RIWAYA: JESTINA
MTUNZI: Tariq Haji
CONTACT: +255624065911
SEHEMU YA SABA
Alitoa camera ndogo na kupiga picha yale maneno, aliporidhika aliondoka na kurudi kituoni kwa ajili ya kuendelea na upelelezi. Inspector Hans ni afande machachari sana na ni kawaida yake kuona kila mtu anapata haki yake. Hivyo baada kuhamishiwa Mashvile alikutana na kesi hiyo ambayo ilishaafungwa muda mrefu. Lakini kutokana na ukaribu wake na profesa Alexander Harison aliombwa aifungue upya kwa kile alichoambiwa na profesa huyo kuwa "ili kumrudisha Alwin kama alivyokuwa zamani ni lazima kesi hii itatuliwe". Aliayakumbuka maneno hayo alioambiwa na rafiki yake huyo. Profesa Alexander alifanya kwa sababu ya mwanae Miryam ambae ilibidi amhamishe mji baada matatizo yaliotokea lakini pia alihofia mwanae kuchizika. Hivyo akaamua kuvalia njuga kesi hiyo ambayo ni ngumu kupita maelezo kutokana na kuwa mwenye ushahidi hawezi kuutoa.
Upande wa Jestina, "Jestina utarudi duniani kama mzimu, lakini jambo la kwanza ukifika ni kwenda kumwambia ukweli Alwin ili arudi katika hali yake ya kawaida ila kwa sasa huwezi kuonekana mpaka pale Alwin atakapokusamehe na kukubali kuwa wewe umekufa maana mpaka sasa ni mtu pekee ambae anaamini hujafa" Malkia Alina aliongea na kumueleza kila kitu Jestina. "Baada ya hapo muombe akupe damu yake kidogo kwa sababu damu yake itakufanya uweze kuonekana na kutoonekana na pia jitambue kuwa wewe si binaadamu tena" aliendelea kuongea,
"sasa kama unasema siwezi kuonekana mpaka nipate damu yake, nitaongea nae vipi" aliuliza Jestina. "Njia pekee ni kuongea nae ni akiwa usingizini" Alijibiwa na papo hapo mwanga mkali ukatokea. Ulipotoweka alijikuta yuko pembeni ya mtu mwenye manywele mengi sana huku akionekana kama kichaa lakini alipomuangalia vizuri akagundua kuwa alikuwa Alwin. Basi alisogea mpaka pembeni ya kitanda na kupiga magoti, Alwin nae alianza kuota na katika ndoto yake alimuona mschana analia. Taratibu alimsogelea ili kjua nini kilichomsibu.
Alwin: mbona unalia, (lakini alipouangalia vizuri akagundua kuwa mschana huyo si mwengine bali ni Jestina, bila mategemeo alimkumbatia kwa ngvu huku machozi yakimtoka) mi nilijua tu kama hujafa.
Jestina: Alwin naomba unisamehe kwa yote nlokutndea, ukweli ni kwamba nilikuwa nakupenda lakini wivu wangu wa kimasomo ulinifanya nisikubali kuingia katika mapenzi na wewe. mambo yote nilioyafanya nilitaka nikuchanganye ili japo mara moja na mimi nikupite darasani lakini nikajikuta nimejichanganya mwenyewe.
Alwin: mi nilishaakwambia kama nishaakusamehe kwa kila kitu kilichotokea, sasa naomba tuinuke nikupeleke kwenu maana wazazi wako wanakusubiri kwa hamu.
Jestina: Haiwezekani Alwin mimi tayari nilishakufa muda mrefu sana, saa hivi nimepata nafasi ya kuja kulipa kisasi changu kwa wale ambao ndio chanzo cha kifo changu, lakini kwa sasa unaeniona ni wewe tu hivyo ntahitaji damu yako kidogo ili niweze kurudi katika hali yangu ya kawaida na kweza kuonekana pale nnapotaka mtu anione.
Alwin: (kwa hasira) damu yangu nitakupa lakini nakuomba uniahidi kitu kimoja, wale wote waliohusika na kifo chako na wao wafe vifo vibaya sana.
Aliokota kama chupa pembeni na kujikata mkononi, kisha akamzogezea mkono Jestina ambae aliushika mkono huo na kuanza kunya damu. Alwin akiwa usingizini alianza kupiga kelele kutokana na maumivu makali ya kichwa alioyaskia. Wale madakatari waliokuwepo zamu walifika katika chumba chake na kumuwahisha hospitali. Hali ya hewa ilibadilika ghafla na radi pamoja na ngurumo zikaanza kupiga zikiamabatana na mvua kali sana yenye upepo ambao si wa kawaida. Katika kaburi alilozikwa Jestina ilipiga radi kali sana na papo hapo Jestina akatokea juu ya kaburi lake huku macho yakiwa mekundu mithili ya damu. "Matt na wenzako jiandaeni kwani hata mungu hawezi wasaidia sasa, mtalipa kwa kile mlicho nitendea" alijisemea hayo kishaa akacheka kicheko kikali sana na kutoweka eneo hilo.
