RIWAYA: JESTINA
MTUNZI: Tariq Haji
CONTACT: +255624065911
SEHEMU YA TISA
"James" Alwin aliita, alipogeuka akamuonesha ishara kwa kupitisha mkono katika shingo akimaanisha ni zamu yake usiku wa siku hio. Lakini alipotezea na kuondoka zake bila hata kugeuka nyuma, Alwin alirudi ndani moja kwa moja alikwenda chumbani kwake. "vipi wameshaondoka" Aliuliza Alwin, "ndio" alijibu Jestina akirudi katika umbo lake la kike. Huo ni mchezo wamekubali kuucheza huku Jestina akiitumia nyumba hiyo kama ngome yake na mtu yeyote atakaekuja kwaajili ya kesi yake basi hujibadilisha na kuwa Alwin. Na hicho ndicho alichokifanya siku ile alivyokuja Inspector Hans kwaajili ya mahojiano. Bado vifo vyote viwili vilibakia kuwa ni gumzo, daktari alieifanyia uchunguzi miili hiyo alikuja na majibu yale yale tu "yoyote aliefanya mauaji haya si kiumbe wa kawaida".
************************************
"Matt mwanangu kwanini uliamua kufanya ushenzi ule"
"Ah ni ushundani tu ndo ulionipelekea kufanya vile"
"sasa umeona madhara yake nimetumia mabilioni ya mapesa kuwahonga majaji na wanasheria waifute kesi ile"
"najua mzee, ila usijali kila kitu kipo sawa na muda si mrefu nitarudi nyumbani"
Hayo yalikuwa ni mazungumzo ya Matt na baba yake kwa njia ya simu, baada kufanya tukio lile ilibidi Matt asafirishwe na kesi ile iuliwe kwa aina yoyote. Sasa anataka kurudi akiamini miaka aliokaa nje ya mji wake ingetosha watu kumsahau na hata wenzake walikata mawasiliano nae kwa sababu aliondoka kimya kimya bila kuwataarifu wenzake chochote. Ni baada tukio lile alilomfanyia Jestina, Matt alisafirishwa na baba yake na kupelekwa Ufaransa.
"Baba naskia Alwin kapona" aliuliza Miryam, "ndio mwanangu kapona kabisa" Profesa Alexander Harison alijibu." Ah basi mimi namaliza mtihani wangu wiki ijayo baada ya hapo nitakuja, lakini usimwambie kitu Alwin" aliongea Miryam kwa furaha sana. Miryam hakuweza kuendelea kusoma Mashvile baada lile tukio na lilisababisha kifo cha Jestina pamoja na kichaa cha Alwin. Na baada baba yake kugundua hilo aliamua kumsafirisha kwa ajili ya kwenda kumalizia masomo yake nchini China na huo ndio ulikuwa mwaka wake wa mwisho wa masomo. Lakini haikupita hata siku moja bila kumuombea uzima Alwin.
Bado inspecta Hans alikuwa njia panda maana aliona kama Alwin anamchezea mchezo mchafu, baada kufikiria sana bila kupata majibu aliamua kwenda nyumbani kwa Profesa Alexander Harison kwa ajili ya kuripoti alichokiona. Safari yake ilikuwa ni ya dakika kumi tu, alipofika alikaribishwa ndani na kuomba kuonana na Profesa. Haukupita muda aliambiwa aingie katika ofisi, "samahani kwa kuja bila taarifa" aliomba msamaha kwanza, "bila samahani". "ukweli kuna jambo linatitaza, kwa sababu jana nilienda kuongea na Alwin lakini nilipokutana nae msibani alisema hanifahamu na wala hatujaongea kitu" alieleza, " wakati unaongea nae majibu yake yalikuaje" aliuliza profesa. "yalikua yenye chuki ndani yake na baadhi yalikuwa ya mkato" alijibu. "Alwin hana majibu ya mkato, ni kijana ambae majibu yake yanaheshima" aliongea profesa na kumshtua kidogo inspecta Hans ambae sasa alishaanza kuamini kama hakuongea na Alwin, sasa swali lilikuwa aliongea na nani kama si Alwin. "na kuhusu mauaji yanayotokea, mpaka sasa ripoti zinasema kuwa si ya kawaida" alijikaza na kuendelea kuongea. "naweza nikaziona picha za miili yao" aliuliza profesa. "ndio" kisha akatoa fail na kumkabidhi profesa.
