RIWAYA: JESTINA
MTUNZI: Tariq Haji
CONTACT: +255624065911
SEHEMU YA KUMI.
"kwanini waliamua kumfanyia ukatili mwanangu, aliwakosea nini" aliendelea kuongea huku machozi yakimtoka. "usijali mama wote waliohusika na kifo cha Jestina watalipa kutokana na dhambi waloifanya" Alwin aliongea huku hasira zikizidi kumpanda lakini alijitahidi kuzizuia. "nakuahidi mama nitakuletea Jestina mwengine, nipe muda tu mpaka mambo fulani yakamilike" aliongea Alwin na kumfanya mama huyo aachie tabasamu kwa mbali. Waliongea mambo mengine mengi huku kwa muda wakisahau machungu yote ya mambo yaliotokea. Baadae Alwin aliaga na kuondoka na kurudi kwao, moyo wake ulifarijika sana kuonana na familia ya Jestina. Hata wazazi wake waligundua furaha alokuwa nayo na wala hawakujali kumuuliza chochote kile.
***************************
Baada ya kifo cha James waliitana karibu wote wale waliohusika na kifo cha Jestina, "jamani natumai mtakuwa mnajua nini kilichotukutanisha hapa" Jay aliongea baada kikao hicho kilichokuwa na waschana sita na wavulana kumi na moja. "tumeshazika wenzetu watatu, na hatujui atafuata yupi" aliendelea kuongea. "lakini kwa nini tulishiriki kitendo kile" aliongea mschana mmoja alieitwa Christina, "hakuna muda wa kulaumiana saa hivi jambo lile ndo lilishatokea kilichobaki ni kutafuta suluhishi kwa hili linalotukabili sasa hivi" aliongea kijana mwengine alieitwa Mark. "lakini wewe, James, Jay na Matt ndo mloyataka" aliongea mschana mwengine alieitwa Jesca. Walianza kulumbana huku kila mmoja akitafuta wa kumtupia lawama, "sasa mukigombana hivo ndio mtafikia suluhisho, hebu acheni upuuzi wenu" alifoka Jay na wote wakanyamaza kimya. "cha msingi hapa ni kumjua muuaji ni nani" aliongea Jay na kuwashangaza wote.
"kivipi wakati muuaji ni mzimuwa Jestina" alijibu Jesca, "kwanza subiri niwaambie kitu, mimi hasa siamini kama mtu akifa anarudi tena duniani eti akiwa mzimu" aliongea Jay. "cha msingi hapa kwanza tuanze kumfatilia Alwin kila anachokifanya, mi nahisi kama si yeye anaefanya mauji basi atakuwa anamjua muuaji ni nani" Aliongea Jay kwa kujiamini.
"oyaa we umekunywa mchana wote huu mtu wangu" aliongea kijana mwengine alieitwa John, "unadhani boya kama yule anaweza kufanya mauaji, hivi we unadhani kuuwa ni kitu cha mchezo" aliendelea kuongea. "hivi nyie hamjiulizi kwanini mauaji haya yameanza baada Alwin kutoka hospitali ya vichaa, kwanini kipindi chote cha miaka kumi hakujatokea matukio kama haya" aliendelea kuongea Jay na sasa maneno yake yalianza kuleta maana ndani ya vichwa vya wenzake. "hapo kidogo inaanza kugonga ndani ya kichwa changu" aliongea Mark kisha akaendelea " sasa tunafanyaje". "hapo ndio kwenye shughuli yenyewe, inabidi tuanze kufanya uchunguzi chini kwa chini mpaka tuapate ukweli" aliongea Jay na kisha wakaanza kupanga mipango ya kuanza kufanya uchunguzi huku kila mmoja akipewa jukumu lake. Baada ya maongezi ya muda mrefu waliagana na kila mtu alikwenda zake kwao.
