Kongole nakupatia, yangu mama kunizaa
mengi ulivumilia, kiwa ndani 'janizaa
'jua mengi mepitia, 'ngine ata kulalaa
Nani kama yangu mama, lenileta duniyani.
Tumboni mimi mtundu, mateke kurusharusha
La kujali 'ngu utundu, kamikali hukurusha
ngozi chanika ja tandu, kliniki di Arusha
Nani kama yangu mama, lenileta duniyani.
Miezi tisa mefika, tumboni nafaa toka
chakula, hewa dimika, kama paka natoroka
'je kafa njaa kichaka, lihali homu 'sabika
Nani kama yangu mama lonileta duniyani.
kichwa kilivyotokea, manesi wanitazama
nilishindwa jitetea, nesi nivuta lazima
sijui wake potea, labda ni kuzima
Nani kama yangu mama, lonileta duniyani
limsikia kilia , kwa uchungu ja mtoto
badae alitulia, nesi beba maji moto
damu lokuwa oshea, pia palopita toto
Nani kama yangu mama, lonileta duniyani
Nyumbani mwangu mwa kwanza, likuwa tumboni mwake
Chakula changu cha kwanza, likuwa maziwa yake
Gari lomiliki kwanza, likuwa mgongo wake
Nani kama yangu mama , lonileta duniyani.
Yeye lala bila kula, hezi niacha bila nyonya
ikifika ni kulala ,, nikumbata bila mwanya
pwagu sije kiholela, mtoto kumpokonya
Nani kama yangu mama, lonileta duniyani
Leo hii nimekua, natambua lopitia
'ta niwe milionea, sezi kulipa fidia
wazimu nikaribia, kijaribu kadiria
Nani kama yangu mama, lonileta duniyani.
Udaktari nasoma, ili nikutunze mama
kuepushe na ulema, sije shindwa kusimama
digri na diploma, nipe dua zako mama
Nani kama yangu mama, lonileta duniyani.
Created by Chonga254
Your Thoughts