Profesa aliziingiza kwenye mashine fulani hivi kama projecta na kuzima taa zote katika ofisi yake kusababisha kigiza fulani hivi, kisha akaiwasha ile mashine na zile picha zikawa zinaonekana ukutani. Lakini aliganda kidogo akiangalia alama za kucha katika miili yote miwili na kubaini kuwa alama hizo zimepigwa katika mtindo mmoja. Haraka alifungua droo na kutoa picha ya ile michoro alioandikwa Alwin kipindi ambacho allikuwa hayuko sawa na kuanza kulinganisha. "unaona kitu gani hapo inspecta" aliuliza profesa, "mi naona michoro tu" alijibu. "angalia kwa makini" alisisitiza profesa ndipo inspecta Hans aliposimama na kusogea kwenye ukuta na kuanza kuzichunguza kwa makini sana. Aligundua kuna maandishi fulani hivi lakini alishindwa kuyasoma
"naona kama maandishi hivi" aliongea inspecta. "ndio katika miili yote miwili kuna jina limeandikwa lakini katika lugha ya kale ya wenyeji wa Mashvile na jina hilo ni JESTINA" aliongea profesa na kumfanya Inspecta kutumbua macho kama mtu aliesakamwa na tonge la chakula kwenye koo. "unataka kunambia kuwa muuaji ni JESTINA au vipi" aliuliza kwa sintofahamu, "ndio inspecta muuajai ni Jestina, hivi umewahi kusikia kama kuna ulimwengu wa watu waliodhulumiwa" alijibu profesa na kuuliza. "ah mi hizo story huwa nazisikia tu lakini siamini kabisa" alijibu inspecta huku akitabasamu, "basi kuanzia leo ndio uamini kama kweli huo ulimwengu upo na mtu akifa kifo cha kudhulumiwa basi hupita hapo kwanza na hukaa kwa muda wa miaka kumi. ikiwa ndani ya kipindi hicho kutakuwa na mtu duniani ambae anaamini mtu huyo amedhulumiwa na haki haijatendeka basi hupata uwezo wa kurudi duniani kuja kuwalipa wale waliomdhulumu" aliongea na kufafanua Profesa "inspecta kazi yako imekwisha sasa kwa sababu hakuna utakalofanya kumzuia Jestina asilipe kisasi. Wewe kazi yako itakuwa ni kushuhudia tu mauaji hayo" aliongea profesa na kuonekana kama kufunga kikao hicho.
*****************************
Sauti za huba ziliskika ndani ya chumba kimoja katika hoteli kubwa katika mji wa Mashvile, "James niahidi kama utanioa".
"niamini wewe ni wangu na kesho nakupeleka nyumbani nikakutamblishe kwa wazazi wangu" James alijibu huku akionekana kunogewa na penzi la mschana huyo, ndani ya chumba hicho taa zilikuwa zimezimwa isipokuwa taa moja nayo ilikuwa ikitoa mwanga hafifu sana na kukifanya chumba hicho kipendeze. Kuna wakati James alifunga macho kwa raha alioipata, alipofungua alijkuta akimuachia mpenzi wake na kuruka pembeni. Hiyo ni baada kuona sura ya Jestina badala ya mpenzi wake, "James unanini mbona umenikata stimu" aliongea mwanamke huyo kwa kudeka. "ah hamna kitu" alijibu kwa kujibabaisha na kurudi kitandani ili aendelee na mchezo, wakati akiendelea kufanya hivo aliangalia dirishani na kumuona Jestina akimuangalia.
"mama" alipiga kelele huku akimsukuma mpenzi wake kwa nguvu na kusababisha ajigonge kichwa kwenye kona ya kitandana na kuanza kutoka damu nyingi na mwisho alitulia tuli. Kicheko kikali kiliskika na kufuatiwa na maneno "na bado utajuta kuzaliwa" kisha kimya kikatawala ndani ya chumba hicho. Alipoona hali imerudi kuwa ya kawaida alimsogelea mpenzi wake na kumtikisa lakini wapi, muda mrefu alikuwa kashapoa. Woga ulimpata na kuamua kuvaa na kuondoka eneo hilo na kuuwacha mwili wa mpenzi wake ukiwa umetapakaa damu.
Asubuhi mapema akiwa kwao, gari ya polisi ilifika na kuonyesha waraka wa kukamatwa James, hakukuwa na jinsi zaidi ya kukubali na kufikishwa kituoni. Alihojiwa kidogo lakini hakutaka kuonyesha ushirikiano, hivo ikatoka amri awekwe mahabusu mpaka atakapokuwa tayari kusema. Masaa yalikatika na hatimae usiku ulifika bila kukubali kuongea chochote. Akiwa kajilaza kwenye kigidoro kidogo, "James...James...hahaha" aliskia sauti ikimwita lakini hakumuona mtu. "Jestina dadangu naomba unisamehe, ujinga tu ulikuwa ukinisumbua" alianza kuomba msamaha huku akilowanisha suruali yake. "mpumbavu mkubwa wewe nani dadaako, kuna mtu anaeweza kumshika dadaake ili abakwe" Jestina alijibu kwa hasira na kumtokea mbele yake. "mamaaaa nakufa" James aliruka huk akipiga kelele, lakini ghafla Jestina akatoweka na kumtokea nyuma yake.
