NAISMA MWISHO

 NAISMA SEHEMU YA MWISHO

Mtunzi: Zamrata Mbwana

No: +255698095257


Mda ule Haidary Frut alivyokuwa anamkimbilia Recho Ndo mda huo huo . Naisma akawa anaenda Ofsini kwa Haidary Frut ivyo aliona awafatilie kwa Nyuma


Basi Recho alikimbilia Kwenye Gorofa lililoko jilani na Hapo lilikuwa alijaisha vizuri alikimbilia juu kabisa   ya Gorofa ilo uku machozi yakimtoka 


"Recho !! Usifanye Ivo nakuomba !


"Apana ! Haidary Bora nifa tu Mimi Sina thamani yeyote kwako Baki Na Naisma wako !!!!


Recho aliongea maneno Ayo nakujiandaa kujitupa  . Haidary alimkimbilia Na kumshikilia kwa Nguvu 


"Apana Recho usifanye Ivo Wewe unasamani kwangu na sipo tayari kukupoteza !!!


Recho alivyo sikia Ivo alimkumbatia Haidary Frut kwa Nguvu Na akaanza kumbusu 😘


"Nakupenda ! Haidary je na Wewe? Unanipenda?


Recho alimuuliza Haidary Frut uku akiendelea kumbusu . Haidary alitulia tu hakutaka amuuzi lafiki yake 


Mda uwo uwo Naisma aliwasili Pale ila Haidary Na Recho hawakumuona walikuwa wanangaliana usoni.


Naisma alivyoona Recho anambusu Haidary na Haidary Frut katulia tu akajua Basi . Kila kitu kishaisha ana lake Tena pale


Alikimbia uku machozi yakimtoka .


"Basi ! Recho tuludi Ofsini usifanye Ivo ! Sikunyingine ! Sawa ?


Recho alitikisa kichwa ishara ya kukubali Na waliludi Ofsini 


"Naisma ! Naisma !!!!!


Novo berry alimuita Naisma Baada ya kukutana nae akiwa analia 😭 


Lakini Naisma akujibu kitu alienda kuchukua mkoba Wake Na kuondoka zake


"Mh !


Mda huo huo Tina alikuja pia baada ya kumuona Novo kasimama kwa kuduwa 


"Vipi ? Mwenzetu ! Mbona umeganda kaa sanamu ?


"Khe ! Shosti Naisma!


"Naisma ? Kafanyaje ?


"Yaani katoka uko analia namuuliza ajanijibu kaenda kuchukua mkoba wake uyo kaondoka zake ! 


"Khe ! Kumbe !  


Mda uwo uwo Haidary Frut na Recho waliingia Na Recho alikuwa anafuta futa machozi ishara ya mtu aliye kuwa analia 


"Aaaanhaaaa!!! Ndiyo maana Basi nishapata jibu !


Novo berry aliongea ivo na Tina alimgeukia na yeye pia aliwaona 


"Aaah ! Novo utanisamehe Mimi siwezi kukaa kimya !


"We ! Tina ? Unataka kumfanya Nini !


Novo berry aliongea kwa kunong'ona uku akimshika mkono Tina .


Haidary alipita Pale na Tina 


"Haidary ! Subili !


Haidary Frut alisimama na Recho  nae alisimama 


"Kwani kimetokea Nini ? Mbona Naisma kaja analia . Alafu nyie pia mnatokea uko !



"Eti !!!!! 😳 Nini ! Nai. Yupo wapi ?


"Ameondoka !


Haidary Frut alitoka Mbio mda huo huo . Kumfata mkewe Naisma


Recho alibaki pale. Na Kina Tina 


"Loh ! Mwanamke ! Shetani wewe Yani unataka Adi uhakikishe wanachana wenzio ! 👌Msiuuuuu 


Tina aliongea Ivo nawakaondoka zao ......