**************************
Jesca akiwa chooni anaoga ghafla moshi ulianza kutanda chumbani kwake, na ulipotoweka alianza kuhisi maji ni mazito sana na alipoangalia vizuri alijikuta anaoga damu. Alipiga kelele kwa nguvu huku akitoka mbio chooni, alianza kusikia sauti za ajabu ajabu zikinong'ona. "we nani" aliuliza kwa nguvu, "Jesaca siku yako ndio leo" aliiskia ikimjibu, "utalipa kwa ulichokitenda" yalizidi kusikika maneno. "unadhani mi nakuogopa, kama unajiamini jitokeze mbele yangu" aliogea kwa kejeli. ghafla taa zikazimika na kuwaka, mbele yake alisimama Jestina huku damu nyingi zikimtoka. Sasa Jesca aliamini kama ule ni mzimu, alianza kupiga kelele huku akikimbilia mlangoni kwa ajili ya kutoka lakini mlango haukufunguka. "nimekoma nisamehe Jestina" alianza kuomba msamaha, "siku ile wakati unafurahia tukio lile hukujua kama ulikuwa unakosea" Jestina alijibu huku akimsogelea na kumkaba koo. Jesca alianza kutapatapa huku akijaribu kupiga kelele lakini hazikutoka. Kwa nguvu Jestina alimrusha ukutani na kumbamiza, alimsogelea na kumtandika makucha mara kadhaa. Jesca alipoona hali mbaya, alijinyanyua na kukimbilia dirishani. Kwa nguvu alijirusha na kuvunja kioo, kwa vile chumba chake kilikuwa gorofani alianguka mpaka chini na kupasuka kichwa na hapo ndio ukawa mwisho wa Jesca. Hali ilirudi kuwa shwari na Jestina alitoweka huku akiacha ujumbe anaouwacha mara zote baada kufanya mauaji.
Kishindo kiliskika na majirani pamoja na wazazi wa Jesca walitoka lakini hali waliokutana nayo iliwafanya washangae, Jesca alikuwa chini huku damu nyingi zikitapakaa sehemu alioangukia. Simu zilipigwa polisi na muda si mrefu walifika eneo la tukio, Inspector Hans alifika kuchelewa lakini alifanikiwa kuona mwili kabla haujapelekwa maabara kwa ajili ya uchunguzi zaid. Aliwahoji wazazi wa Jesca kama wanajua lolote kuhusiana na kifo cha Jesca lakini walikuwa hawajui chochote. Basi baada taratibu zote kufanyika mwili wa Jesca uliingizwa kwenye gari na kupelekwa hospitali kwaajili ya uchunguzi zaidi. Vifo hivo viliendelea kuacha gumzo kwa watu wote, hasa watu wa usalama maana kila walipojaribu kuchunguza waliishia kwenye mambo ya mizimu jambo ambalo wengi hawakukubaliana nalo. "jamani sisi tunaonekana wapumbavu sana" aliongea mkuu wa kituo cha inpector Hans, "tukimuacha huyu muuaji atasababisha kuachishwa kazi" aliendelea kuongea.
"mnajua sisi wote tulikosea mwanzo" aliongea inspecta Hans na kuwashangaza wote, "unamaana gani kusema hivo?" aliuliza mkuu wao kwa mshangao. "nina maana kuwa mauaji yote haya yanahusiana na kesi iliyotokea miaka kumi iliopita" aliendelea kufafanua inspector. "Kwahiyo unamaanisha haki haikuyendeka katika kesi ile au" aliuliza kwa hasira mkuu wake.
"kwa kweli mkuu sasa itabidi heshima nieke pembeni sasa maana unataka kunifokea bila msingi, kesi ile ulikabidhiwa wewe na ushahidi wa kutosha kuwa Jestina alibakwa na mwanaume zaidi ya mmoja akiwemo mtoto wa mheshimiwa waziri mkuu Matt, lakini kwa tamaa zako binafsi ukala pesa na kukanusha ushahidi badala yake ukasema kuwa aliebaka ni Alwin. ulifanya hivo makusudi kwa kuelewa kuwa Alwin asingeweza kusema lolote kwa sababu alirukwa na akili. Sasa vyote vinavyotokea leo ujue na wewe umehusika. Na kama nilivokwambia nimekukera basi fanya unalotaka" alimaliza kuongea Inspector Hans na kutoka katika chumba hicho cha mikutano.