Aliinua mkono wake na kumtandika kucha za mgongo na kumfanya apige ukwenzi wa maumivu. Kwa kweli James alijua hicho ndio kiama chake maana kila alivojaribu kujitetea ni kama alikuwa akichochea moto. Jestina aliendelea kumrarua mpaka alipohakikisha amemmaliza kabisa, kuhakikisha haishi tena alikpiga kucha za koromea na kulikata. Kama kawaida yake aliacha ujumbe na kutoweka, siku ya pili asubuhi maaskari waliripoti kifo cha James. Wengi walishtuka hasa waliohusika kwa namna moja au nyingine katika kifo cha Jestina. Hali hiyo haikuwatisha wao tu bali mpaka watu wengine ambao hawakujua chochote juu ya matukio hayo. Kila kukicha vyombo vya habari vilitangaza mauaji mapya yanayofanyika hukua ikiaminika kuwa muuaji ni mtu ambae amebobea na anauwa kwa sababu ya kulipa kisasi. Kama kawaida inspeta Hans alirikodi tukio hilo katika mafaili yake na kuondoka. Sasa hakuumiza sana kichwa kwa sababu alishajua muuaji sikiumbe wa kawaida.
Upande wa Alwin hali yake ilizidi kutengemaa na sasa mwili wake ulishaanza kurudi na vidonda vidogo vidogo vilishaanza kukauka. Familia yake ilifurahi lakini haikuwa hivyo kwa familia ya Jestina ambayo bado walikuwa ni wenye majonzi sana hasa kwa kumpoteza mtoto wao pekee. Hilo lilimuathri sana mama yake na kupelekea baadhi ya wakati kuzimia kutokana na msongo wa mawazo. Hata baba yake pia ilimathiri na kupelekea kudhoofika kimwili japo si sana. Siku hiyo Alwin alipanga kwenda kuwatembelea ili kuwajulia hali, aliondoka kwao asubuhi mapema na kuelekea kwa Mr Hendrix. Alipofika alikaribishwa ndani vizuri na mfanya kazi kisha akaenda kuitwa Mr Hendrix. Alifurahi sana alipomuona Alwin na kumkumbatia "Mungu ashukuriwe kwa kukupa uzima mwanangu" aliongea huku akijizuia machozi yasitoke. "asante, habari za siku nyingi" Alwin aliuliza, "kama unavoziona mwanangu, kwa kweli tokea Jestina atutoke maisha yetu yamekuwa magumu sana sijui hata kwanini Mungu ametutenda kiasi hichi" Alijibu Mr Hendrix na wakati huu alishindwa kuyazuia machozi na kuyaacha yatiririke kuonyesha machungu alokuwa nayo.
"hapana mzee wangu usiseme hivo, Mungu hajawatenda ila amekupeni mtihani kama alivowapa wengine tu ili kukupimeni imani. Yeye ndie aliewapa Jestina na yeye ndie aliemchukua kwani kuna ubaya gani mtu kuchukua kilichochake. Nyie jueni tu kama Jestina amepumzika lakini hatopata amani ikiwa bado mtaendelea kumlaumu Mungu kwa kifo chake" Alwin aliendelea kumliwaza Mr Hendrix ambae alikuwa akilia kama mtoto mdogo.
"mwangu we huujui uchungu nlokuwa nao, kifo cha Jestina kimepelekea mpaka mamaake kupata maradhi ya kuanguka. Ukweli Alwin naogopa kumpoteza mke wangu" Alwin alivyosikia hivo alishtuka kidogo na kuomba kwenda kumuona. Bila kinyongo Mr Hendrix aliongozana nae mpaka chumbani, alimkuta akiwa amelazwa huku akiwa amewekwa drip. Alwin alisogea mpaka pembeni yake na kukaa kwenye kiti "habari yako mama" aliongea kwa sauti ya chini. "nashkuru sijui wewe Alwin" alijibu mama huyo japo kwa tabu kidogo. "pole kwa yote yaliotokea",
"asante mwanangu, kwanini lakini" alijibu huku akilia. ""pole kwa yote yaliotokea", "asante mwanangu, kwanini lakini" alijibu huku akilia. "yote ni kazi ya Mungu na kama tunavojua kazi ya Mungu haina makosa cha msingi mamaangu kukubaliana kama Jestina hayupo tena nasi" Alwin aliongea huku akimshika mkona mama Jestina kwa ajili ya kumliwaza.
ITAENDELEA
Your Thoughts