SIKU ISIYO NA JINA SEHEMU YA NANE

SIKU ISIYO NA JINA

Na: Emmanuel Charo

WhatsApp: +254796273110


Sehemu ya Nane


Ilipoishia sehemu ya Saba

'jaribu, Angel yuko mikononi mwa mwehu'

'usijali analindwa na Risasi Tatu huyo'

'bro yuko mikononi mwa Abdul'

'Abdul ndio nani huyo'

'fanya kumtuma utajua baada ya ametoka mikononi mwake'

'huwaamini Risasi Tatu ama'

'bro ungejua moto wa huyo kiumbe anaitwa Abdul, ungehofu hata kumtuma huyo jini, nakushauri wambie hao Risasi Tatu wasitishe zoezi lao maana ni hatari kwao'

'haiwezi wapo Urusi hadi hivi tunaongea'

'wambie wasitishe zoezi la kumfuatilia huyo mtu'

'duh! Sawa acha niwafahamishe'

'fanya hivyo hii misheni ni nzito hawawezi kile kiumbe'

'ni sawa lakini misheni si kudili na huyo kiumbe bali ni kumlinda Angel'

'Abdul atawamaliza akigundua anafuatiliwa'


*******

Endelea sehemu ya Nane


"Unaikumbuka safari ya Kwa museveni?"

Adrian alishtuka kuulizwa swali hilo na mtu aliyejitambulisha kama Romeo

"Naikumbuka" Kwa kinyonge na sauti hafifu alijibu Adrian 

"Kama unaikumbuka mbona ushinde ukiuliza Kwa nini uko hapa"

"Sasa safari ya Uganda na hapa uhusiano uko wapi"

"Kijana Eddy siku zote mie husema siasa mchezo mchafu, nilipokuuliza ulishtuka dhahiri, maana wewe ulijua ni siri sio"

"Nyie mbona wehu"  sauti ya kinyonge ya Adrian ilipotea ghafla na kuwa ya kikakamavu na iliyoonyesha hasira ndani yake

"M'meshinda kuniweka hapa hamsemi mnataka nini kwangu"

"Relax ndugu, ninachotaka ni wewe kuwa hapa hadi huyu akamilishe Kazi yake"

Kwa mara nyingine tena Adrian anaonyeshwa mtu aliyefanana na yeye


******

Willy Baro, baada ya lalama nyingi kutoka Kwa familia ya Frankoo Sari aliidhinisha kufanyika Kwa upasuaji wa mwili wa marehemu kufahamu fika kiini cha kifo chake. 

Hili linatukia baada ya mchezo wa paka na panya kati ya polisi na mshukiwa mkuu wa mauaji, mchezo huo ni kama panya anatawala himaya ya paka inashangaza! Na eti sikuwa paka ameondoka la hasha panya anachezea masharubu ya paka hasa maajabu! 

Waliopo usiku wa giza wanasema huenda panya anakula meza moja na paka wakiwa faraghani ilihali wakiwa kweupe ndio huvaa upaka na upanya kuaminisha wanyonge, hizo ni semi za walio gizani.

Kunao waliobarikiwa na wapo kwenye nuru muda wote wanajua kijana wa watu aliangushiwa jumba bovu kama si kugongwa kichwa na yai viza, halafu kuna wale wasio jua kunaendelea nini.

Wengine wanasema kesi ipewe Mzee lumbwi aitatue, lakini ya Mzee lumbwi heri mchezo wa paka na panya uendelee maana kwake mnyonge siku zote hana haki. Hawa wa Mzee lumbwi ni kama hawajui vitimbi vyake, yote tisa kumi kila mtu hakosi la kusema


Familia ya mwendazake Frankoo Sari, ilifika asubuhi na mapema kwenye hospital kuu ya mkoa wa pwani almaarufu makadara kushuhudia zoezi Hilo muhimu kugundua kiini hasa cha kifo chake.

Familia yenyewe ilikuwa na mvutano, wengine waliona ni kupoteza muda maana wanajua alikufa Kwa kupigwa risasi hivyo hawaoni umuhimu wa zoezi Hilo.

Nuru pia alisafirishwa toka mariakani ili pia ashuhudie zoezi hilo.

Kwa jumla waliingia watu kumi ndani ya kile chumba akiwemo Nuru, mamake, ndogo wake Nuru Kwa Jina Nusra yupo kidato cha tatu, wanausalama watatu ambao kazi yao ilikuwa kumdhibiti Nuru maana alikuwa bado Yuko kizuizini na wataalamu wakufanya shughuli hiyo.

Nusra alishangazwa na udogo wa chumba hicho na vifaa alivyokuta ndani hamkai hospitali hasa

"Mmmh" aliguna

"Dogo ni nini" Nuru alimuuliza ndogo wake

"Nadhani chumba sicho hiki"

Nuru Kwa kidole alimuonyesha ndogo wake waandishi wakubwa yaliyokolezwa weusi 'POSTMORTEM ROOM'

"Mmmh" aliguna tena 

"Wanangu na mshauri muende nje tu si vyema kuona nyeti za baba yenu japo kafa"

"Labda ndogo wangu hapa aende nje lakini mimi.."  alisita kidogo na kumfuata mamake na kumunong'onezea sikioni.

"Ni sawa" mama yake alijibu.


"Mko tayari, nawaomba mjikaze Kwa mtakayoyaona kwenye zoezi hili,kama ushawahi shuhudia ni sawa kama bado na roho yako ni nyepesi nakuomba Kwa taadhima utoke nje"

Alisema kiongozi wa ile shughuli

Hakuna aliyetoka.