🖤🖤🖤


Naisma aliludi kwao uku akiwa analia 😭 alifika Sebleni Na alimkuta Mama yake anangalia TV 


"Mama !!!!


Alifika na kumkumbatia Mama yake uku akilia .


Mama yake alishtuka Sana akamuita Baba yake na mdogo wake Jasmini .


"Mimi sijui !  Amekuja nakuanza kulia ! 


 "Baba ! Nimemkuta Haidary akiwa Na Recho wakiwa wanabusiana !


"Oooh!!! Mwanangu uliwakuta katika mazingira Gani ?


Naisma alielezea yote Alivyo wakuta Haidary Na Recho 


"Okay ! Binti yangu ! Ila ungechunguza kwanza au ungemsubili mwenyewe Haidary umuulize !


"Apana ! Baba toka mda Ni liwahisi Na leo nimesibitisha !


"Mh ! Sisi atuwezi kuwaingilia mahusiano yenu !!!!


Baba Naisma aliongea Ivo Mara Mda uwo uwo Haidary alingia Ndani na kukuta Familia yote ipo pale 


Naisma Alivyo muona tu . Haidary Frut aliinuka nakukimbilia chumbani.


"Naisma ! Naisma ! 


Haidary Frut alimfata Nyuma uku akimuita Na walifika chumbani


"Mke Wangu Naisma !


"Nyamaza tu ! Haidary Aina haja yakujikomba kwangu nimeona kila kitu mlichokuwa mnakifanya Wewe Na uyo Recho wako !


"Apana ! Naisma sio ivyo ulivyo elewa wewe ni !


Haidary aliongea kwa kumbembeleza mkewe Naisma ambae alikuwa anahasila mno hakutaka kuelewa chochote kwa mda ule


"Niache Haidary ! Inatosha umenizalilisha vya kutosha yaani ! Yaani ! Nilikuwa sahihi kipindi kile kukukataa ! Najuta Mimi Naisma !


Naisma aliongea uku akilia nakujishika kichwa . Haidary alimkumbatia Naisma .


"Apana Haidary ! Niache 


Naisma aliongea Na kumsukuma kwa Nguvu .


"Yaani umenizalilisha unajifanya Recho Rafiki ako kumbe Ni mwanamke wako ! Yaani simtaki kumuona ata uyo Recho apa ! Ni bora tuachane tu leo leo kila mtu na Hamsini zake uende uko ukakae Na uyo Recho wako !


"Khe !  Naisma Ndo umefikia uko mke Wangu ! 


"Sitaki ! Uniite mkeo kuanzia Sasa na Naomba Talaka yangu !


"Jamani ! Naisma Basi Nisamehe mke Wangu !


Haidary aliongea Na kupiga magoti uku machozi yakimtoka 


"Sitaki ! Nipe Talaka yangu Sasa ivi !


"Jamani ! Mbona utaki kuwa muelewa ! Naisma Basi kuwa ata Na Roho ya uluma au kumbuka ata Yale mazuri niliokufanyia ! Wewe mbona nilikukuta mala kibao tu Na Lamek ! Na sikukumu vibaya na zamani alikuwa mtu wako !


"Sitaki ! Ngonjera zako Haidary ! Naomba Talaka yangu !!!!


Haidary alikaa kimya kwa mda 


"Okay ! Si umezamilia kuachana Na Mimi Naisma !


Haidary aliongea uku akimuangalia Usoni Naisma Na machozi yakimtoka 


"Ndiyo ni kheri tuachane tu ! 


"Sawa! Ila Mimi sikutaka mapenzi yetu yaishie ivi Ila Wewe Ndo umetaka !


Haidary aliinuka Na kwenda kabatini Na kuchukua Nguo Zake kazaa Na aliondoka zake 


"Haidary !!!!! Unaenda wapi !? Sasa mbona unijibu !?


Haidary alitoka Pale alipita sebleni bila kusema chochote alivyofika nje alikutana Uso kwa Uso na Recho 


"Haidary ! Mbona mabegi unaenda wapi ?


