Katika pitapita zake za mtaani...Sungura kaamua kuingia dukani na kuuliza ..
"Mna karoti hapa?"
wenye duka wakamjibu.."wala hatuna karoti"...Sungura kaamua kusepa zake.
Siku ya pili Sungura akarudi tena pale dukani na kuuliza tena..
"Mna karoti hapa?"
Wenye duka kwa ukali wakamjibu Sungura..."Hivi wewe...si tulikwambia hatuna karoti na wakati mwengine ukirudi hapa tutakugonga misumari ya kichwa kwa nyundo wewe endelea kusumbua tu!!..
Siku ya tatu Sungura akarudi pale pale dukani n kuuliza...
"Mna misumari hapa?"
Wenye duka wakajibu.."Hapana wala hatuna misumari"
Kisha Sungura akauliza..."Na nyundo je? " Wakamjibu "wala hatuna nyundo"
Kisha kwa upole Sungura akauliza "Mna karoti hapa?"...
MWISHO.
Your Thoughts