******

Angel alizinduka kabla ya kufikia hospitalini, uelekeo ukabadilika na kuelekea hotelini.

"Tatizo nini Mpenzi" aliuliza Abdul 

"Nani Mpenzi wako, na ukome kuniita Mpenzi"

Angel aliinuka toka pale kitandani na kuelekea mlango ulipo.

Abdul alitabasamu tu, Angel aliufikia mlango na kugundua umefungwa alijaribu lakini wapi alimugeukia Abdul 

"Tafadhali sana nakuomba ufungue mlango nitoke"

"Angel si rahisi namna hiyo, sijui yule kikaragosi wako akisikia uko na mimi ataamini kweli, anajua tuliyamaliza. Hivi sasa wewe ni mateka wangu, hauendi popote pale."

Kisha alimfuata Angel alipo na kumshika Kwa nguvu na kumvuta na kumrusha kitandani

"Nisikilize mrembo mimi ni mtu mzuri ukifuata maelekezo yangu na pia ni m'baya ukienda kinyume na matakwa yangu"

Angel alibaki kimya na kuonyesha uwoga waziwazi na machozi yalianza kulowanisha mashavu yake.


Abdul alitoa sigara na kuiwasha na kuvuta Kwa sekunde kadhaa, Kwa mwendo wa aste aste alitembea hadi Kwa dirisha na kutoa moshi kupitia mapua na kinywa chake, Kwa mwendo huo huo alirudi na kukaa pembeni mwa Angel, na kuanza kuzishika nywele zake laini, Kwa kutumia kiganja chake na Kwa utaratibu alimfuta machozi. Abdul naye akajilaza pembeni mwa Angel,

"Kiapo changu kinanitesa, sikujua Manu atakuwa na mke mrembo kama wewe"

Angel aligeuza kichwa na kumtazama Abdul ambaye naye Aligeuza kichwa na macho yao kugongana, bado Angel alikuwa analia

"Ninja atabaki kuwa Ninja siku akiwa samurai ni tetemeko la dunia"

"Sikuelewi unaongelea nini" alisema Angel

Abdul aliinuka na kumuinua Angel kisha akamshika mikono

"Uzuri ilikuwa maelezo haya uyapate toka Kwa Yule kiumbe"

"Kiumbe yupi huyo"

"Mumeo, Manu"

"Manu si mume wangu"

"Kweli! Si mumeo hadi namaliza kukusimulia upande wangu utajuta Kwa nini ulifahamiana naye"

"Unanitisha"

"Sikutishi ila na amini baada ya simulizi hii utakuwa mfu"

"Mimi tayari ni mfu"

Abdul alisafisha koo lake.


"Uko tayari kumjua Manu ni nani, Una roho ya kubeba taarifa nzito nzito au wewe ni lege lege, unasikia Manu kauwa unachanganyikiwa"

"Nambie basi acha kupoteza muda"

"Ok ni sawa"


*******

"Mkuu bado upo kumbe"

Ujio wa Henessa Mafaa pale makadara ulishangaza wengi maana walijua ameenda ziara nchini Urusi.

"Bado nipo, shughuli vipi imeanza au bad..." 

Maongezi yao yalikatishwa ni Nusra aliyekuwa akiangua kilio kutoka chumba kilichokuwa kikifanyiwa upasuaji wa mwili wa Frankoo Sari

"Heshima yako mkuu" mwanajeshi alemsindikiza Nusra alimpigia salute Henessa

"Vyereje"

"Binti hajazoea haya mambo, alikuwa anazua zogo eti babake anafanyiwa unyama"

"Maskini ni kweli wanayasikia tu wakiyaona hawaamini"

"Acha nirudi ndani maana kuna Yule mwehu"

"Twende sote"


Moja, mbili walijikuta ndani, upasuaji ulikuwa ukiendelea vyema, macho ya wanafamilia yalikuwa mekundu na mashavu Yao yakilowa machozi waliyokuwa wakitoa kimya kimya

Mwili ulitolewa risasi tisa kifuani upande wa kulia, na kipande cha kisu chini ya kitovu, vyote viliekwa kwenye mfuko maalumu Kwa uchunguzi, mwana pathologia alikuwa amekamilisha kazi yake lakini Henessa akaamuru Ampasue bega lake la kushoto, bila hiyana alianza kazi hiyo, aligundua kuna uvimbe mahali hapo.

Kwa umakini alifuatilia uvimbe huo na kutoa kalamu maajabu!

Kalamu hiyo haina tofauti aliyokabidhiwa Henessa kule Palestina, muundo ni huo huo iliyokabidhiwa Joan ampe Angel.


Mtaalamu alitaka kuieka kwenye ule mfuko maalumu alipoeka zile risasi na kile kipande cha kisu lakini Henessa aliamuru apewe.

Nuru alipinga jambo lile, lakini Kwa kuwa mtaalamu anatambua cheo cha Henessa, alisafisha kalamu ile na kumkabidhi Henessa.

Henessa baada ya kupewa kalamu ile alianza kutoka na kumkonyezea Nuru


********

"Unaiona hii" Abdul alimuonyesha kalamu Angel, Angel alishangaa kuona kalamu aliyokabidhiwa ni Joan ipo mikononi mwa Abdul, hakuamini kwa Kasi ya ajabu aliinuka na kuufukia mkoba wake na kufurukuta cha kushangaza akaikuta kalamu ile ipo salama salimini.

"Wow the show is about to begin" alisema Abdul baada ya kuona Angel pia yuko na ile kalamu.


Itaendelea 


Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Your Thoughts