Haidary Frut akujibu kitu zaidi machozi yalimmwagika tu


"Khee ! 😳


Recho aliingia Ndani alisalimia na kwenda chumbani alipokuwa Analala na Alichukua vitu vyake vyote pamoja na Nguo Zake .


Kiatu . Recho akaondoka zake 

"Yaani ! Ningendelea kukaa pale Naisma atanigeza Supu ...  !


Recho aliwaza akiwa Ndani ya Gari Na alienda kutafuta Chumba Na kupanga uku akiwa anaendelea kwenda kazini Kama kawaida .......

☘️


"Khe !! Kwaiyo Adi leo hamjui Haidary Frut yupo wapi?


"Ndiyo ! Novo alichukua mabegi Na kuondoka zake !


"Khe ! Au kaamia kwa yule ibirisi ! Mchawi mweusi Yule 👌 


Mda uwo uwo Recho alipita Na alikuja kukaa pale chini 


"Samahani ! Naisma nimewasikieni yote mliokuwa mnaongea Na wenzio !


"Kwaiyo ! Kama umesikia unataka uje kutupiga !👌 


Recho aliongea Na Tina akamjibu 


"Jamani Mimi sijajakishari Ila Naomba tu ! Mnisikilize jamani ! Naisma ! 


"Okay ! Ongea nakusikiliza ! 


Naisma alijibu kwa Nyondo


"Kwanza ! Samahani Naisma najutia makosa yangu Adi hii leo ! Kwanza Mimi sikai Na Haidary Kama mnavyo zani nyinyi Na Mara ya mwisho Ni siku alioondoka Na Mimi Ndo siku iyo ya mwisho kumuona Haidary Na Akunambia chochote ata nilipo muuliza ! Ni makosa yangu Adi leo sijui lafiki angu Haidary alipo enda ! Sikuile Mimi Ndo nilifosi kumbusu baada ya kuona nataka nijiue lakini hakuwahi kuwa Na hisia na Mimi alinichukulia Kama Lafiki tu ! Naisma ? Haidary anakupenda Sana Tena Sana kuliko unavyo fikiria Wewe na Hajawahi kukusaliti na Wala hakuwa mtu Wangu !


Recho aliongea uku machozi yakimtoka . Wote waliguswa . Naisma machozi yakimtoka Na alianza kulia kwa uchungu alimkumbuka siku ile alimbembeleza Sana amsamehe japo kosa alikuwa lake. Naisma alilia kwa uchungu Na walianza kumbembeleza wenzie 


"Sasa atakuwa wapi? Haidary Wangu ! Je Kama atakuwa ameenda kujiua je ? Aaaaa!!!!!!


Masiku yalikatika . Na Recho aliondoka Aliludi Kwao Mwanza Na Naisma aliendelea na maisha yake alimtafuta Haidary lakini hakumpata akaenda kumuuliza Hadi mdogo wake Fahadi nae akasema ajui alipo Haidary Frut.


Masiku yalivyozidi kwenda Naisma alijiona yupo tofauti mwilini mwake Na baadhi ya vyakula akila alitapika . Alivyoenda kupima akaona Ni mjamzito . Aligundua ni ya Haidary Frut alifurahi Sana Na alitmani Haidary Frut angekuwepo...Familia  yake ilifurahi Sana ilivyopata Taarifa iyo Na mimba ilikuwa Na ulifika Mda wa kujifungia akajifungua mtoto wa kiume aliitwa Samiri alifanana Sana na Haidary Frut. Masiku yalizidi kukatika Na mtoto alifika miaka miwili . Na Naisma alinza Kwenda kazini .....


💟


Tina siku ya mapumziko ya jumapili akiwa ananunua mahitaji yake super market   alishangaa kumuona Haidary Frut akiwa kavalia suti alipendeza Sana na yeye alikuwa anafanya manunuzi 


"Khe ! Haidary Frut !!!!!!!