Harakati za kuokoa maisha ya Alwin zilianza punde tu alipofika hospitali huku madaktari wakijitahi kadri ya uwezo wao. Habari zilimfikia profesa Alexander Harison na bila kuchelewa alitoka kuelekea hospitali, dakika kumi baadae aliwasili hospitali na kutokana na cheo chake aliruhusiwa kuingia katika chumba ambacho matibabu ya Aklwin yalikuwa yakiendelea. Wakati huo daktari alikuwa na sindano ya usingizi mkononi, nia ilikuwa ni kumchoma Alwin ili alale kwa sababu ingemsaidia kukabiliana na maumivu lakini Profesa Alexander alipiga kelele kumzuia "usijaribu kumchoma hiyo sindano utamuua kabisa" aliongea profesa. Kisha akasogea mpaka pembeni yake na kuanza kumgusa sehemu mbali mbali za mwili wake "muacheni hivohivo, yupo katika wakati mgumu sana, akifanikiwa kupita wakati huu basi huenda akapona lakini pia kuna uwezekano kupoteza maisha kwa sababu anazinduka kutoka katika usingizi wa kifo" aliongea Profesa na kuwafanya madaktri wote wamshagae na swali kubwa lilikuwa anajuaje vile bila hata kufanya uchunguzi wa kitaalamu. Lakin hakuna aliemuuliza swali lolotea na waliamua kutoka hasaa katika chumba hicho na kumuacha peke yake akiwa na Alwin.
"Leo nataka nikuoneshe nina uwezo gani katika sita kwa sita" kijana Frank akiwa na mpenzi wake kwenye gari. Alikuwa akiendesha gari kwa kasi sana bila kuchukua tahadhari kama huo ulikuwa ni usiku na barabara ilikuwa imepita katikati kijipori kidogo. Wakati anaendesha alifungua zipu na kutoa uume wake
"oyaa fanya huduma ya kwanza basi" alimwambia mpenzi wake, "we huoni kama ni hatari hiyo" alijibiwa. "acha uboya wewe sasa dereva si mimi, we utakuwa unaramba pipi mi ntakuwa naendesha" alijibu huku akimshika kichwa na kumuinamisha, kuona mpenzi wake kakomaa ilibidi amridhishe. Kutokana na raha kuna wakati Frank alifunga macho, lahaula alipoyafungua aliona mschana kasimama katikati ya barabara na katika harakati za kumkwepa gari ilimzidi na kuacha njia na kupinduka. Ilipotulia Franka alimuangalia mpenzi wake ambae muda mrefu alikuwa ameshakata roho, wakati akihangaika kujitoa akaona miguu kwa nje huku ikichuruzika damu nyingi sana tena yenye kutoa harufu mbaya sana.
Alipepesa macho ma alipoyafungua hakuiona tena, alijitahidi na kufanikiwa kutoka kwenye gari huku damu zikimtoka kichwani. Alianza kutembea taratibu huku akiskilizia maumivu lakini alihisi kama kitu kikimfata kwa nyuma, alipogeuka hakukuta kitu lakini apogeuka tena mbele uso kwa uso na mschana . "wewe ni nani" aliuliza huku akirudi nyuma maana kwa muonekano tu hakuwa mtu wa kawaida, "leo umenisahau" alijibiwa kwa sauti yenye kujirudia. Aliiskiliza kwa makini na ndipo sauti hiyo ikagonga vizuri kwenye ubongo wake "hapana, haiwezekani Jestina kashakufa" aliongea huku haja ndogo ikianza kumtoka. Na ndipo Jestina akaziondoa nywele zake usoni na kumfanya Frank atoe macho kama mjusi aliebanwa na mlango. "Utalipa kwa ulichokitenda, kifo" aliongea Jestina na kupotea, kushuhudia vile Frank alitoka nduki.
"Jestinaaaa...." Alwin alizinduka kutoka usingizini kupiga kelele huku akiliita jina la Jestina, kwa bahati nzuri Profesa Alexander alikuwepo hivyo alimuwahi na kumwambia atulie. Alwin alianza kulia kama mtoto mdogo "kweli Jestina wakufanyiwa vile", "tulia Alwin mimi nipo kwa ajili yako" aliongea Profesa huku akimbembelea. "kwanza nataka kumuona Jestina" aliongea Alwin huku akijaribu kusimama. "mwanangu huwezi kumuona tena", "kwanini" "Jestina ameshafariki na huu ni mwaka wa kumi tokea kifo chake" alijibu Profesa. Machozi yalizidi kumtoka Alwin huku akijilaumu kwanini aliruhusu Jestina wake afanyiwe unyama kama ule. Ilibidi profesa atumie njia za ziada kumtuliza mpaka alipohakikisha ameshaanyamaza, "sasa pumzika kesho utakwenda nyumbani kwani wazazi wako wanakusubiri kwa hamu" aliongea profesa na Alwin alikubali. Baada ya hapo profesa aliondoka na kuwaambia madaktari kuwa keshi atakuja kumchukua Alwin.
