdul.
Kisha huyo akaondoka ufukweni pale.
BAADA YA MASAA MAWILI
Angel aliwasili Mombasa akafikia Kwa rafiki yake Joan. Joan na Angel walikutana mara ya Kwanza katika chuo cha Ugunja huko kaunti ya Siaya Kwa pamoja wakiwa wanasomea "Occupational therapy" urafiki wao ulikomaa hadi sasa wakiwa washaajiriwa bado wao husaidiana hapa na pale.
"Leo umeamua kunishtukiza sio" Joan alisema huku akimpokea begi ya rafiki yake
"Ndio ili nije ni muone shemeji maana si kwa kumficha huko" angel alijibu akitabasamu huku akiinua mikona yake, Joan alielewa somo kwani alimkumbatia Kwa hisia rafiki yake
"A wapi shosti wanaume hawaeleweki siku hizi Mie nipo kama unavyoniona" Joan alisema Kisha akamuachia Angel
"Karibu nyumbani"
"Nishakaribia mwaya"
"Ndoa yenu lini" aliuliza Joan
"Siezi funga ndoa na muuaji" alisema Angel huku Kwa mbali macho yake yakianza kutengeneza unyevu unyevu
"Angel mbona unaamini hivyo na wewe"
"Ulimwengu mzima unajua kuwa yeye ni muuaji"
"Si hivyo Manu ndio kawasili juzi toka Urusi, haya kamuua vipi huyo sijuii ndio Frankoo"
Kisha Joan aliinuka na kuelekea chumbani kwake kisha akarudi mkononi amekamata gazeti moja Kwa moja alimrushia gazeti lile Angel.
Angel alichukua gazeti lile na kulikunjua na kubaini lilikuwa lile lile aliloliona Siaya
"Nimelisoma tayari hili" alisema Angel
"Kama umelisoma mbona unaamini Manu ni muuaji"
Kauli hii ilimfanya Angel kulitazama tena gazeti Hilo Kisha akarudisha macho yake Kwa Joan
"Hukulisoma, baada ya kusoma Tu headline najua ulishindwa kuendelea maana ni mtu unayempenda, ni kwambie gazeti hilo limemtetea Manu japo ukisoma headline utadhani wanamuongelea kama muuaji la hasha" aliongea Joan
"Mbona asinitafute kama asharudi au kunijulisha kama anarudi" Angel alimtupia kauli hii Joan
"Maybe alikuwa anataka kuku suprise lakini alipotua akakutana na msala huo sasa anaishi kujificha"
"Mbona ajifiche kama yeye si muuaji, nimepoteza imani kwake"
"Angel amini Manu si muuaji na usiwaze Hilo"
"Sikuwaza hata kumsaliti Miaka yote miwili alipokuwa Urusi nilivumilia, nikakwepa vikwazo vya kila Aina lakini kumbe mwenzangu ana yake"
"Angel amini Manu si muuaji"
"Acha kumtetea basi"
Mara simu ya Angel ilianza kuita aliangalia na kuona ni namba haina jina, alitaka kupuzia lakini Joan akwambia labda ni Manu huyo, Alipokea
"Hey malaika Abdul hapa naongea"
"Ooh handsome nambie" alijibu Angel
Abdul hakuamini ameitwa handsome na mrembo huyo akabaki kimya moyo ukimdunda si kawaida, kweli Abdul amepagawa
"Hello Handsome mbona kimya"
"Nikufurahia sauti yako tamu inayoingia kila mahali"
"Mmmh!"
"Kweli pia mimi nimeshafika Mombasa"
"Unanidanganya"
"hata pia Mimi nimetumia ndege ndio maana, badae"
Kisha simu ikakatika.
Angel alishusha pumzi ndefu
"Anaitwa Abdul mwanaume atakayechukua nafasi ya Yule muuaji" akasema Angel
"Shosti acha hizi basi wewe na Manu mmetoka mbali"
"Sikuwaza hilo hadi nakutana na Abdul leo"
"Yaani Una maana mushakutana leo hii"
"Ndiyo safari hii ilikuwa kumtafuta Manu lakini itageuka kuwa likizo fupi ya mapenzi"
"Angel nakushauri kama umetoka Siaya Hadi Mombasa ili kumtafuta Manu usirudi nyuma, uzuri ni kwamba najua mahali anaishi hivyo nitakuelekeza kwake sawa"
"Kweli Joan" uso wa Angel ulipatwa na mng'ao na kutabasamu ghafla
"Jinsi ulivyotabasamu na kutoka katika hali ya majonzi inaonyesha jinsi gani unampenda, pumzika baada ya masaa mawili nitakuelekeza kwake"
Alisema Joan
"Nitashukuru" Angel Kisha akainuka na kumkumbatia tena Joan
"Sina muda wa kupoteza hebu nipeleke sasa hivi" aliongea Angel japo anajua mahali Manu alipo Kwa mujibu wa laptop yake kwani anamfuatilia kupitia namba yake ya simu.
"Ok subiri kidogo nijiandae" Kisha Joan aliinuka na kuingoza chumbani kwake.