Tina aliongea Na kumkimbilia Yule Kaka . Na alimgeukia 


"We !!!!! Haidary Frut ulikuwa wapi mbona uonekani unatafutwa pia mkeo Naisma anamtoto wakiume umefanana nae Hatari !!!!!


"Samahani ! Dada sijui unaongea kuhusu Nini ? Na huyo Haidary Frut Ndo Nani ?


"Kheeeeee 😳 !!!! Inamaana Ndo watu wawili wawili kiasi hiki ! Aya samahani !!!!!


"Okay !!! 


Yule Kaka aliondoka zake na Tina alibaki kuduwaa tu 


Siku iyo walienda kazini na ulikuwa Mda wa Lunchi


"Yaani ! Nyie  Haidary Frut yupo mzima kweli mbona Hadi leo aonekani !?


Novo berry aliuliza uku wakiendelea kula 


"Yaani Ana Roho ngumu ! Kama yupo Hai mbona adi leo ajaludi kumuona mwanae ! Jamani 


"Enhe !!! Nimekumbuka nyie Jana nimekutana Na mtu amefanana Na Haidary Frut vibaya ! 


"Haidary Frut!!!!!!!!


Novo berry pamoja na Naisma walishangaa Sana


"Jamani ! Sio Haidary Frut nilimfata akakataa !


"😢 Da !!! Sasa Haidary Wangu atakuwa wapi ? Hadi leo !!!


"Sikieni Tina Na Naisma aijalishi uyo atakuwa Haidary Frut au sio Lazima tukutane nae uso kwa uso !!!!!


...........🍂🍂🍂🍂


Siku iyo walitoka kazini na walielekea ufukweni mwa bahari wakiwa wanatembea tembea wakakutana Na Yule Kaka ambae kafanana Na Haidary Frut 


Walishangaa Sana Na walimuita kumuliza . Naisma alianza kulia mbele ya Yule Kaka


"Sasa ! Haidary atakuwa wapi jamani !!!


Yule Kaka alitoa Leso yake na akampa afutie machozi . Naisma alishindwa ata kusimama alilia Sana


💝💝💝💝


Naisma alipoteza Furaha Alijua Haidary Frut atakuwa kashakufa na ata kazini hakuchangamka kabisa Mda mwingi alikuwa anajitenga tenga tu alimisi Haidary Frut Na upweke ulimtawala


"Mh! Tina tutampoteza uyu shoga ako ivi unajua ayupo Sawa ! Kabisa uyu!


"Nikweli Novo ! Sasa tutafanya Nini ? Unafikiri bora tungejua uyo Haidary Frut ! Yupo wapi ? Atujui 


"Da !!!! Huu mtihani mwanzo alikuwa analinga amtaki Haidary Frut Asaivi kikowapi alishazoea ! Haidary Frut anaenda kumbembeleza Yani Kama Yule Kaka ni Haidary Frut kweli Na amekataa tu kumkomesha Naisma Basi kamuweza kweli kweli Yani !👌


Tina alimalizia kusema Ivo nakuchukua Juice 🍹 nakunywa 

.🦜


Naisma siku iyo akiwa Na Familia yake . Weekend wakiwa Na watoto wao Samir Na Abduly mtoto wa Mdogo wake Jasmini 


Walisikia Honi ya Gari na alieingia Pale walikuwa watu wawili Yule Kaka aliefanana Na Haidary Na mdada alikuwa mkubwa mkubwa kidogo ...


Walikalibishwa Na walikaa  


"Haidary !!!! Kalibu Nyumbani !!!!


"Asante ! Baba !


Naisma alibaki kushangaa uyu Kaka sindio Yule aliekataa kuwa yeye sio Haidary Frut . Sasa mbona Baba yake anamuita ilo. Jina Na anakubali 


"Sa.sa.samahani Wewe sindio Yule Kaka uliosema sio Haidary Frut ? Au !