Wakati Alwin akiwa amepumzika huku machozi yakilowanisha mashavu yake, ghafla umeme ulizimika na papo hapo Jestina akatokea lakini alikuwa katika umbile lake la kibinaadamu "Jestina" Alwin aliita kwa uoga. "usiogope Alwin mimi siko hapa kukudhuru" Jestina alijibu. Alwin alijaribu kumgusa lakini mwili wa Jestina ulikuwa wa baridi sana. "wewe si ushakufa" aliongea Alwin, "ndio" alijibu Jestina "sasa kama umeshakufa hapa unafanya nini" Alwin aliuliza tena. "ndio hilo nnalotaka kukwambia, mimi nimepewa nafasi ya kuja kuwalipa wale wote walionifanyia ubaya kwa hivyo nakuomba uvumilie kwani wote watalipa vilivyo" aliongea Jestina huku machozi yakimtoka lakini hayakuwa ya kawaida zilikuwa ni damu zilizokuwa zikitoka machoni. Alwin alimshika mkono na kumwabia "mimi niko pamoja nawe na sito pumzika mpaka nihakikishe wamemalizika" kisha akamvuta ili amkubatie lakini Jestina alipotea na kujikuta akikumbatia hewa.
***************************
Mlango ulifunguliwa na kuingia kijana mmoja huku akipiga kelele "nimemuona, jamani nimemuona na anakuja kuniuwa". "oya tulia kwanza, shusha pumzi na ukae kwenye kiti" aliongea mwenzake, "haya tuambie huyo uliemuona ni nani na kwanini anakuja kukuuwa" aliulizwa. "jamani acheni utani nimemuona tena anatisha sana, najuta kwanini nilifanya vile","tuambie basi nani huyo unaemsema". Kijana huyo hakuwa mwengine isipokuwa Frank ambae alionekana kuchanganyikiwa, "oyaa tuambie basi nani huyo anaetaka kukuua". "Jestina jamani" aliongea Frank na kuwafanya wenzake waanze kucheka, "wee hebu tuambie leo umekunywa ngapi" Jay aliuliza. "washkaji mimi sijalewa, amini msiamini nimemuona tena anatisha si mchezo" alijaribu kujitetea Frank lakini wenzake walizidi kumcheka. "oya hebu msindikize geto akalale kwanza labda pombe imepanda kichwani" Jay aliongea na watu wawili wakamchukua Frank mkukumkuku na kumpeleka chumbani. "oya dogo pumzika kwanza kesho asubuhi tutaongea fresh" James aliongea na kutoka, kwa bahati mbaya aliufunga mlango kwa nje.
Frank alijaribu kutafuta usingizi huku akijipa moyo labda kweli atakuwa kalewa lakini ghafla hali ya hewa ndani ya chumba hicho ilianza kubadilika. "ah hahahahahah......" sauti kali ya kicheko iliskika, "nisamehe Jestina, ujinga tu ulikuwa ukinisumbua" alianza kuomba msamaha. "hahahaha msamaha wako haukubaliki na leo utakiona cha moto" Jestina aliongea huku alizidi kutisha na kuanza kuangua kilio ambacho kilimbana na mruzi mkali uliopenya kisawasawa kwenye maskio ya Frank. Alianza kusikia maumivu makali sana, na damu ziianza kumtoka kwa wingi sana masikioni. "Jestina nakuomba unisamehe niko chini ya miguu yako" aliomba lakini ni kama alikuwa akiomba azidishiwe adhabu. Kwa makucha makubwa katika mikono ya Jestina alianza kumchanachana bila huruma, Frank alipiga sana kelele lakini hazikuskilikana kutokana na chumba hicho kuwa katika nyumba nyingine tafauti na ile waliokuwepo wenzake. Alikimbilia mlangoni kujaribu kujiokoa lakini wapi mlango ulikuwa umetiwa loki kwa nje. "unakwenda wapi unadhani" Jestina aliuliza kwa sauti nzito yenye mikwaruzo, wakati huu alikuwa kashaabadilika na kuwa katika mwili uliokuwa ukitoka funza wengi na wenye harufu kali sana ya kuoza. Harufu hio ilimfanya Frank anze kutapika, mpaka aliishiwa nguvu. Jestina alimsogelea alipo na kumshika koo na kuanza kuliminya mpaka kulinyofoa kutoka shingoni. Frank aliaga dunia huku mwili wake ukiwa hautaminiki, kabla ya kutoweka aliandika ukutani kwa damu "AMELIPA".
ITAENDELEA.
Nzuri
ReplyDeleteYour Thoughts