Baada ya kama dakika tano Joan alitokea pale chumbani akiwa hana tofauti na alivyotoka hapo
"Shosti buana sasa ulikuwa unafanya nini chumbani" alitaka kujua Angel
"Kujiandaa si ndio" Joan alinena na kuachia kicheko hafifu
"Haya twen' zetu basi" Alisema Angel Kisha na kuinuka pale sofani alipokaa
"Hebu Keti Kwanza"
"Kama nilivyokwambia sina muda wa kupoteza Joan"
"Haya shika hii" Joan alimkabithi kalamu Angel
"Baada ya kutangazwa kama muuaji Manu alikuja kuomba hifadhi hapa kwangu, baada ya kuwatoroka Maafisa wa usalama hapo changamwe kwani alifika nchini Kwa njia ya meli"
"Kumbe ulijua ujio wa Manu na hukunambia" alihoji Angel
"Manu alikaa hapa Kwa dakika tano tu" Joan alipuzia kauli ya Angel Kisha na kuendelea
"Alinipa kalamu hiyo na kunambia siku nitakayo kutana nawe ni kukabidhi" alihitimisha Joan.
Angel aliitazama kalamu ile Kwa umakini kisha akafungua kizibo cha kalamu ile na kugundua ilikuwa chip fulani
"Ni letee begi yangu tafadhali" alimuomba Joan
Joan alifuata agizo na kumchukilia begi Angel
Angel alitoa laptop yake na kuichomeka Kalamu ile mahali pa usb port, mara maneno
"Updated version" yaliyotokea kwenye skrini ya ile laptop Kisha yakafuatia na picha ya Angel na Manu wakiwa wamekumbatiana picha hiyo ilichukuliwa katika uwanja wa kimataifa wa ndege Mjini Malindi siku Manu anaelekea Urusi. Vidoti viwili vyekundu vikatokea vikiwa umbali wa kilomita tano tu, kidoti cha Kwanza kilionyesha Nyali bila shaka alipokuwa Angel na chengine Bombululu
"Manu yupo Bombululu" Angel alivunja ukimya uliotawala chumbani mule
"Aliniambia nikikupa kalamu hiyo utajua mahali alipo kumbe ni kweli, Siri ni gani?"
"Nikuulize Joan Manu hakukwambia anaishi wapi?" Angel naye alirusha swali
"Alichonambia kalamu hiyo ndiyo itanijulisha anaishi wapi iwapo tu itamfikia Angel"
"Kwa hiyo hukujua hata kuitumia maana hata haina ulinzi wowote ule"
"Angel hicho ndicho kimenishangaza, Manu aliniambia anayeweza kuitumia ni wewe peke yake ikiwa utatumia laptop aliyokukabidhi, ikiwa laptop nyengine hata haitosoma" Alishusha pumzi Joan
"Hadi akanipa ni ijaribu hata haikusoma kweli, nimekuwa na wasiwasi huenda pia kwako isisome lakini nimeshangaa".
"Acha nipumzike nitaenda kwake kesho"
"Sawa shost ukikutana naye utajua ukweli wote, nilimuuliza lakini nikaambulia hiyo kalamu" akasema Joan
"Ngoja nikaandae msosi, mgeni najua yuko ubao mbaya" Joan aliongea na kuachia kicheko
"Hata hujakosea twende wote shost"
Wote walielekea jikoni.
*****
Baada tu Angel kuichomeka Kalamu kwa laptop yake Manu alipata taarifa kupitia saa yake maalumu aliyoivaa.
Manu alikuwa katika mtaa wa Vietnam ndani ya Bombululu , alionekana kupata mng'ao wa kipekee baada ya kupata taarifa hiyo.
"Labda anajiuliza Kwa nini sijamtafuta au kumjulisha kuwa niko nchini, sijui kama ananitazama kama nani muda huu" aliwaza Manu
"Akianza tu kunifuatilia kutumia ile kalamu basi nitaenda kwenye zile fukwe nilimpeleka kwa mara ya kwanza aliponitembelea" akatabasamu
"Najua atafahamu mara moja sehemu hiyo pia nina amini itasaidia kuyeyusha hasira zake kwangu"
"Dah hata sijui hili litaishaje, inabidi nipambane ili wananchi na ulimwengu mzima ujue ukweli kile kinaendelea hapa Kenya" aliwaza kijana huyu
Aliangalia simu yake kuona kama Angel ashaanza kuja hapo alipo lakini Kwa zaidi ya masaa tatu hakukuwa na mabadiliko.
"Lazima atakuja" alijipa matumaini.
Baada ya siku tatu Manu ndiyo aliona Angel akianza kuelekea alipo naye akaanza safari Kwa fukwe fiche kama anavyoaamini.
*****
"Mmmh anaenda wapi huyu" Angel alishangaa kuona kidoti kinacho muonyesha Manu kikianza kuondoka mtaa wa Vietnam,
"Try the new feature"
Ujumbe pale Kwa laptop yake ulitokea
"Hii nayo ni gani" alijiuliza badala yake aka finya command ya "ignore" kisha huyo akaendelea kupeleka gari aliyopewa ni Joan
Aliona kidoti hicho kikiwa kimefika workshop, kikasimama takribani dakika mbili, kisha kikaongeza Kasi kwenye barabara kuu ya Mombasa-Malindi
"Amepanda gari huyu, acha niwahi" alijisemesha Angel
Wakati huo ndio anaimalizia Nyali bridge
Angel aliendesha Kwa kasi lakini hilo halikumzuia kuendelea kufuatilia kidoti kile.