***********************************
(miaka kumi iliyopita)
"asante sana inspector kwa kufika hapa japo nimekushtua" aliongea baba yake Matt, "kwa wewe muheshimiwa hata kama ningekuwa nimelala basi ningeamka na kuja" aliongea inspectar Brandon. "sasa inspecta ni hivi kuna kesi umepewa uisimamie lakini kwa bahati mbaya sana kesi hiyo na mwanangu anahusika" aliongea Waziri mkuu ambae ndio baba yake Matt, "una maanisha kijana wetu Matt anahusika na kifo cha Jestina" aliuliza inspecta kwa mshangao. "ndio inspecta, sasa nataka unisaidie kitu kimoja", "kitu gani hicho". "nataka hiyo kesi ife na ikiwezekana ushahidi upotee kabisa au tafuta yoyote tu umbambikizie" aliongea waziri huku akisogeza bahasha iliovimba. "lakini unajua muheshimiwa kazi hiyo ni ngumu sana" aliongea inspecta huku akiimezea mate ile bahasha. "ah halafu ukifanikiwa kufanya hivyo nitaandika barua rasmi upandishwe cheo" aliongea waziri na kuzidi kutia tamaa inspecta Brandon. kuskia hivo aliinuka haraka na kuchukua ile bahasha kisha akasema "usijali mzee nitahakikisha kesi inakwisha mara moja" na kuondoka. Waziri alitabasamu na kujisemea "hakuna kinachoshindikana mbele ya pesa".
Inspecta Brandon alirudi kituoni huku akipanga jinsi ya kuizima kesi hiyo, alikuwa na mawazo mengi sana kichwani hasa alipofikiria kupandishwa cheo. Alitumia mbinu zote anazozijua mpaka akafanikiwa kupotosha ukweli wa kesi hiyo na kumsingizia Alwin kuwa ndie aliefanya jambo lile. Habari za kukanushwa kesi hiyo zilimfikia profesa Alexander Harison, alisikitishwa sana lakini hakukuwa na njia nyingine ya kufanya zaidi ya kukubali tu. Wakati wote huo Alwin alikuwa hospitali hajitambui kwa maneno mengine alikuwa amerukwa na akili. Na kutokana na hilo kesi hio ilifungwa moja kwa moja na hivyo Matt na wenzake kuwa huru. Baada ya tukio hilo ndipo waziri mkuu akaamua kumuondoa kwa muda mtotot wake huku Inspecta Brandon akipandishwa cheo na kuwa mkuu wa kituo chake jambo ambalo hata wenzake hawakujua limetokeaje lakini hakuna alieuliza.
***********************
(baada miaka kumi)
"Profesa tayari wameshaakufa wanne lakini bado hakuna aliekuwa tayari kukubali kuhusika na kifo cha Jestina" alisema Alwin wakati akiwa anaongea na profesa. "tulia kijana madhali hawataki kusema wacha Jestina alipe kisasi kwa kuwauwa mpaka pale watakapokubali kusema ukweli" Aliongea profesa huku akitabasamu. Maongezi yao yaliendelea kwa muda mrefu sana mpaka mwisho walikubaliana wakutane baada wiki moja kujadili tena swala hilo. Baada ya hapo kila mmoja aliondoka na kuelekea nyumbani kwake, lakini Alwin alipita makaburini na kuzuru kaburi la Jestina. "natumai umepumzika kwa amani mpenzi wangu, usijali watalipa kwa kile walichokufanyia" aliongea Alwin na kuweka ua juu ya kaburi la Jestina na kisha akaondoka zake. Jay na wengine waliendelea kumfatilia Alwin wakiamini yeye ndie muuaji na Alwin tayari alishawashtukia hivo kupita kaburini kwa Jestina ilikuwa ni kuwachanganya wanaomfatili pasi na kujua kumbe wao pia wanafatiliwa na Alwin.
"unajua mke wangu Alwin kabadilika sana siku hizi" aliongea Mr Kelvin kumwambia mkewe, "kivipi mbona mi namuona yupo kawaida tu. "hapana mke wangu mi nakwambia tena Alwin kabadilika sana tokea atoke hospitali ya vichaa" alisitiza Mr Kelvin. "mhh haya lakini mi namuona kawaida tu isipokuwa siku hizi kachangamka sana tafauti na zamani" aliongea mama Alwin huku akiachia tabasamu akionesha kufurahishwa na mabadiliko ya Alwin. Wakati wakiendelea kuongea Alwin aliingia na kuwasalimia, waliitika kwa pamoja na baadae Alwin akaenda zake chumbani kwake.
Itaendelea
Your Thoughts