Naisma aliuliza kwa mshangao na wote walibaki kimya 


"Mh ! Kwanza nitangulize Samahani ! Wazazi Wangu pia ata kwa Naisma ! Nisamehe ! Naisma kweli ! Mimi Ni Haidary Frut ! Samahani kwa kukuongopea !


Naisma alianza kulia 


"Nakwanini Haidary ! Ukaamua kuniongopea !


"Ndomana nikatanguliza Samahani ! Naisma nilifanya vile kwa sababu ya tulivyoachana Mara ya mwisho ! Ukutaka kunisikiliza hata kidogo Naisma ! Ivyo nilienda mbali Sana mkoa wa Iringa Na Simu Raini niliivunja kwa hasila baada ya kufika uko !


"Samahani! Baba uko Iringa Ni kwanani !?


Baba Naisma alimuuliza Haidary Frut.


"Iringa Ni kwa Mzee mmoja ambaye nilimfahamu Baada ya kuja kununua matunda. Kipindi kile ambacho nilikuwa nauza matunda alivutiwa Na Mimi na aliniita mwanae . Lakini yeye anakaa Iringa alikuwa akija uku Basi anakuja kwa mwanae. Mwanae mwenyewe Ndo uyu Dada niliekuja nae Hapa . Nilienda Iringa na nilimsaidia Sana Yule Mzee katika mashamba yake kuanzia kulima Hadi mazao na alipata mazao mengi Sana ! Ndipo alipovutiwa zaidi Na Mimi na kuniuliza Kama nimesoma . Nikamuelezea elimu yangu ndo akanambia ataongea Na Binti yake ataniajili nae anakampuni yake ! Basi nilipanga nikae mkoani ilinga lakini nikamkumbuka Naisma ! Nikasema nitaludi kwa ajili yake ! Sikujua Kama nilimuacha Na mimba . Na nilivyoludi nilikataa sio Mimi kwasababu sikutaka kuja kulupu labda angekuwa kashaolewa Naisma ! Nikaona nichunguze Kwanza Na leo nimeludi Hapa Naisma kwa ajili yako  ! Naomba unisamehe Naisma bado Nakupenda !


"Apana ! Sipo tayari ! Kukusamehe Haidary ! Yote alionifanyia kujifanya sio Wewe ! Eti na bado nikusamehe ! Hapana !


Haidary Frut aliongea akiwa kapiga magoti Na kulia kwa uchungu


"Okay ! Sina sababu ya kuendelea kuishi Kama unitaki ! Naisma nimekwambia nimeludi kwaajili yako 


"Dada Naisma ! Msamehe shemeji 


Watu wote walimsihi Naisma lakini hakukubali .  


Haidary Frut aliinuka Na kumchukua . Mwanae Na kumbusu uku akilia kwa uchungu 


"Nisamehe Mwanangu !


Haidary Frut alisema kauli iyo iliyomshtua kila mtu Pale


Haidary Frut alitoka nje bila ya kusema chochote kile 


"Dada Naisma ! Je Kama Haidary akienda kujizulu kisa Wewe !


Hapo Ndipo kauli iyo ilimshtua. Naisma Na kuinuka Mbio kukimbilia Haidary Frut ambaye alikuwa kashafungua Geti ili aondoke Zake 


Haidary !!!!!!!!!!!!!!


Haidary aligeuka nakumuangalia Naisma uku akilia . Naisma alifika Pale nakumkumbatia Haidary Frut kwa Nguvu !


"Nakupenda ! Haidary Wangu usiniache !!! Nakuomba !


Haidary Frut hakuamini kauli iyo Kama anatamka Naisma alifurahi Sana wakakumbatiana kwa Furaha Na mabusu . Na walishikana mikono wa kaludi Ndani.......🙏 


MWISHO

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.