Alipofika lights mkabala wa soko kuu la kongowea aliona kuwa Manu yuko maeneo Pirates lakini akiwa anaelekea kaskazini, Angel aligundua Manu anaelekea wapi moyo wake ulianzia kudunda ovyo.
"Anajua namfuaata ndiyo maana, wow I love you Manu" alipayuka Angel.
Baada ya dakika ishirini alifika katika fukwe za pirates, kama kawaida yake watu walikuwa kibao, hakujishughulisha nao alianza kutembea Kwa takribani dakika ishirini nyingine kuelekea kaskazini.
Kwa mbali alimuomba Manu akiyaangalia maji, Angel alitafuta sehemu ya juu kidogo umbali kutoka alipo Manu
"Wow ni yeye hatimaye" aliwaza Angel akitaka kuteremka mahali pale lakini alisita kidogo baada ya kuona msichana mwengine akinyatanyata kuelekea mahali alipo Manu, hivyo alisubiri aone kitakacho endelea.
Machozi yalianza kumdondoka Angel akiwa haamini kile anachokiona.
Japo alikuwa hasikii wanachoongea Kwa umbali alipokuwa lakini vitendo vyao vilimuthibitishia wawili hao walikuwa wapenzi tena wa muda mrefu. Alijihisi apige kelele lakini alijikanya. Aliizungusha shingo yake upande wa magharibi na alichoshuhudia hakuamini macho yake, mita Mia mbili toka alipokuwa alimuomba mwanaume aliyeshikilia bastola na macho yake pia ameyaelekeza Kwa Manu na msichana yule alipomtazama vizuri aligundua mwanaume Yule ni Abdul
"Kumbe jambazi huyu"
Kisha alirudisha macho yake Kwa Manu na alichokiona kilimumaliza nguvu kidogo alizokuwa zimebaki
Manu alikuwa ameshika kiuno yule msichana kiuno toka nyuma kisha yule msichana aligeuka na kumkumbatia Manu Kwa hisia Kali.
Msichana yule alijishika sikio kama anatoa kitu fulani kisha kurusha mkono wake kuelekea baharini, kisha alimvuta Manu na wote Kwa pamoja wakaruka kingo zile za chuma za fukwe Ile na kutumbukia baharini.
Watu wawili waliduwaa Kwa kitendo kile wote wakiwa sehemu tofauti za fukwe Ile.
Kwa mbali boti ya mwendo Kasi iliibuka na kuelekea kaskazini.
Angel alimuona Abdul akiongea na simu kisha huyo akapotelea vichakani.
Angel aliinuka haraka haraka mahali pale na kuteremka kisha alirudi mahali pale alipokuwa maana alikuwa amesahau begi yake iliyokuwa na laptop yake na Ile kalamu aliyopewa ni Joan.
Aliangaza macho yake pale ufukweni na kuona boti iliyotelekezwa aliipanda haraka haraka, akafungua begi lake na kuto laptop na Ile kalamu yake aliichomeka haraka haraka na kuona uelekeo wa Manu na kugundua anaelekea kusini badala ya kaskazini kama walivyoondoka. Alijaribu kuiwasha boti Ile lakini ikikataa kabisa. Ganga ganga za mganga hatimaye boti Ile ilinguruma alianza kuwafuaata wawili wale.
Lakini alisita kuendelea kuwafuaata hakujua usalama wa ile boti pia kiwango cha mafuta, alirudi kwa kinyonge mahala alipoiacha gari ya rafiki yake.
Alivuta pumzi ndefu baada ya kukaaa kwenye gari lakini kuna kitu kilikuwa kinamkera kwenye ile laptop yake, ule ujumbe wa "try the new feature" mara hii alipiga try
"Wow!" Ukemi ulimtoka
Maana kwenye skrini ilitokea ile boti waliyopanda msichana yule na Manu.
Boti ilipunguza mwendo na kusimama, Angel alitazama Kwa makini japo alikuwa hasikii wanachoongea lakini ni kama walikuwa na ugomvi fulani, Yule msichana ghafla alimsukuma Manu ndani ya maji kisha akaiondoa boti ile kwa kasi. Angel alishangaa. Boti ile ilipotea mahali pale na kubaki maji yanayochezacheza, machozi yalimdondoka.
Ghafla Manu aliibuka mahala pale na kuanza kuogelea kuelekea magharibi ghafla kulitokea boti nyengine kubwa kuliko Ile ya msichana aliyemurusha Manu ndani ya maji.
Pia hii nayo iliendeshwa na msichana.
Ilisimama karibu na Manu kisha yule msichana akamsaidia kupanda boti ile.
Angel alishangaa baada tu ya Manu kueka mguu mmoja ndani ya boti laptop yake iliandika 'Signal Lost'
Itaendelea
Your Thoughts